Kubeba gari ya Uber ama Lyft, na zinginezo gari za kukodishwa inaweza kuwa njia moja ya kupata faida kipesa. Lakini, yeyote afikiriyaye kuendesha gari ya kukodishwa anapaswa kwanza kuelewa mambo kadhaa kuhusu malipo ya bima. Kwa sababu wenye kukodisha gari hizi si wenyeji binafsi wa gari hizo, hawachukuwi madereva kama wafanyakazi wao. Kwa hio, kila mmoja aendeshae gari hizi huchukuliwa kama mfanyakazi binafsi, mwenye kujitegemea mwenyewe, hiyo yamaanisha kuwa kampuni haihusiki na hasara ya kifedha dereva huyo anaweza kumbana nayo, ikiwa hasara ya gari( kama kwa gari zingine) na majeraha ya kimwili9 kwa madereva wengine, abiria ama wenda kwa miguu)

Kawaida, huduma yoyote yenye kutafuta faida inataka bima ya kibiashara.kuliko bima ya kibinafsi, na mwenye kupana bima hiyo anataka malipo ya juu kwa sababu ya madai ya ajali- hatari ikiwa juu na malipo ni zaidi vilevile. Hatari ni kubwa zaidi kwa madereva hao kwa sababu muda wautumiyao barabarani ni mrefu, kwa hiyo bahati mbaya ya kupata ajali ni kubwa zaidi.Hata hivyo, wengi kati ya madereva wa Uber na Lyft hawawezi kumudu na hawana bima ya kibiashara.

Hivyo, nini ifikapo kwa dereva asababishae ajali anapoendesha gari ya kukodishwa?
• Yule ama wale ambao wamejeruhiwa wanapeleka malalamishi yao kwa bima binafsi ya mwendeshaji gari- iwe kwa hasara ya mali ama ya mwili, ama ya vyote pamoja. Idara husika ya kampuni ya bimainachunguza, na wakigundua kwamba gari ilikuwa imekodishwa, watakataa dai hilo. Zaidi ya hiyo, kampuni nyingi wataghairi bima ya huyo dereva kuwa hakuzingatia vizuri masharti ya mkataba. Dereva atajilipia mwenyewe kwa hasara na jeraha, na vilevile atakarabati gari za wenyewe kwa bei yao

Suluhisho, sasa, ni ipi?
Chache kati ya kampuni ya bima ya kibinafsi zimetowa jibu.Ijapokuwa hawafuniki gari hizo za kukodishwa kwenhye bima zao, wameidhinisha kidogo bima hizo kwa njia ya bima ya kibiashara. Yeyote aendeshae gari ya kukodishwa atakikana kuongeza udhibitisho huo kwenye sera zao, ama kujitayarisha kujilipia mwenyewe ajali inapotukia. Kwa hivyo, ikiwa unaendesha gari ya Uber, Lyft ama ingineo yote ya kukodishwa, ni lazima kuchunguza pamoja na mwenyeji wa bima yako na kuhakikisha unabeba uthibitisho huo kwenye sera zako