Utamaduni una jukumu muhimu katika maisha tunayoishi na kushilikiana na wengine. Kuelewa utamaduni wetu wenyewe na wale wengine husaidia kuziba vikwazo na kuimarisha juhudi za kushirikiana pamoja.
Tofauti inayoonekana ya kitamaduni kati ya wanainchi wapya kutoka Afrika na wenyeji wa Maine inahusisha mbinu zetu tofauti za mavazi. Waafrika nanao mshangao wakati wa kiona kwamba Wamarekani wengi wanastahili sana wakati kufuatana mavalio. Ukifika kwenye mikutano ya kawaida au matukio ya kijamii, tofauti katika mtindo mara nyingi huonekana sana. Mara nyingi Waafrika wanavaa zizuri sana na Wamarekani wengi watavaa kikawaida. Wamarekani wanaonekana kama kuimarisha faraja wakati Waafrika wanapendelea mtindo. Kutambua kwamba tofauti hii ipo inaweza kusaidia kila mtu kujisikia vizuri. Njia moja si sahihi na nyingine mbaya – ni tu bidhaa ya utamaduni.
Wakati watu kutoka Afrika wanajiandaa kwa mkusanyiko wowote wa kijamii wanafikiria mbele juu ya kile watakachovaa na kuzingatia hasa maelezo ya vinavyolingana. Soksi, kwa mfano, inahitaji kufanana vizuri na viatu. Wakati wa harusi, au mkusanyiko mwingine wa sherehe, watu huangalia kila mmoja kwa kushangaza na kubadilishana pongezi kuhusu mavazi. Ni kawaida sana kusikia watu kuzungumza waziwazi kuhusu jinsi wanavyohisi kuhusu mtindo wa wageni, aina ya nguo, na bei. Hii pia ni kweli nchini Marekani, hata hivyo lakini sikwa kiwango hicho.
Katika Afrika, watu mara kwa mara wanatathmini nguo za kila mmoja. Wakati mwingine watu wanaweza hata kuvuka barabara na kumkaribia mgeni ikiwa wanaona shati nzuri au jozi la viatu kuuliza wapi walipopata hiyo. Utasikia watu njiani kutaja bidhaa za premium, kwamufano: Giorgio Arman, Versace, Ralph-Lauren, Dolce & Gabbana na Gucci.
Katika nchi nyingine kama DR Congo na Kongo Brazzaville, kuna kundi la watu wanaojiita Sapeur au La SAP (Société des Ambianceurs et des personnes elegantes) ambalo ina maana ya Society of Ambiance-Makers na watu wenye kifahari. Kikundi hiki kimetokea tangu wakati wa kikoloni, wakati wananchi walipenda kuwaelezea wa wakoloni kwamba pia walikuwa na ustaarabu. Harakati ya Sapeur inaendelea leo na imefanya athari kubwa juu ya thamani ya watu mahali kwenye mavazi. Kwa kweli, watu wengine wanapenda kuvaa zaidi kuliko kitu kingine chochote. Linapokuja suala kati ya kula na kuvaa watu fulani labda unapuka chakula chache lakini kununua na kuvaa nguo za gharama kubwa.
Waafrika mara nyingi wanapendelea mtindo wa Italia na hapa watu wa Maine kutoka Afrika wanaelezea wasiwasi kwamba hawawezi kupata maduka mengi ambapo wanaweza kununua viatu vya Kiitaliano au nguo. Pia hawawezi kupata nguo za Afrika kwa urahisi. Ukosefu wa upatikanaji wa sehemu huelezea kwa nini Waafrika mara nyingi huacha kuvaa nguo za jadi. Sababu nyingine ni kwamba hawaoni wengine wanavaa mitindo kutoka nyumbani, na kuacha mitindo hii ili kuzoea.