Georges Budagu Makoko
Uzuri wa demokrasia ni mfumo ambao msingi wake unampa mwanchi nguvu na mamlaka ya kuamua watayempigia kura kama viongozi. Takriban watu 7.8 bilioni kote duniani hawajapata na fursa ya kuwachagua viongozi wao wenyewe, lakini wamarekani (U.S citizens) wamejiandikia ukurasa wa historia kwa kujitokeza takriban watu 161 milioni katika uchaguzi wa urais wa 2020. Ukweli ni kwamba, uchaguzi wa 2020 uliwahusisha wananchi wengi zaidi marekani katika historia ya kisasa – licha ya kuwa na janga la korona ambalo limeangamiza maisha ya mamia ya maelfu ya watu na kuziteketeza familia nyingi. Hata katika mateso hayo yote mamilioni ya wamarekani walijitokeza kuhakikisha kuwa wametimiza haki yao ya upigaji kura.
Rafiki zangu ambao ni wahamiaji wanaamini kuwa sababu ya wengi kujitokeza ni kuwa walitaka kuyapigania maadili ya kidemokrasia. Watu wenye rangi walijitokeza kupiga kura kwa uwingi na tunajivunia hilo kwa vile sauti zetu haziwezi kupuuzwa katika mchakato huo wa uchaguzi. Hata vijana ambao kwa kawaida hawashiriki uchaguzi walijitokeza.
Nimekuwa marekani kwa muda wa miaka kumi na minane(18) na kushiriki katika chaguzi kadhaa na sijawahi shuhudia uchaguzi wa aina hii ambapo mshindi hatangazwi siku ile ya uchaguzi nayo hali ya sintofahamu inaendelea kukua kila kuchao kwa jamii ya wahamiaji matokeo yasubiriwapo na taifa zima. Niliiweka simu yangu karibu nami nyakati zote huku nikiamka kila mara usiku kuangalia kama matokeo yametangazwa. Watu wengi niwajuao walichukua muda mwingi wakiongea na marafiki wa Marekani na wa ughaibuni, sote tukijaribu kubashiri matokeo kamili. Kila niliyemjua alilenga matokeo .
Hisia zetu pamoja na wahamiaji wenzangu zilikuwa nzito. Miaka minne yenye majaribio chini ya uongozi ulikuweko imekuwa migumu kwa jamii ya wahamiaji. Wengi wamenielezea kuwa walipoteza uaminifu katika nchi na kuwa walipoteza matumaini, na ndoto zao kufutiliwa mbali kwa miaka minne iliyopita. Walizungumza kuhusu athari za sera za Trump kwa jamii ya wahamiaji hapa Maine na kusema kuwa tabia ya Marekani kuwakaribisha wahamiaji ilibadirishwa. Walisema kuwa walisumbuliwa akili na amri za hapa na hapa zilizowalenga wahamiaji na kuwa maelfu ya watu walivunjika moyo na Marekani na wakakusudia kuhamia Canada kutafuta hifadhi.
Wanajamii wanaamini kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu ni habari nzuri kwa wahamiaji na wanaamini siku zijazo zitakuwa zenye manufaa kwao. Wamepata pumziko na kuwa hawataamkia jumbe za tweeter zikiwaarifu wafunge virago na kuikimbia nchi waliyoiamini kuwa kama nyumbani.. Watu waliuzungumzia uchaguzi wa Joe Biden kama ushindi dhidi ya woga. Binti mmoja niliyezungumza naye ambaye ameshiriki katika chaguzi tatu za Marekani kutoka awe raia wa nchi hiyo alisema, “Uongozi uliokuweko ulikuwa wenye shida kwa wahamiaji na kubadilishwa kwa sheria mara kwa mara kuhusu uhamiaji kulifanya maisha ya wahamiaji kuwa magumu sana. Tumaini langu kwa huu mfumo mpya wa uongozi ni kujua cha kutarajia na si kushtuliwa kila wakati. Miaka minne iliyopita ilikuwa ya kushtua moyo. Nina matumaini kuwa utawala mbpya wa Joe Biden utaleta uponyaji” Tumaini limerejeshwa ughaibuni na hata Maine. Mkongo mhamiaji anayeishi Kenya alinieleza kuwa, “ Uongozi wa Marekani umebatilishwa kabisa. Tumaini letu kuuona ukirejea tena.”
Ukweli ni kuwa kumuona rais aliyekuwa mamlakani akitilia shaka matokeo ya uchaguzi ,unawatia jamii ya wahamiaji kuhofia uwezo wa kuzuka kwa machafuko. Wahamiaji wengi kutoka nchi za Afrika , wana kumbukumbu za machafuko baada ya uchaguzi haswa chama cha kisiasa kikikosa kukubaliana na matokeo ya uchaguzi. Mifano ya hivi karibuni ni ile ya 2015 uchaguzi wa Burundi , 2017 uchaguzi wa Kenya na uchaguzi wa DR Congo 2018. Wahamiaji wanaowaona Republicans wakigoma mitaani huku Rais Trump akiyapinga matokeo ya uchagujzi wana hofia kuzuka kwa machafuko na vita. Demokrasia ni lazima ilindwe; ikipotezwa huchukua miaka mingi kurejeshwa na wakati mwingine huweza kupotezwa kabisa Kwa mfano miaka ya 1930s uchajguzi wa kidemokrasia ulimrejesha Hitler mamlakani lakini wale wa Nationalists walichukua serkali na kulazimisha ajenda yao kote nchini.
Sala yangu ya dhati ni kwamba mamia ya miaka ya kujenga taasisi madhubuti za kidemokrasia nchini marekani itashinda uchoyo na uyanguyangu binafsi . Mungu aibariki Amerika kwa kurudi kwa maadili yetu ya msingi.