Nsiona Nguizani, Rais wa Jumuiya ya waAngola wa Maine, anakadiria kwamba kuna zaidi ya 2500 WaAngola wanaoishi Maine, na jamaa 629 zinazoomba hifadhi za ukimbizi zinasubiri. “Kila mwanaAngola humu Maine alikimbia toka nyumbani kwa sababu fulani,” amesema, “na mawazo ya hofu waliyo leta pamoja nao ni matokeo ya yale waliyoishi Angola.” Kwa msaada wa Manuel Kiambuwa, makamu wake, bwana Nguizani anatarajia kubadili mawazo hayo ya hofu. “Tunataka kuhimiza wageni kutumia ujuzi wao kusaidia Maine. WaAngola ni watu wenye akili, na wanao  mengi wanao weza kutoa. Tunataka watu wetu kuja pamoja na kuleta faida zao kwa serikali ya nchi hii ambayo imetusaidia wakati wetu wa mahitaji. ”

 

Wote wawili mabwana Kiambuwa na  Nguizani wanasisitiza kwamba waAngola wanaishi kwa hofu nyumbani, na kwamba huleta hisia hizo za hofu pamoja nao wakati walihamia hapa Maine. “Serikali haikufanyie kazi yoyote, ni udikteta tu, wanakubaliana kama inajifanyia kazi yenyewe.”  Wamefasiria kuwa nchini Angola watu wanaogopa polisi, kugawa maoni yao, mikutano ya kisiasa, ya mahakama, hakimu. Ikiwa unamwona mwandishi wa gazeti akija kwako nchini Angola, unakimbia mbali, wamesema, na kuongeza kwamba nchini Angola unaweza kuuawa ajili tu ya kutoa tu mawazo yako kwa sauti.

 

Kiambuwa na Nguizani wanasema kuwa kwa jumuiya yao  hitaji lao kubwa ni kuamini kuwa wako salama humu Maine, na kwamba mfumo hapa  ni tofauti na jinsi ilivyo kuwa Angola, na kwamba mtu wowote, ikiwa ni pamoja na wanaotafuta hifadhi, ana haki za kisheria. “Tunapaswa kusema tena na tena kwamba ‘wewe ni salama hapa,'” wanasema, lakini kuongeza kuwa ni vigumu sana kwa watu kuacha hofu yao nyuma yao. Hata hivyo, Kiambuwa na Nguizani wana matumaini makubwa kwa jumuiya ya waAngola nchini Maine. “Humo Angola serikali ilitaka kutuweka katika hali ya kugawanyika, na hivyo hatuwezi kufanya kazi pamoja kwa mfumo bora. Hii ina maana hatuna historia ya kuunganishwa pamoja, na inachukua muda kwa kujenga akili mpya. Hapa Maine tutajifunza kufanya kazi pamoja, “amesema Nguizani.

 

Wanaume hawa wawili walikutana hapa Maine, na Kiambuwa alishangaa sana na akili na ujuzi wa Nguizani kiasi kwamba alimshawishi kuongoza kazi kwa ofisi. “Kama wewe ni mtu wa akili, unapaswa kugawanya ujuzi wako,” alisema, akiongezea, “Yeye ni mtu mzuri anaye tusaidia.” Makamu wa Kiongozi Kiambuwa ameajiriwa kwa dakika ya mwisho, hivyo Kiambuwa akaingia ndani yake mwenyewe. “Sisi ni timu nzuri,” alisema. “Mimi ninamaliza muda wangu, na yeye ni mwepesi.” Nguizani anakubali. “Mimi ni muanzishaji tu. Mimi napitisha muda wangu mwingi kwa kufikiria namna gani ninavyoweza  kusaidia kizazi kinao kuja – jinsi ninavyoweza kufaa kwa watu wangu – tunataka kizazi kinachokuja kuangaza! ”

 

Jumuiya ya Angola ya Maine ilikuwa imelala kwa muda flani, na hali yake ya kisheria ikashindwa, hivyo baada ya kushinda uchaguzi, maafisa wapya waligeuka mawazo yao ya kwanza kurejesha ushirikiano wa chama chao na serikali. Sasa inakuja kazi ngumu ya kujenga shirika kutoka ndani. Wanaume wawili hawa hawana kitu kingine kama sio kustahimili, hata hivyo, nao wameamua kuwaleta pamoja watu wao na kukuza shirika lao. Kwanza kabisa, wanataka kuhakikisha kuwa wageni wapya wanaokuja Maine wanajua mahali pa kwenda kwa kupata msaada. Wanasema kuwa kila mtu wa Angola nchini Maine ni moja kwa moja mwanachama wa Jumuiya, hata hivyo wametambua kuwa watu wa Angola wanaogopa vyama, na wanaogopa kukusanyika, hivyo kushinda hofu  hiyo itakuwa muhimu kwa ukuaji wa shirika. “Jumuiya ni ya muhimu,” Nguizani amesema. “Huwezi kufanya hivyo peke yake huku Marekani.” Wanaume hawa wawili wanakubaliana juu ya malengo yao kuu. “Shirika letu halitakiwe  kuwa hapa tu kwa ajili ya karau, au kusaidiana kwa mazishi. Tunataka mambo yale, lakini zaidi tunataka kubadilisha Maine, kwa njia iliyo nzuri, kwa kutolea Serikali. Tunataka kusaidia wanachama wetu kujiunga na kikundi cha wafanya kazi na tunataka familia zetu kusaidia shule zibaki zenye kufunguliwa kwa kutuma watoto wetu kwao. ”

 

