Je! Unajua kwamba, kwa mujibu wa Shirikisho la Taifa la Ulinzi wa Moto, idara za moto nchini Marekani zimejibu kwa kiasi cha nyumba 355,400 zilizoshika moto kila mwaka kati ya 2012-2016? Takwimu zao zinaonyesha kwamba ajali hizo za moto zimesababisha vifo kwa moto vya watu karibia 2,560 na  majeraha ya moto ya raia 11,670 kila mwaka, pamoja na gharama kiasi cha $ 6.5 bilioni moja kwa moja kwa uharibifu wa mali.

 

Vyanzo vyetu miongoni mwa jamii za waAfrika humu Maine waliozungumuza nasi kuhusu haja ya ku elimishwa na kupewa mafunzo kuhusu namna ya kuishi katika aina za nyumba hizi tunazo hapa Maine. Huko Afrika, nyumba nyingi hujengwa kwa matofali yaliyo chomwa moto, matofali ya udongo, au matofali ya saruji/(block-ciment), na vifaa hivyo ni sugu kwa moto. Kwa upande mwingine, hapa Maine, nyumba nyingi hujengwa kwa mbao, ambayo inaweza waka moto saa yoyote ile. Zaidi ya hayo, idara za moto katika Afrika huwa kama hazipo. Uwepo wa idara ya moto na jukumu lake katika usalama wa watu hapa Maine huonekana kama mshangao kwa walio wapya hapa. Baadhi ya watu walisema kwamba ilikuwa kwao kitisho wakati waliposikia mara ya kwanza magari ya vizimya moto barabarani ziki jibu kwa simu za dharura. Sauti kubwa na taa za kungaa sana za gari za polisi ziliwatisha na kuwa changanyikisha, walivyosema. Walifikiri kwamba jirani yao alikuwa ame shambuliwa. Huko Afrika, nyumba kushika moto ni haba, na kwa hivyo, wakazi wengi wana uzoefu mdogo wa magari ya kuzima moto.

 

Walisisitiza kwamba kuna makundi makubwa mawili ya wahamiaji waAfrika humu Maine – wale wanaotoka maeneo ya mijini, na wale wa maeneo ya vijijini. Wakazi wa mijini huko Afrika wanafahamu aina za nyumba sawa na hizi tunazo hapa pamoja na huduma zao – singa za umeme, kuhami, mabomba – lakini maisha ni tofauti sana katika maeneo ya vijijini ya Afrika. Kwa mfano, wakazi wengi wa vijijini hupikia chakula chao nje au kwenye eneo la jikoni lililo tengwa na nyumba kuu. Wanapika kwenye jiko la mkaa au la kuni, au kwenye jiko la gesi. Kuwepo kwa jiko ndani ya nyumba za waMarekani na magorofa sio kawaida katika nchi za Afrika. Watu waliofika hapa karibuni wanapaswa kukabiliana na kuzoea hali ambao wakati mwingine siyo ya kawaida ya kuishi.

 

Vyanzo vyetu vimesema kwamba wangependa kupewa mafunzo ya kina katika maeneo mengi ya maisha yao ya ndani, mara tu wanapo pata nafasi ya kukaa kuishi ndani ya Maine, na hasa sana jinsi ya kuwa salama katika nyumba zao mpya. Kwa sasa, mafunzo mengi hufanyika kwa jaribio na hitilafu, ambayo inaweza kuwa hatari wakati wa kukabiliana na moto. Baadhi ya mafunzo wanayoomba inahusiana na usalama wa moto: jinsi ya kutumia kwa usalama na ufanisi vifaa vya kutumia umeme, ni nini kitambulisho cha moshi na nini la kufanya ikiwa wanaondoka, na namna gani ya kujibu kwa dharura ya moto. Maelekezo ya usalama wakati wa moto – kwa vifaa kama vile vizimya moto – huwa kawaida kwa Kiingereza na wala havipatikane kwa wengi ambao bado ni wahamiaji wapya. Wahamiaji wanaelezea kuwa makampuni ya Marekani haipaswi kufikiri kwamba kila yeyote anayekuja hapa ana ujuzi wa kukabiliana na moto, au kujua kusoma Kiingereza.

 

Zaidi ya hayo, wahamiaji wapya wangependa kupata mafunzo juu ya kuhifadhi matumizi ya nishati; kushughulikia uchafu toka nyumbani, ikiwemo mfumo wa kutengeneza upya chakata; kujua chakula gani ni cha afya na ni gani cha kuepukwa; na vipi usalama wa barabarani. Wakati mwingine kujua hata mambo madogo ya msingi ndani ya nyumba inaweza kuwa vigumu; kwa mfano, ni hali gani nzuri ya joto ndani ya jokofu, na ni chakula gani kinapaswa kuwekwa kwenye jokofu au kwenye friji. Mengi kati ya yale waonao kawaida wale waliokomalia hapa Maine huenda ikawa mambo ya kuchanganyisha kwa wahamiaji wapya.

 

Tumebarikiwa na maisha yetu na nyumba zetu, wala hatuwezi kukubali kuya poteza. Nyumba ni pahali pa maisha yetu ya ki binafsi na papo ndipo watu hutumia muda mwingi wa wakati wao. Nyumba zetu ndizo mahali tunapoweka kumbukumbu zetu nyingi na vitu ambavyo ni vya thamani na yenye kufaa kwetu. Ni mahali hapo ndipo tuna jiepushia baridi na pia hatari nyingine zozote ambazo zinaweza kututishia katika mazingira ya huko nje. Tunalala nyumbani mwetu kila usiku baada ya shughuli zetu za kila siku.

 

Sote tunataka kulinda nyumba zetu salama, kwa faida ya jamaa zetu na kwa jamii kwa ujumla. Tunapaswa kujitahidi kuungana mkono na kuzifanya jamii zetu zenye usalama na zenye nguvu kabisa. Hatuwezi kudhani kwamba kila yeyote huyo anajua jinsi ya kuwa salama katika nyumba za mbao, pamoja na jikoni za ndani na vifaa vya umeme. Kufahamu pamoja na ku elimishwa zaidi kuhusu usalama wa moto ni haja muhimu.