Serikali ya shirikisho inapendekeza kuwa gharama za utunzaji wa watoto zinapaswa kuwa chini ya 7% ya bajeti ya wastani ya jamaa, lakini ukweli wa mam kwa familia nyingi hapa Maine ni tofauti sana.Wastani wa gharama za utunzaji wa watoto Portland zinakadiriwa kuwa sawa na $16,381 ambayo inazidigharama ya masomo katika vyuo vikuu vya serikali vya miaka minne

Tulikaa pamoja na Katie Soucy kutoka Starting Strong na kujifunza kuhusu chaguzi na mipango tofauti

Ninawezaje kupata mtoa huduma ya watoto?
Kupata mtoa huduma ya watoto inaweza chukua muda mrefu, kwa hiyo ni vizuri kuanza kutata miezi kaza kabla mtoto hajaanza(Hata kabla mtoto hajazaliwa!) Huduma moja nimefurahia sana ni OEO’s Childcare Journey Map(www.portlandofopportunity.com/how-do-i-find-childcare) ambayo inapatikana katika lugha nyingi.
Kila mmoja anapaswa kuiangalia. Kwa kuongeza, habari ya mawasiliano na ukadiriaji wa ubora kwa watoa huduma wote wa leseni ya utunzaji wa watototo inapatikana kwenye mtandao www.childcarechoices.me, pamoja na usaidizina mapendekezo ya jinsi ya kupata huduma bora inayofaa kwa jamaa yako. Mwishowe ni vizuri kupanga wakati wa kukutana na mkurugenzi au mwalimu, tembelea program na ujifunze juu ya falsafa yaoya utunzaji.Ni muhimu kujisikia vizuri kama mzazi.Mwishowe fikiria kuweka jina lako kwenye zaidi ya orodha moja-hakika kuna uhaba wa nafasi katika Maine

 

Ninajuaje ikiwa ningeweza kustahiki msaada wa kifedha?
Kujua ikiwa unaweza kustahiki msaada wa kifedha kunaweza kutatanisha sana. Programu tofauti zina vigezo tofauti. Ninawashauri watu kuanza na wakala wa karibu na kwao wa HeadStart, kwa sababu kwa kawaida wanaweza kusaidia jamaa kupanga kupitia program tofauti. Mahali pengine pazuri pa kuanzia ni Child Care Subsidy Program ya serikali ya Maine.Maombi (na habari zaidi ) hupatikana kwenye https://www.maine.gov/dhhs/ocfs/ec/occhs/step.htm.

 

 

Orodha ya wahudumu ni ndefu kiasi gani?
Orodha ni ndefu kwa sababu hatuna nafasi za kutosha za utunzaji watoto ili kukidhi hitaji, haswa kwa watoto wachanga. Ijapokuwa gharama kubwa kwa wazazi, huduma za utunzaji wa watoto mara nyingi hupata faida ndogo sana Tumeshuhudia kupungua kwa idadi ya watoa huduma katika jamii yetu. Kwa miaka wakati huo huo tukiona familia zaidi na zaidi paoja na watu wazima wote wakienda kazini. Kwa bahati mbaya janga limezidisha tu shida ya utunzaji wa watoto na watoa huduma wengi kufunga kwa sababu ya kupungua kwa uwezo na kuongezeka kwa gharama

 

Ninawezaje kushiriki?
Ukosefu wa huduma bora ya watoto yenye bei rahisi ni suala ngumu lakini kwa kufanya kazi pamoja tunaweza kujenga jamii ambapo watoto na familia kutoka asili na hali zote wanapata msaada wanaohitaji kufikia uwezo wao kamili. Starting Strong inawakutanisha wadau kutoa taarifa na kutetea sera ambazo zitasaidia kutatua shida hii.Tunafurahia sana kuwakaribisha wazazi katika kazi hii, na tumeanza kuhudhuria mikutano ya kila mara ya wazazi ili kuweka sauti ya mzazi na uongozi katika juhudi zetu. Ukitaka kujua zaidi angalia tovuti yetu na jiunge na orodha yetu https://www.portlandstaringstrong.org.

 

Kupata huduma ya watoto bora nay a bei rahisi ni muhimu. Ikiwa unahangaika kupata mtoaji wa huduma ya watoto umuaminie na uwezae kulipa bila shida-jua kuwa hauko peke yako. Tafadhali kumbuka kuangalia tovuti yetu ili upate msaada ukitembea ndani ya tovuti hiyo wakati huu mzuri lakini wenye mkazo na changamoto( inapatikana katika lugha nyingi) https://www.portlandofopportunity.com/how-do-i-find-childcare