Wakichukuliwa pamoja, bwana Nguizani na bwana Kiambuwa wamekuwa nchini humu Marekani kwa miaka kumi, na wote wawili ni mifano bora ya maarifa na akili ambao Maine inahitaji kwa kikundi cha wafanya kazi. Bwana  Nsiona Nguizani aliwasili wa kwanza, Januari, 2012. Alipewa hifadhi, na sasa anaishi kama mkazi wa kudumu, alioa, na wanawe watatu ambao huenda shule Portland. Huko Angola, ambako alisoma shule la utunzaji na biashara, alikuwa miongoni mwa 1% ya idadi ya watu waliopata elimu ya juu. Amejenga kazi iliyo na mafanikio kama meneja wa mradi wa mashirika ya kiserikali ya matibabu na kazi kwa mashirika kama vile UNICEF, USAID, na EU, huko akisafiri kati ya ofisi za Paris na Luanda. Baadaye  alipo azimishwa kuikimbia Angola kutokana na tatizo na vurugo ya kisiasa, aligundua alipofikia Marekani kwamba angehitaji kuanza elimu yake tena na tena akitafuta kurudilia kiwango hicho hicho cha maisha alichokua nacho huko Angola. Alijisikia kutokuwa na furaha, ndipo aliamua kujifunza Kiingereza. Alipokosa kuorodheshwa alisubiri kuandikwa kwa shule la watu wazima wa Portland kwa muda wa miezi sita, aliamua bora kufundisha mwenyewe, ndipo aliangalia mafunzo ya GED nje ya maktaba, na mwaka wa 2013 alipata GED yake. Baadaye alipata shahada ya msaidizi katika mambo ya biashara na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Maine ya Kusini mwa Maine na mahitimu kwa uhasibu na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Kusini mwa Maine (USM). Ni wakati alikuwa kwa USM ndipo aligundua shauku yake mpya ya kiakili. “Nilipenda uchumi. Ime nipa maono pana ya dunia, “alivyo sema. Kwa sasa anafanya kazi katika kituo cha afya cha Maine  kama mwenye kuhusika na huduma kwa mgonjwa, lakini ni katika njia ya mpito kuelekea kwa kazi mpya.

 

Bwana Manuel Kiambuwa aliwasili Maine mnamo mwaka wa 2016 alipokuwa na umri wa miaka 25. Mwana pekee bado hai katika familia ya watoto sita, alichezea mchezo wa bahati nasibu, na nje ya waAngola 2000 ambao waliopima bahati yao, alikuwa mmoja wa watu wane ambao walichaguliwa, na mmoja kati ya watatu ambao waliokuja hapa Marekani. Alikuwa amemaliza miaka mitatu huko Angola kwa chuo kikuu kabla ya kuhamia, na mara alipofika hapa, aliamua kujua jinsi ya kuendelea na elimu yake – alijua kuwa anahitaji shahada ili kuanza kazi ya kuridhisha. Alipokuwa katika fani zake, alijitolea kwa muda kwa Elimu ya Watu wazima wa Lewiston, huko  akifundisha kuhusu kompyuta na teknolojia. Ya kufuata alihamia Portland, ambako alifanya kazi ya uhifadhi wa nyumba kunako hospitali ya Maine kwa muda wa miezi sita. Mchezaji maarufu  wa soka, alialikwa kujiunga na klabu ya mpira wa miguu huko Boston, na akahamia huko kwa muda, lakini alipotambua kwamba maisha huko Boston ni gharama ghali, na akifikiria alikuwa bado na umri mdogo ili kuanza kazi ya kitaaluma katika soka, alirudi Maine , na uamuzi wa kwenda katika usimamizi wa michezo. Kwa sasa anafanya kazi kama kocha wa soka kwenye shule la secondari la Portland, anafundisha lugha ya Kireno na pia ujuzi wa msingi wa kompyuta – kama vile matumizi ya Microsoft  na barua pepe – na hivi sasa anataka kupata shahada katika uchumi na usimamizi  pamoja na usimamizi wa michezo katika chuo kikuu cha Southern Maine Community College.

 

Ma bwana Kiambuwa na Nguizani wamechangia kuunda shirika isiyo ya faida, the International Fund for the Development and Modernization of Angola (IFDMA) “Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo na Uimarishaji wa Angola. Lengo ni kukusanya mchango kutoka duniani kote kusaidia mahitaji ya WaAngola walio baki huko nyumbani, na kujenga shule, viwanja wa michezo, na vituo vya michezo kusaidia vijana kufikia ndoto zao. Bwana Kiambuwa anasisitiza kuwa haitoshi kuishi kwa amani Maine, bali kwa wale ambao wameweza kukimbia wanapaswa kukumbuka watu ambao wamewaacha nyuma, na kujaribu kuwasaidia. Ana ndoto juu ya mabadilishano  kati ya Angola na Marekani, na ya kwamba nchi hizo mbili kujifunza kutoka kwa kila mmoja. “Tunataka kuonyesha jumuiya, nchi kuwa sisi ni nani, na nini tunaweza kutoa. Kama jamii, tunataka kushirikiana na serikali, na kuleta uwezekano na faida kwa Maine. ”

 

Angola ina moja ya jumuiya za wahamiaji inayoongezeka kwa kiasi kikuu humu Maine. Kutoka nchi ya watu milioni 30, ambayo ina tu 4-10% ya idadi ya watu wenye elimu, wale wanaokimbia nchi yao kwa sababu ya ukiukwaji wanaoteseka kwa mikono ya serikali yao na kufikia kupata usalama huko Maine wanakuna ujasiri na nguvu. Uongozi mpya wa Jumuiya ya waAngola wa Maine inatarajia kupunguza mpito wao kwa maisha yenye manufaa hapa, ambayo pia itafaidia Maine pia. Kwa maelezo ya mawasiliano, angalia kwa ukurasa wa Facebook wa Jumuiya ya Angola ya Maine.