by Jean Damascène Hakuzimana

Mnamo Novemba 4, Waziri mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopia aliamuru shughuli za kijeshi dhidi ya mkoa wake wa kaskazini wa Tigray ambao unapakana na nchi ya Eritrea. Mashambulizi ya serikali ya shirikisho dhidi ya hamura ya makombora ya Tigray na vifaa vizito vya uhifadhi wa silaha katika eneo la mji mkuu wa mkoa wa Mekelle unaanzisha kuongezeka kwa hali ya hofu inayoweza kuzorotika na kuchochea mzozo ndani na nje ya Ethiopia, hata kusababisha janga kwa pembe ya Afrika .

Waziri mkuu Abiy Ahmed ameelezea mgomo huo kama mashambulizi ambayo anaahidi kuendelea ya kujihami dhidi ya wanajeshi wa Tigray walioshambulia majeshi ya serkali ya shirikisho. The Telegraph imeripoti kuwa karibu askari 100 wa serikali wanatibiwa kwenye tovati kwa majeraha ya bunduki, wakati kesi za walio hali mahututi zinakimbizwa na ambulensi kwa huduma za kiafya katika mkoa wa Gondar.

Serikali imetangaza hali ya dharura huko Tigray na imepiga kura mahali hapo kushikilia ufadhili wa kifedha kwa mkoa. Kwa kukamata udhibiti na kupunguza uhalali wa uongozi ,wabunge wa shirikisho wameidhinisha serikali ya mpito huko Tigrey.

Muungano wa Tigrey Revolution Front [TPLF] na Abiy Ahmed wana historia ndefu katika miaka ya 1970’s muungano huo na miungano mingine, iliungana kuuangusha utawala wa Mengistu.Hatimaye walimpindua miaka ya 1990’s. Chama kimoja, Eritrea Peoples Liberation Front (EPLF) ilitangaza uhuru wa Eritrea. Baadaye Tigray peoples Liberation Army ilichukua uongozi wa miungano iliyosalia pamoja na kiongozi wake Meles Zenawi akawa waziri mkuu wa Ethiopia nafasi aliyoishikilia kwa miaka 20. Akiwa uongozini, serikali ya Tigrey iliyatenga makundi ya makabila mengine jambo ambalo lilileta wasiwasi dhidi ya serikali na kutengeneza njia kwa Abiy Ahmed wa kabila la Oromo kushika hatamu mwaka wa 2018.

Aljazeera inaripoti kuwa viongozi wa mkoa wa Tigray walianza kufanya ugomvi na serikali ya Abiy Ahmed mara tu alipokuwa waziri mkuu. Walimshtaki kwa kuwaweka pembeni wakati aliporafikiana na uongozi wa Eritrea. Na kwa kweli, baada ya kupaa kwake madarakani, waziri mkuu Abiy alipiganisha viongozi wafisadi katika nafasi za juu ambao wengi wao walikuwa kutoka Tigray. Tigray inaamini kuwa hatua ya kurekebisha uhusiano kati ya serikali ya Abiy na Eritria ni njia ya kuwadhibiti wao. Baada ya shambulio la angani na serikali ya shirikisho, Tigrey ilifunga anga lake na kuzuia barabara kufikia mkoa huo. Muungano wa TPLF umekamata kituo cha kijeshi cha uongozi cha shirikisho cha kaskazini, kitendo ambacho waziri mkuu Abiy Ahmed amekiita ‘crossing a red line’

Ethiopia inakabiliwa na changamoto nyingi kwa sasa zaidi ya ugomvi baina yake na Tigrey pamoja na janga la COVID 19 na mzozo mkubwa na Misri juu ya mto Nile. Waziri mkuu Abiy Ahmed, alipewa tuzo ya amani ya Nobel mnamo 2019 baada ya juhudi zake za kupatanisha mgogoro nchini Sudan, Sudan kusini, Djibouti, Kenya na Somalia. Kwa sasa uwezo wake wa kutuliza gasia wahitajika sana katika nchi yake mwenyewe. Bara zima linaangalia jinsi gani atakavyo fanya.