By Jean Damascene Hakuzimana

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyofunuliwa mwezi huu inaonyesha kwamba Sudan Kusini haijafanya maendeleo makubwa kuelekea uponyaji wa vidonda vya taifa hilo changa miaka kwa miwili baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua maisha ya watu 40,000 na kuwahamisha zaidi ya watu milioni mbili.

Jumuiya ya Wapasha habari( Associated Press) imeripoti kuwa badala ya uponyaji, nchi hiyo iko inagawanyika katika mikato ya ukabila, pamoja na wanasiasa wanaowapa silaha jamii kugongana wao kwa wao. Hii haitawashangaza wasomaji wa Amjambo Africa, ambayo imeripoti katika nakala zilizopita juu ya mgawanyiko wa viongozi wa kisiasa wa ngazi za juu wa Sudan Kusini kwa kitambulisho cha ukabila

Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini, ambayo iliwasilishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, inataja ufisadi uliokithiri kama hatari kwa uponyaji wa taifa, na inabainisha kuwa viongozi wa Sudan Kusini wanaonyesha nia ndogo la kisiasa kwa kushtaki uhalifu mkubwa, na badala ya hiyo wanaendelea hata sasa kuwapa silaha wanamgambo katika jamii zao.

Kulingana na ripoti hiyo hiyo, unyanyasaji wa kijinsia na uhaba wa chakula vinaendelea kuchochea mzozo unaozidi kuongezeka katika nchi, ambao inaorodheshwa kuwa kati ya nchi masikini zaidi kwenye faharisi ya maendeleo ya kibinadamu. Mbali na kule kuishi katika mizozo isiyo na mwisho, zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa Sudan Kusini wana njaa, hali ambayo ilizidishwa kuwa mbaya kutokana na mafuriko ambayo yamesababisha wengi kutoka majumbani mwao tangu mwezi wa Julai.

Wakaaji wapya wa Maine wenye asili ya Sudani Kusini ambao wamezungumza na Amjambo Africa siku zilizopita wakionyesha matumaini ya kupona kwa haraka kwa taifa baada ya viongozi hasimu kuvunja patano ya makubaliano ya amani mnamo Februari 2020 iliyolenga kumaliza migogoro ya silaha na kuiunda serikali ya umoja. Kinyume na matumaini hayo,ripoti ya Umoja wa Mataifa imefunua kuwa wahusika wa taifa wanaendelea kupeana silaha wanamgambo wa ndani kwa lengo la kushambulia jamii jirani. Na haya yote yanatokea licha ya vikwazo vya silaha vilivyoamriwa na Umoja wa Mataifa.

Serikali imetupia mbali ripoti ya Umoja wa Mataifa. “Ripoti hizi zote zimeandikwa na watu wanao keti vizuri katika hoteli za Juba. Wanaandika ripoti kama hizo ili kuhakikisha wanaendelea [katika nafasi zao], amesema ”msemaji wa serikali Michael Makuei, ambaye pia alithibitisha kuwa nchi kwa kweli inatekeleza makubaliano ya amani.

Nchi hii yenye utajiri wa mafuta inapambana na shida za kiuchumi, pamoja na kushuka kwa thamani kwa sarafu yake. Reuters inaripoti kuwa mnamo Julai 2020 benki kuu ya nchi iliishiwa na akiba ya fedha za kigeni. Baraza la Mawaziri lilikutana Ijumaa, Oktoba 9 na kukubali kupitisha sarafu mpya na kuacha pauni ya zamani ya Sudan Kusini ili kuokoa uchumi. Sudan Kusini ina akiba ya tatu kwa ukubwa wa hifadhi ya mafuta katika bara la Afrika, baada ya Nigeria na Libya.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa Sudan mnamo mwaka wa 2011 lakini ikaingia vitani tena miaka miwili baadaye, wakati Rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar walipoanza ugomvi kati yao. Baadaye, chini ya upatanishi, viongozi waliungana tena mikono katika juhudi za kutuliza nchi.

Inakubaliwa sana kuwa ikiwa nchi itapona, viongozi hao wawili watahitaji kutumika pamoja, na kwamba kile watakacho waambia makabila yao na wafuasi wao kitakuwa ufunguo wa mchakato wa amani.