“Ibuye ribonetse ntiryica isuka, translated”
Jiwe lililotambuliwa haliwezi umiza jembe

Machi tarehe 12 ilikuwa siku ambayo janga kubwa hili la ugonjwa wa Covid-19 liligonga rasmi jimbo letu la Maine ikiwa na kesi yake ya kwanza. Mara tu baada ya hapo, katika matumaini ya kulinda kila mtu kuwa na afya na usalama, Gavana Janet Mills alitangaza hali ya hatari. Katika wiki za kwanza kwanza, woga la lisilojulikana bado ilionekana dhahiri kwenye nyuso wa watu. Hakuna mtu aliyejua bado jinsi gani virusi hivi vitatugusa, na sote tulitaka kujifunza jinsi ya kujilinda, pamoja na wapendwa wetu, kutokana na hatari hii. