Naye Georges Budagu Makoko

Mauwaji ya George Floyd mnamo Mei 25 na afisa wa polisi wa Minneapolis ilikuwa ni ushahidi dhahiri wa unyanyasaji wa watu weusi na wale wenye kutekeleza sheria na mara kusababisha mawimbi ya mshtuko kokote Marekani na ulimwenguni kote. Mamilioni ya watu ilifurika mitaani kudai haki kwa ajili ya Floyd, pamoja na mabadiliko ya kimfumo kwa namna ambayo watu weusi hutendewa nchini Marekani, hasa kuhusiana na utekelezwaji wa sheria, ambapo utumiaji wa nguvu namna isiyo sawasawa umesababisha vifo vingi mno. Watu kokote nchini wameomba mabadiliko ya sera na taratibu zitekelezwe kwa haraka ili kuhakikisha kwamba kila raia nchini Marekani anatendewa sawa sawa.

Kama mtu ambaye alikuwa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo idadi kubwa ya mauaji yakutisha yaliyotukia yamefanyika mikononi mwa watu wasio na huruma, ilikuwa uchungu sana kwangu kutazama video ya kifo cha George Floyd. Kuona mtu asiye na tumaini, asiye na msaada akipondwa kwa ardhi, kwa uchungu na kuomba pasipo kusikiwa wamulindie maisha, ilikuwa shida sana na kunifanya nishangae kuhusu jukumu la maafisa wa polisi katika jamii ya watu weusi. Onyesho la afisa wa polisi akifinya shingo ya Floyd dhidi ya ardhi sio jambo ambalo ninaweza kusahau kwa urahisi. Ukweli ni kwamba afisa huyo wa polisi alisaidiwa na maafisa wengine, na inaonekana hakuwa na wasiwasi wowote juu ya waangalizi mashahidi wa kifo, hali wakiwaomba ma afisa hao wawe na moyo wa huruma, na wakichukua video ya mauwaji hayo, ilikuwa ya kusumbua zaidi. Hakuna kitu kili amsha dhamiri ya maafisa. Na kama mtu mweusi anaye lea mwanawe katika nchi hii, nashindwa kupata maneno ya kueleza namna gani mauaji haya yameweza kutokea, Kipekee inaonyesha picha kubwa ya ubaguzi wa rangi uliomo nchini Marekani.

Wakati maisha ya mwanadamu yanapopotea mikononi mwa watu wasio na huruma yoyote ile, hasira na huzuni zinazoshika wapendwa wa mwathirika huacha kumbukumbu zenye uchungu ambazo hukaa nao milele, na kuongeza maswali yasiyo na mwisho juu ya nini watu wengine wanawatenda ubaya kwa wanadamu wenzao. Oktoba 4, 2011 nilimpoteza binamu yangu, ambaye nilipenda sana, baada ya kuuawa mikononi mwa wanamgambo wa Mai Mai katika mkoa wa Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Binamu yangu aliuawa pamoja na wafanyikazi wengine saba wanaotoa huduma za kitaifa wasio na hatia. Waliteswa na kuuawa kikatili na kuachwa barabarani. Nafikiri dakika za mwisho za maisha yao, na dua zao kuomba rehema, ambazo hazikuzingatiwa wakati wanachukuliwa pumzi zao za mwisho.

Mamilioni ambao walio ingia mabarabarani katika karibu kila mji wa Marekani, hata ulimwenguni kote, wakati huu katikati ya janga la COVID-19 lililoko, wakiwatamani sana viongozi wa Marekani kurekebisha mfumo wa sasa wa utekelezaji wa sheria ili iweze hatimaye kuhakikisha usalama wa wote, bila ubaguzi wa rangi au taifa. Mabadiliko haya yanahitajika sana. Kwa wahamiaji, ambao wamehamia Amerika baada ya kukimbia kifo na mateso katika nchi zao, ni vigumu kuelezea watoto wao kwamba mambo waliyoyakimbia yanaweza bado kuzingatiwa hapa nchini Marekani. Wahamiaji hutumika kuishikilia nchi hii kama mfano wa viwango vya juu vya haki, na udemokrasia.

Maombi yangu ni kwamba nchi hii ninayoipenda sana itaungana siku moja, na mizizi ya mgawanyiko na ya migogoro haitapata tena ardhi yenye rutuba. Ubaya unakua wakati wowote haujabainika, na huu ni wakati wa kukabiliana na uovu wa ubaguzi wa rangi na kuushinda.