By Georges Budagu Makoko, Publisher
Kwa kukua katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nilitumainiaka kuwa na haki ya kupiga kura siku moja. Lakini Rais Mobutu Sese Seko pekee ndiye alikuwaka anaandaa uchaguzi wakati wa miaka yake yote 30 ofisini – na sio wakati huo nilpokuwa nikiishi nchini DRC kama mtu mzima. Kwa hiyo nilipiga kura kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012, iliyo kuwa mwaka wa kwanza nilivyostahiki kufanya hivyo, baada ya kupewa uraia wa Marekani mnamo mwaka wa 2011. Tangu wakati huo sijawahi kukosa nafasi ya kupiga kura.
Nimeishi Marekani sasa miaka17. Katika kipindi hicho cha muda, nimeshtushwa mara kwa mara na idadi ya Wamarekani wanaostahiki kupiga kura – lakini hawafanyi hivyo. Kuchukua kwa urahisi uwezo wa kupiga kura ni kama kusikitisha mamilioni ya watu ulimwenguni kote ambao hawajawahi kushirikishwa haki hiyo kutokana na serikali za kikatili na za kukandamiza wanazoishi ndani. Uchaguzi huko Marekani unavutia sana wahamiaji wa KiAfrika. Tunawaona kama mfano mzuri wa mfumo wa demokrasia huko Marekani. Ninawasihi wote wanaoweza kupiga kura kufanya hivyo – jukumu hili kubwa la kufanya maamuzi muhimu kwa niaba ya wananchi halingepaswa kutupiliwa mbali.
Viongozi wengi barani Afrika huingia madarakani kwa kutumia nguvu za majeshi, na hawaachi madaraka hayo kwa hiari. Mara tu wakiwa madarakani, wanakuwa na busara kabisa katika kuteua wanaobaki kwa kuingia serikali yao. Katika nchi nyingi, uchaguzi wa wateule hawa haitokane na sifa wala ubora, lakini kwa upendeleo wa kibinafsi wa kiongozi. Sauti ya kiongozi mmoja huzidi wasiwasi wa watu wengine wote.
Kwa miezi kadhaa iliyopita Maine imechapishwa pande zote na alama za kampeni kwa upande wa wagombea ambao wanajiandaa kuendesha uchaguzi mkuu unaokuja ifikapo Novemba 5. Wagombea na wafuasi wao huonekana kwenye mabaraza ya umma na kugonga milango ya watu ili kugawa maoni yao ya kisiasa, kuzungumzia juu ya maswala ambayo wanajali, na kuwaelezea watu kuhusu mipango yao ya kutatua shida ili kubadilisha maisha ya watu kwa njia nzuri. Mitaa na maeneo ya umma yote ya Maine imefurika na chapa za kampeni zinazobeba ujumbe tofauti unaowakilisha maadili ya wagombea pamoja na kile wanachokisimamia. Ujumbe hizi zote zinalenga kupata kuaminiwa na watu.
Swali kuu ambalo watu wangepaswa kuuliza wakati wa msimu wa uchaguzi ni “nani aliye mgombea bora?” Kuamua vizuri na kwa busara kuhusu uchaguzi wa viongozi wazuri kunaweza kutengwa kwa urahisi na mhemko ulioinuliwa na usanifu wa kampeni na itikadi. Watu wengi hawauchukui muda wa kukagua tabia ya mgombea na nini msimamo wake juu ya maswala, na kuruhusu mazungumzo ya kampeni kuathiri maamuzi yao. Tabia ni muhimu katika mgombeaji – mtazamo wao wa ubinafsi, shauku na upendo wa kiraia, uwezo wa kutathmini na kuelewa mahitaji ya watu, na uwezo wa kutatua shida. Tunahitaji viongozi waliochaguliwa kupata suluhisho kwa changamoto muhimu.
Maamuzi inayofanywa na waliochaguliwa ya atharisha maisha ya watu kwa njia muhimu. Mifano ya hivi karibuni huko Maine ni pamoja na gavana ambaye aliwezesha wanaotafuta hifadhi kupata Msaada wa Jumla, baada ya gavana wa zamani ambay alikuwa amekataa katu katu msaada huo. Mifano mingine ni pamoja na uamuzi wa Portland kupanua matoleo ya mapema ya K kwa mwaka huu wa shule, na uamuzi wa serikali kutaka wilaya zote kutoa pre-K ifikapo mwaka wa shule wa 2023-2024. Maamuzi haya yanaonyesha wazi ni kwa nini tunapaswa kuwa na uangalifu katika kutoa kura zetu.
Kwa kuwa wahamiaji wengi wamekua chini ya serikali za kukandamiza na huenda wamepitia ghasia au vurugu na kuteswa kulingana na uchaguzi huko nyumbani kwao, wanaweza pia kuwa wamepitia wasiwasi mwingi wakati wa msimu wa uchaguzi huko Maine. Wange paswa kuhakikishiwa ya kwamba uchaguzi utakuwa wa amani hapa, na kwamba kushiriki ni salama.
Ni jambo la kutia moyo sana kuona wagombea tisa kutoka jamii ya wahamiaji wakiwa katika mbio ku shindania uchaguzi wa ofisi ya bodi za shule na mabaraza ya jiji huko Maine. Hii ni ishara wazi kwamba wahamiaji wanataka kukumbatia demokrasia na wanachukua jukumu muhimu katika mfumo wa maamuzi ya serikali.
Viongozi wana nafasi na uwezo wa kuokoa au kuharibu jamii yetu. Ni jukumu letu kuwashirikisha viongozi hawa wanapochukua maamuzi mazito – na pia kupiga kura kwa mutu aliye bora sana.