“Maisha ni msingi ambako kila kitu kingine hujengwa juu, Ndicho kitu cha thamani zaidi tulicho nacho, kwa hivyo tunapaswa kukitunza. Maana tunaishi tu mara moja. “- Georges

Wazaliwa wa Maine wenye asili ya Kiafrika ambao walizungumza na Amjambo Africa! mwezi huu wametambua kuwepo kwa tofauti kubwa za kitamaduni kati ya Waafrika na Watu wa Maine kulingana na mitazamo ya afya. Kula kwa afya, mazoezi ya mwili, na uchunguzi wa uzito vimo miongoni mwa wasiwasi mkuu kwa Wamarekani, juhudi za kugonda ao kupoteza uzito ni lengo moja wapo kubwa kati ya malengo ya kawaida watu wanayoshiriki pamoja. Kwa kweli, kulingana na CDC, asilimia hamsini ya Wamarekani wanatazamia sana kugonda ao kupoteza uzito. Kwa hivyo, hongera zote za kijamii kwa yeyote ule anayepoteza uzito zina pokelewa vizuri sana katika Amerika. Kinyume ya hiyo, katika nchi nyingi za Kiafrika, kupoteza uzito hueleweka vibaya sana. Maana kupoteza uzito huonekana kama alama ya ukosefu, shida, na hali mbovu ya kimaisha, kwa hiyo, kunenepa ao kuongeza uzito huonekana kama alama ya utajiri na wingi wa ustawi.

Watu kutokea Afrika ambao walizungumza na Amjambo Africa! walisema kama kisha kuja kwa nchi hii, kabla ya kutambua kuwa Wamarekani wamezingatia sana kupoteza uzito, walikuwa wamefanya makosa makubwa kwa kupongeza marafiki wao wamarekani wapya kuhusu kuongezeka uzito! ‘Pongezi’ hizo zimekuwa bila kutaka matusi yasiyo ya hiari kutokana na mtazamo wa marafiki zao wapya. Wao walifasiria kwamba katika nchi nyingi za Kiafrika hali hii inachukuliwa kama pongezi kusema kwamba mtu anaonekana vizuri baada ya kupata kuongeza uzito. Walizihaki wakisema kwamba huko nyumbani hakuna wakati wowote ule wangehofu ajili ya kupoteza uzito!

Watu wachache walitoa maoni yao kwamba kawaida ya kitamaduni ya Marekani ya kujaribu kupoteza uzito imeanza kuwaadhiri bila kujua. Walisema kwamba huko nyumbani hakuna wakati wowote ule wangejaribu kutaka kupoteza uzito, au kufikiri kwamba kuongeza uzito ilikuwa suala la kiafya, lakini kwa sasa vyombo vya kijamii vya upashaji habari pamoja na taarifa mbalimbali vina gusa sana mtazamo wao kuhusu kile kilichoonekana mwanzoni kuwa urembo. Wakati huu, matajiri nchini Afrika ambao wanaweza kupata chakula cha kutosha wameanza kutafakari juu ya udhibiti uzito kama kipengele muhimu cha afya.

Utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili bado huwa tendo haba huko Afrika. Mazoezi huchukuliwa kama tukio la kijamii kuliko kuwa sehemu ya hali ya maisha ya kiafya. Kwa mfano, vijana wanaweza kuja pamoja ili kucheza mupira wa miguu au mpira wa kikapu. Kinyume na hiyo, wakati wa majira ya joto hapa, Wamarekani wa umri wowote ule hujaa mabarabarani na penye nafasi za umma, wakipiga mbio na kuendesha baiskeli kama aina ya mazoezi. Watu wengine huenda hata kuamka asubuhi mapema na kwenda kwenye vituo mazoezi ya afya kabla ya kujielekeza kazini. Matukio ya uchumi inaonyesha umuhimu wa tamaduni kawaida hii katika jamii ya Marekani, pamoja na kampuni za mazoezi ya mwili zinazozalisha mabilioni ya dola kila mwaka.

Hatimaye, wazaliwa wa Maine wenye aslili ya kiAfrika waligawa maoni yao kwamba wana wasiwasi kuhusu ubora wa chakula wanachokula hapa. Huko nyumbani chakula karibu chote kilikuwa kikaboni, na wala hakikufanyiwa mabadiliko yoyote, tofauti na hapa nchini Marekani. Watu waligawa maoni yao kusema kwamba wangependa kujuwa zaidi kuhusu vyakula vyenye afya kwa kukula hapa, na ni vipi visivyo. Humo Afrika, wakati mwandishi wa kipande hiki alipokuwa akikua, chochote kile ambacho kingeweza kuongeza uzito juu ya mtu kilikuwa kinahesabiwa kuwa chenye afya – maziwa, nyama, maharagwe na viazi hasa. Mboga mboga zilikuwapo nyingi, lakini watu walio wengi hawakuzipenda. Watu walikuwa wanazihaki kwamba kula mboga mboga ni kama mbuzi au ng’ombe wanao kula nyasi!