By Jean Damascene Hakuzimana

Vyama vya siasa vya wapinzani vinagombana kabla ya uchaguzi wa rais na wa bunge uliopngwa kufanywa tarehe Mei 20 nchini Burundi, kulingana na Mtandao wa Televisheni wa Global China. Aljazeera anaripoti kwamba mapigano hayo ni pamoja na shambulio la mabomu ya tarehe Mei 11 iliyowauwa watu wawili kwenye baa katika mji mkuu wa Bujumbura.

Kwa kushindana kwa vyama vya siasa ni pamoja na chama chenye nguvu cha rais aliye na madaraka Conseil National Pour la Défense de la Démocratie (CNDD-FDD), na Baraza kuu la Upinzani la Kitaifa (CNL), chama kikuu cha upinzani, kinachoongozwa na Agathon Rwasa, kiongozi wa zamani wa waasi. Mikusanyiko mikubwa na hadhara zaendelea kufanywa licha ya tatizo la COVID-19. Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linashutumu chama tawala kwa kuchochea hofu kwa umma wakati wa uchaguzi unaoendelea na inaripoti mauaji inje ya vyombo vya sheria, kutoweka, ukatili wa kijinsia, utesaji, na kushikwa gerezani kiholela.
Nchi hii ya Afrika Mashariki inakwenda kupiga kura baada ya miaka ya machafuko na usalama mdogo kufuatia hatua ya mwaka wa 2015 wa Rais wa sasa Pierre Nkurunziza kwa

kuchukua hatua ya tatu mfululizo baada ya kunusurika kwa mapinduzi ya kijeshi iliyo endeshwa na mshirika wake wa zamani, Jemadari Niyombare. Tangu jaribio la mapinduzi hayo, Nkurunziza hajatoka nchini katika hali yoyote rasmi. Mara baada ya raia, kuamua kutoa maoni ya kisiasa yanayopingana na yalitolewa mara kwa mara hadharani, ulipuaji wa sasa wa chama tawala unaonekana kuwa na madhumuni ya kudhibiti na ujumuishaji wa madaraka.

Baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka wa 2015, Burundi ilimtuhumu hadharani jirani wake wa kaskazini Rwanda kwa kuhusika katika jaribio la kumuondoa Nkurunziza. Rwanda imekataa katukatu madai hayo, na kinyume ya hayo ikamushtaki Burundi kwa kutunza kundi la waasi, Kikosi cha uDemokrasi kwa Ukombozi wa Rwanda (FDLR), ambacho ni adui wa Rwanda. Mashutumu hayo yanaendelea, na vikosi vya jeshi za pande hizo mbili pambana namna isiyo ya kawaida. Mnamo tarehe Mei 8, askari walipambana na kuvuka mpaka usio halali wa ziwa Rweru, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Rwanda.

Burundi imewafukuza maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Haki za Binadamu mara kwa mara, na sasa hivi imepiga marufuku vyombo vya kimataifa vya utangazaji wa habari, kama vile Sauti ya Amerika, na BBC, ikiwatuhumu kujiingiza katika siasa za ndani. Mnamo tarehe Mei 12, Burundi ilimwondosha mkuu nchini wa Shirika la Afya Ulimwenguni na wafanyakazi wake bila kutoa maelezo yoyote, kulingana na ripoti iliyo tolewa na France 24.

na mwandishi wa Habari za Afrika Jean Damascene Hakuzimana akiandika kuhusu uchaguzi wa kiraisi na wa bunge wa