By Kathreen Harrison

  “Jitu Mlala usingizi ambaye ni Afrika yupo anaamka wakati huu” aliyatangaza hayo Daktari Arikana Chihombori-Quao, Balozi wa Umoja wa Afrika kwa Marekani. Fursa hiyo ilikuwa ni wakati wa mazungumuzo yaliyo dhaminiwa na Baraza la viashara Ulimwenguni la Maine humu Portland ambayo ilitembelewa na balozi huyu mnamo tarehe Septemba 12 na 13 kwa ziara ya siku mbili kwa mwaliko wa diwani wa Jiji la Portland Pious Ali.

Dr. Arikana Chihombori-Quao was resplendent in a pink gown made by fashion designer Adele Masengo Ngoy of Portland

“Nimekutana mara ya kwanza na Mheshimiwa Arikana Chihombori-Quao kunako mkutano wa kila mwaka wa wa Marekani wapya viongozi mashujaa mnamo December, 2018. Nimekuwa nikitaka kila wakati kuleta jamii ya Waafrika ugenini walio humu Maine ili sote pamoja tuijenge jamii, na nilikuwa nikitafuta fursa hiyo. Tulikuwa na siku chache za mshangao, “alisema hivyo diwani Ali
Waheshimiwa mashuhuri wasio wachache walihudhuria hafla ya Baraza hili la viashara Ulimwenguni la Maine, wakiwemo pamoja na Mwakilishi Rachel Talbot Ross, Madiwani wa Jiji la Portland Pious Ali na Jill Duson, Diwani wa Jiji la Portland Kusini Deqa Dhalac, na Waziri wa zamani wa Kazi ya Umma na Ujenzi wa Somalia, Eng. Nadifa Osman.
Baada ya hotuba ya ukaribishaji ya mkurugenzi mtendaji wa Baraza la viashara Ulimwenguni la Maine, Kate McCarthy, Diwani Ali aliwasilisha Balozi Arikana Chihombori-Quao akiwa na ufunguo kwenye Jiji la Portland, na Diwani wa Jiji la Portland Jill Duson alisoma tamko kutoka kwa Meya Strimling, humo akitangaza mwezi wa Septemba 2019 kuwa Mwezi wa Urithi wa KiAfrika katika Portland.
Ziara ya Daktari Arikana Chihombori-Quao ilikuwa ya kazi nyingi. Alhamisi, alikutana kujadili kuhusu uwezekano wa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Maine, Chuo Kikuu cha Maine ya Kusini, Chuo cha Thornton, Ushauri wa Global Tides, na Idexx. Alhamisi jioni, Waafrika wanaoishi ugenini, Wamarekani wa asili ya Kiafrika, na mheshimiwa Arikana Chihombori-Quao walishiriki pamoja chakula pia mazungumzo.
Diwani Ali alibaini kuwa mkutano huo, ambao uliowaleta pamoja vizazi vya Waafrika walioletwa hapa kutoka vizazi vya kale pasipo utashi wao, na vizazi vya wahamiaji wa hivi karibuni kutoka Afrika, haikuwa ya kawaida hapa Maine, ambapo jamii hizo mbili huchanganyika isivyo ya kawaida. Alionyesha matumaini yake kwamba mkutano huo hautabaki wa kipekee. Ijumaa, mheshimiwa Arikana Chihombori-Quao alitembelea Shule la sekondari la Deering.
Siku ya Ijumaa jioni, baada ya muhtasari ulio dhahiri na dhahiri wa historia ya ukoloni barani Afrika, na unyonyaji usio koma wa mali asili yake na kampuni za kimataifa na za serikali za nje hadi leo, Balozi alieleza mabadiliko ambayo yapo karibu.

 

Representative Rachel Talbot Ross, South Portland City Councilor Deqa Dhalac, Portland City Councilors Pious Ali and Jill Duson

 

 

 

 

Former Minister of Public Works and Reconstruction of Somalia, Eng. Nadifa Osman shares a laugh with South Portland City Councilor Deqa Dhalac

With fashion designer Adele Masengo Ngoy of Portland and her daughter

With Dr. Ahmed of Deering High School

 

With Georges Budagu Makoko, publisher of Amjambo Africa

With Claude Rwaganje, Executive Director of ProsperityME

 

 

 

 

 

 

