Angela Okafor braids hair

“Kuonekana tofauti kunatokana na urembo wa asili pamoja na njia kujitengeneza bora”
Tamaduni ya kusuka nywele Afrika imekuwako tangu miaka maelfu. Zaidi ya kuwa mapambo, aina tofauti za kusuka nywele ilikuwa ki historia imehusishwa na kabila la mtu, umri, hali ya ndoa, utajiri, uwezo, dini, na / au nafasi kijamii. Mitindo ya nywele pia hubadilika kukiwako matukio maalum, kama vile ndoa, maandalizi ya vita, na sherehe nyinginezo za kijamii. Mfano wa kusuka nywele umekuwa mara kwa mara imara na wenye kufafanua, na katika bara ambapo maelfu ya makabila waliishi karibu wamoja na wengine, wanamemba wa kabila moja wapo wangeweza kutambua wanamemba wa kabila lingine kwa mtindo wa nywele zao. Kwa nyakati za sasa, kusuka nywele kumekuwa moja wapo wa biashara ya faida sana barani. Kwa jumla, kusuka nywele kumewekewa kwa wanawake, ila baadhi ya wanaume husuka nywele zao.
Wakazi wa Maine wenye asili ya KiAfrika wamesema kwamba walipofika hapa, walikuwa na shida ya kupata bidhaa ya nywele na vyumba vya urembo vilivyo na vifaa vya kutosha kwa kutunza na kutinda nywele zao. Wanasema kwamba walipaswa kutegemea marafiki kwa mtindo wa nywele zao, au labda wasafiri kwenda Boston au maeneo mengine ili kusuka nywele zao. Wamesema kwamba vyumba vya urembo hapa Maine vinavyo weza kutunza nywele za wa Afrika ni vichache sana. Hii inamaanisha kwamba wakati wowote kunapo kuwa harusi, watu huwa kama kwa mapambano kwa kupata chumba cha urembo, na kwa hiyo wanapaswa kusubiri kwenye mistari mirefu ili nywele zao zipate ku tengenezwa. Kanuni za kukataa leseni ziko ngumu, pamoja na vikwazo vya kusema lugha, inamaanisha kwamba wanawake wa kiAfrika walio na ujuzi wa kutengeneza nywele, na wenye uzoefu mkuu tangu nyumbani, hawajaweza bado kuwa na jinsi ya kuanzisha vyumba vya urembo hapa Maine.
Wanawake wa KiAfrika wanatambua kwamba kusuka nywele huwasaidia kulinda nywele zao wakati wa majira ya baridi na pia ni njia ya kukomboa muda, kila wakati inapowezekana kusuka mara moja baada ya miezi mitatu na bado inaonekana vizuri. Wametambua kwamba kukomboa muda katika nchi inayoendelea kama vile Marekani ni muhimu sana, na kwamba tofauti za nywele za wazungu, ambazo zinaweza kupambwa kwa urahisi kwa muda mfupi kila siku, nywele za KiAfrika zinahitaji muda wa kutosha na jitihada zaidi ikiwa hazi sukwe. Wameonyesha kuwa nia ya kuwepo zaidi vyumba vya urembo humu Maine kwa siku zijazo – kwa wazi, pamoja na zaidi ya Wazaliwa wa Kiafrika 10,000 wanaoishi katika jimbo, bila kuhesabu watoto wao, hii ni pengo inayotarajia kujazwa na wajasiriamali wenye kibali na wanaofurahia kufanya kazi na nywele .