Vegetables and fruits.

Wanasayansi hukubaliana kwamba chakula tunachoweka miilini mwetu kila siku, pamoja na mazingira tunamoishi, hufaa sana katika kuamua ikiwa tunaishi maisha mazuri na kuwa tuna muda mrefu wa kuishi ambao sisi sote tunataka. Hata hivyo, wahamiaji walio wengi hula vyakula visivyo vya kujenga afya humu nchini Marekani, kwa sababu hawazoei mfumo wetu wa ugavi wa chakula, pamoja na maandiko ya lishe juu ya vyakula, na kwa hiyo wako kwenye hatua ya ku hatarisha afya zao.
Afrika, watu wengi hununua chakula chao kwenye soko la umma. Chakula hicho kinauzwa na watu ambao wame kinunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima, na vyakula vyote hivyo ni kikaboni. Kwa maana watu wengi hawana chakula cha kutosha barani Afrika, vyakula vyenye afya vinaonekana kama vyenye kuwa na uzito katika protini, na wyenye thamani kuu ya kaloriki. Fetma sio shida ya kawaida. Watu hunywa maziwa wakati wanaweza, kwa kuwa ni gharama ghali, watu wengi hawawezi kuimudu, wakati hapa Marekani maziwa ni karibu sana, pamoja na kuwa watoto hupata kila siku maziwa shuleni yote pamoja chokoleti na maziwa ya wazi. Vinywaji vyenye sukari laini pia ni gharama ghali humo Afrika, kwa hivyo watu hawavinywi sana. Kwenye sehemu mojawapo za Afrika maji safi hupatikana kwa urahisi- hasa kwa wale walio nusurika kijamii – ila mara nyingi watu hupaswa kunywa ao maji machafu ao kuchemsha maji yale kabla ya kuyanywa
Milo ya watu mara nyingi hubadilika sana wakati wanafika Marekani. Vyakula vya kawaida huenda kuwa vigumu kupata, na mara hapo vinywaji vya sukari, vyakula vya kukaangwa, nyama, na vyakula vya kaloriki vingi hupatikana kwa urahisi. Wahamiaji mara nyingi hupunguza kula vyakula vya afya bila kutambua matokeo ya afya. Maandiko ya lishe juu ya chakula haipo Afrika, na Waafrika wengi wanao hamia hapa hawajui jinsi ya kuyasoma. Pia, kwa sababu sio sehemu ya utamaduni wa kiAfrika, walio wengi hupuuza kabisa maandiko hayo. Hata hivyo, maandiko haya yote ni katika lugha ya Kiingereza, na kwa hiyo haufikiki kwa wengi wa wahamiaji wapya.
Hata hivyo, kama Wamarekani, kila mtu hutaka kuwa na afya njema, na wageni wapya tulio sema hapo wangependa kupewa mafunzo juu ya jinsi ya kujua kuchagua chakula bora cha afya kwa familia zao hapa Marekani. Wangependa kufunzwa jinsi ya kusoma maandiko ili waweze kuelewa ukubwa wa kuwahudumia, kalori na maudhui ya sodiamu, na thamani ya lishe katika vyakula ya kila siku. Watu pia wangependa kujua zaidi kwa ujumla kuhusu viungo vilivyomo katika vyakula vinavyouzwa hapa ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa kwenda sokoni kununua chakula. Mara nyingi wageni wapya wanahisi kabisa kuwa wameshtushwa na kile wanachokiona katika njia baina ya maduka makubwa.
Wahamiaji kutoka Afrika wameelekeza kwamba elimu zaidi inahitajika ili kukuza afya ya kula na namna ya kuishi kwa jamii zao pia wanawahimiza wageni wapya kutafuta ushauri wa matibabu kutoka kwa watoa huduma za afya. Wameelekeza pia kwamba watoa huduma za afya waandae mipango inayolenga kuwasaidia wageni wapya kujifunza jinsi ya kupitia mfumo wetu wa usambazaji wa chakula. Wamependekeza kwamba madaktari waongee na wagonjwa wao kuhusu mwanzo wa tabia nzuri ya kula na hali ya maisha wakati wanahamia katika nchi hii. Ushauri wa msingi: kunywa maji badala ya soda, punguza juisi, epuka vyakula vya kukaanga, epuka vyakula vinavyotengenezwa kama vidonge na ndazi zilizofungwa mu vifurushi, kupunguza vyakula vya kukaanga, kupunguza utumiaji wa nyama nyekundu, kula huduma ya vyakula vitano vya matunda na mboga kwa siku, kudhibiti unywaji wa pombe za kulevya na pia kufanya mazoezi ya mwili kila siku .