“Baada ya uja uzito mrefu, na miaka mingi ya huduma ya kujifungua mimba, mwishowe mtoto amezaliwa, na jina la mtoto ni Mkataba wa Biashara Huria ya Bara la Afrika/African Continental Free Trade Agreement (AfCFTA). Tunahitaji kumlea mtoto huu kwa makini sana, na kumsaidia kukua na kukomaa. Nchi zote 55 barani Afrika zinahitaji kukusanyika kwa pamoja katika makubaliano hayo, ambayo yalifungwa na Umoja wa Afrika, yaliyoanzishwa mwaka wa 2013, na kuridhiwa mwezi wa Machi uliyopita mwaka wa 2018. Mwishowe tunaongea sasa kwa sauti moja. Ni uamuzi muhimu sana ambao tulikuwa tumehitaji kuuchukua zaidi ya miaka 700 iliyopita, tangu wakoloni wa kwanzakwanza walipofika Afrika – ili kuchukua nafasi ya haki yake muhimu ulimwenguni. Kuanzia Julai 2020, Afrika itaingia kwenye soko la dunia kama ‘Afrika’ badala ya nchi 55. ”
Daktari Arikana Chihombori-Quao alisema kwamba AfCFTA ni mabadiliko ya mchezo. Makubaliano ya kihistoria yatawezesha nchi za KiAfrika kushindana na wenhye uchumi kubwa za mkoa – kitu ambacho nchi moja moja kibinafsi haikuweza kusimamia peke yake, kwa sababu ya udogo wao, na kiasi kidogo cha uchumi. Mkataba wa Biashara Huria ya Bara la Afrika utaruhusu wafanyakazi wa KiAfrika kufanya kazi mahali popote watakapotaka kwenye bara; kuhoja bidhaa kwenye mipaka ya kitaifa bila kuchelewa; kufungua utalii na biashara ya kusafiri ndani ya bara.
“Wakati huu, nchi za Afrika zinataka kuwa mabondia, wanao tupwa mara kwa mara kwenye uwanja wa ndondi wakipambana na wapiga ndondi wenye uzito mwingi. Kwa mfano, Afrika Magharibi huzalisha 65% ya kakao ya ulimwengu, lakini mwaka jana tu ulianza kutengeneza kiwanda chake cha chokoleti. Watu wanaongea kwa haki juu ya ufisadi wa viongozi wamoja wa KiAfrika, lakini ikiwa tutazungumza juu ya ufisadi – acha basi tuzungumze juu ya ufisadi wote. Angalau dola bilioni 50 huondoka Afrika kila mwaka kwa sababu ya ufisadi. ”
“Afrika lazima itoke kwenye njia ya kupoteza. Tunahitaji kujiunga pamoja kama WaAfrika, na marafiki wa Afrika, na kumuelewa kwa nukta ya ukweli, wala sio uwongo. ”
Balozi aliwasihi jamii ya wafanyabiashara wa Amerika kuamka kwa ujio wa Mkataba wa Biashara Huria ya Bara la Afrika.

“Wazungu wako tayari – WaChina wako tayari – watu ambao hawako tayari ni Wamarekani. Popote ninapoenda, jumuiya ya wafanya biashara wa Amerika haijui kuwepo kwa AfCTFA. ”
Siku ya Jumamosi asubuhi, alipokuwa akielekea uwanja wa ndege wa Portland Jetport kwa safari ya kurudi Washington, DC, Daktari Arikana Chihombori-Quao alishirikisha mawazo mengine kadhaa .. Anajitahidi kuhamasisha waishio ugenini wa KiAfrika – wakiwemo Wamarekani wa asili ya KiAfrika – ili kusaidia kujenga uwezo wa Afrika. Database itazinduliwa mwezi wa Oktoba kwa wanachama wa waAfrika wanao ishi ugenini ili kusajili majina yao, na ustadi walio nao, pia balozi huyo aliwasihi jumuiya ya jamii ya WaAfrika wa ugenini kujipanga wenyewe kwa kutarajia uzinduzi huo. Aligundua kuwa sura za KiAfrika za waishio ugenini zimefunguliwa huko Florida, New York, Minnesota, Texas, na Carolina Magharibi, pia aliongea juu ya umuhimu wa kuungana kama wanamemba wa Jumuiya ya WaAfrika wa ugenini na kushinda juu ya urithi mrefu mnoo wa utumwa na ukoloni.
“Fanya kazi kwa bidii, kaa chonjo, na kumbuka kuwa Afrika ni nyumbani kwako. Kukuza bara lako kwa njia yoyote ile muhimu, kama vile makabila mengine kutoka sehemu mbali mbali zingine za ulimwengu waliopo hapa Marekani wanavyo fanya, “alisema. “Mambo mazuri yanatarajiwa kutokea Afrika.”
Ujumbe wa umoja kutoka kwa Balozi Arikana Chihombori-Quao ulitoa sauti moja na ya Abdullahi Ali, mwenye asili ya Somalia. Alisema, “Ninaamini waishio ugenini wa Kiafrika wanapaswa kuchukua jukumu la kuijenga Afrika ya kisasa ilio unganishwa. Ufafanuzi wa Umoja wa Afrika kuhusu waishio ugenini wa KiAfrika ni walio ungana pamoja na kutiana moyo – sio tu wahamiaji wa Kiafrika wa hivi karibuni ambao wanaishi inje ya bara, lakini mtu yeyote wa asili ya KiAfrika, ikiwa ni Mwafrika-mwAmerika, Walatino weusi, wale wa Kutoka Karaibe, au waAfrika waliozaliwa wahamiaji. Wanaoishi ugenini wanaweza kuchukua jukumu la mihimu katika udemokrasia, uwekezaji uchumi, ujumuishaji, na maendeleo ya bara hilo.