By Damascene Hakuzimana

Mahojiano na madaktari wawili wafaransa kwenye kituo cha Televisheni cha Ufaransa LCI yameibua hasira katika vyombo vya habari baada ya madaktari hao kupendekeza kwamba majaribio ya chanjo ya COVID-19 Yaliyo tazamiwa kuzinduliwa huko Ulaya na Australia yange paswa kujaribiwa kwanza Afrika. Jaribio hilo ni kuona ikiwa chanjo ya Kifua Kikuu cha Bacille Calmette-Guérin (BCG) ingefanikiwa katika kutibu COVID-19. Ingawa chanjo hiyo haijulikani sana Marekani, mara nyingi – huwa mara kwa mara na matokeo mchanganyiko – inapewa kwa watoto na watoto wachanga katika nchi ambazo magonjwa ya kifua kikuu ni ya kawaida.

Takwimu za michezo, wakuu wa kisiasa, na raia wa kawaida kutoka Afrika na ulimwenguni kote walionyesha hasira zao kwa maoni ya madaktari hawa. Walisema maoni hayo kuwa ya ‘ubaguzi wa rangi.’ Madaktari hao wawili wahusikao ni Paul Mira, mkuu wa kitengo cha utunzaji mukuu wa wagonjwa katika Hospitali ya Cochin huko Paris, na Camille Locht, mkurugenzi wa utafiti katika Taasisi ya Afya ya Ufaransa.

Pendekezo la Mira, “Linaweza kuwa la uchokozi. Tunge paswa kufanyia utafiti huu barani Afrika, ambapo hakuna kinga ya uso, hakuna matibabu, wala utunzaji mkuu wa wagonjwa – ikiwa kama karibu na ilivyokuwa kwa kesi fulani utafiti juu ya Ukimwi, iliyofanyika miongoni mwa makahaba, tunapima vitu kwao, kwa sababu tunajua kuwa wamekuwa kwa hatari kubwa sana na wala hawajikinge wenyewe?”

Umesema kweli, “alijibu Locht.

AfricaNews iliripoti kuhusu majibu makali kutoka kwa mwana nyota wa kimataifa wa mpira wa miguu barani Afrika. Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea kutoka Ivory Coast Didier Drogba aliyeyashutumu maoni yasemayo kwamba Afrika inapaswa kutumiwa kama mahali pa jaribio la suluhisho la mchafuko huu wa coronavirus unaoendelea.

“Haiwezekani kabisa ikiwa tunaendelea kuvumilia mambo kama haya … Afrika sio maabara ya upimaji. Ningependa kukemea kwa nguvu na waziwazi udhalilishaji huo, uwongo, na masemi ya ubaguzi. Tusaidieni kuiokoa Afrika… ”Drogba aliandika kwenye Twitter.

Demba Ba wa kilabu cha Uturuki Istanbul Basaksehir pia alijibu kwa hasira kwenye Twitter. Barua yake ilisomeka, “Karibu huku Magharibi. Ambapo wazungu wanajiamini kuwa ni bora zaidi na ya kwamba ubaguzi wao wa rangi na ujinga ndio kawaida. ”
#waAfrika sizo panya za maabara #waAfrika sio nguruwe za Guinea yamekuwa yakiendeshwa kwenye Twitter tangu yalipojitokeza mahojiano yenye utata wa Madaktari hao. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani matamshi ya madaktari hao, akiwatambulisha kama wenye ‘ubaguzi wa rangi’ na kwa bahati mbaya wenye kukumbukumbu za ‘mtazamo wa ukoloni.’
Pious Ali wa Maine, aliyeulizwa kutoa maoni, alisema, “Tangu Ufaransa ilipokua barani Afrika mnamo mwaka wa 1659, wakoloni wameendelea bila kukoma kuiga kila kitu walichoweza… Naita Umoja wa Afrika kupinga moja kwa moja ubaguzi huu ulio wazi. Mababu zetu wanaweza kuwa hawakuwa na vifaa vya kupigana na wakoloni, lakini viongozi walioko sasa hawana udhuru… Zamani za kale ndizo siku ambazo wakoloni walizoea kutumia nchi masikini kama maabara yao. ”

Jumuiya ya Wanahabari inaripoti kwamba Daktari Jean-Jacques Muyembe, mkuu wa taasisi ya kitaifa ya biolojia huko Congo-Kinshasa, na anayeaminika kwa kukomesha kusambazwa kwa Ebola Jamuhuri ya Congo, amechukua maoni tofauti kwa maonyo hayo, akikaribisha majaribio hayo barani Afrika. “Chanjo hiyo itatengenezwa nchini Marekani, au Canada, au Uchina. Sisi ni miongoni mwa wagombea wa kufanya upimaji huo hapa, “alisema Muyembe. Maoni yake mara yalizusha utata mkuu huko DR Congo huku kukiwa tuhuma ya wanainchi kutumiwa kama nguruwe wa Guinea.

Kulingana na Deutsche Welle ya Ujerumani, shirika la wanasheria la Moroko limesema kwamba lita nia ya kumshtaki Daktari Mira kwa tuhuma la matusi yanao elekea ubaguzi wa rangi. Shirika lisilo la Kiserkali la Ufaransa linalo pinga ubaguzi wa rangi, SOS Racisme, lilitoa taarifa ikisema “Hapana, Waafrika sio nguruwe wa Guinea,” na ikafafanua kule kulinganishwa kwa UKIMWI na makahaba kama ‘shida tata’ na ‘isiyokaribishwa kamwe. CSA, aliye mwangalizi wa maadili ya redio na televisheni huko Ufaransa, aliiambia AFP kwamba imepokea malalamiko hayo.
Ijumaa, Aprili tarehe 3, Mira alinukuliwa akisema, “Nataka kuwasilisha ombi langu la msamaha kwa wale wote ambao waliumizwa, walishtuka, na kuhisi kutukanwa na maneno niliyoyasema wazi kwa nguvu.”