Kulingana na ripoti ya 2019 na Taasisi ya Uingiaji Chuo Kikuu na Mafanikio, wastani wa wahitimu wa chuo kikuu cha Maine wanadaiwa $ 32,600 kwa mkopo wa wanafunzi wa mwaka jana. Wakati elimu ya juu inaweza kukusaidia kuendeleza kazi yako, hii sio siri kwamba gharama yake inaweza kuwa kizuizi kigumu cha kushinda. Iwapo wewe ni mwanafunzi anayetaka ingia chuo kikuu au tayari umehitimu, kuna mipango ya usaidizi wa mikopo kwa wanafunzi ambao inaweza kusaidia.


Hapa Maine, kuna deni ya ushuru kwa wanafunzi wanaoishi na kufanya kazi katika jimbo baada ya kuhitimu. Mikopo ya Kodi ya Fursa ya Elimu ya Maine (mara nyingi hujulikana kama Fursa Maine) hutoa deni ambayo inaweza kudaiwa kwenye kurudishwa kwa ushuru wa serikali. Kulingana na mwaka uliohitimu kutoka chuo kikuu, utapokea faida tofauti. Wanafunzi waliohitimu zamani zile kama mwaka wa 2008 wanastahiki, lakini hawatapata faida sawa na ya mhitimu wa hivi karibuni. Tangu 2016, wahitimu wanastahiki kupewa hadi $ 77 kwa mwezi kwa digrii ya washirika; na hadi $ 367 kwa mwezi kwa digrii ya shahada; na hadi $ 338 kwa mwezi kwa digrii ya kuhitimu. Ikiwa ulihitimu na digrii ya shahada mwaka jana na sasa unaishi na kufanya kazi Maine, unaweza kuona una mkopo wa juu kama wa $4,404.


Njia ambayo mkopo hutumiwa inategemea na meja yako. Kwa wasio wa meja ya STEM (sayansi, teknolojia, uhandisi, au hisabati), deni la ushuru litashughulikia kila unachodaiwa na Jimbo la Maine katika ushuru. Kwa mfano, ikiwa ulilipa $ 2,000 kwa mkopo wa wanafunzi mwaka jana, lakini unadaiwa na serikali $ 2,500 kwa ushuru, utalipa serikali $ 500 tu baada ya mkopo kutumia. Ikiwa deni ya ushuru ni ya thamani zaidi kuliko ile unayo deni kwa serikali kwa ushuru, deni yoyote ambayo huwezi kutumia inaweza kushikiliwa na kuendelea hadi miaka 10. Ikiwa wewe ni STEM meja, deni la ushuru linahesabiwa kuwa la kurejeshwa- inamaanisha kwamba baada ya kutumiwa kwa ushuru wako wa mapato, na kuwa umelipa ushuru wako, utapata hundi kwa barua au kupokea amana ya moja kwa moja ya deni lililobaki .


Ni ya muhimu kukumbuka kuwa wakati unastahiki kurudishiwa hadi $ 367 kwa mwezi na digrii ya shahada, hautapokea kiwango hicho cha mkopo ikiwa unalipa viwango vya chini. Ikiwa unalipa $ 200 kwa mwezi kwa mkopo wa wanafunzi, utapokea kiwango kilicho kwa mkopo: $ 200 x 12 (miezi) = $ 2,400. Ikiwa unalipa $ 400 kwa mwezi kwa mkopo wa wanafunzi, ambayo ni zaidi ya kikomo cha mkopo, utapokea zifuatazo kwa mkopo: $ 367 x 12 (miezi) = $ 4,404. Ikiwa wewe ni STEM meja na malipo yako yako chini ya nambari ya juu ya mkopo, kimsingi unasamehewa kwa jumla ya deni yako yote. Ni lazima ulipe kila mwezi, lakini pia pesa hizo hurejeshwa kwako baada ya toa hesabu ya ushuru wako kwa jimbo.


Ili kupokea faida kutoka kwa Fursa ya Maine, unahitaji kujaza kartasi ya fursa ya kielimu wakati una orodhesha malipo yako ya Maine juu ya ushuru wa kurudishwa dhidi ya mapato. Unaweza kupata karatasi hii kwa tovuli
www.opportunitymaine. org na www.maine.gov Pamoja na kikaratasi hicho, una wasilisha tu hati rasmi, uthibitisho wa mkopo, na uthibitisho wa malipo yote juu ya mkopo. Baada ya hayo yote kuwasilishwa kwa Huduma ya Mapato ya Maine, utapokea mkopo wako. Fursa ya Maine ni mpango wa kipekee wa motisha uliyoundwa ili kuwahimiza wale walio na digrii kuishi na kufanya kazi hapa Maine. Kwa chochote kile meja yako inaweza kuwa, ni mpango mzuri sana wa misaada ya mkopo wa wanafunzi na muda mfupi inaochukua kumaliza karatasi wakati wa msimu wa ushuru inaweza kukuokoa maelfu. Ili kujua kiwango cha juu cha mkopo kinachopatikana kwa mwaka uliohitimu, au kwa maelezo zaidi, chunguza https://www.opportunitymaine.org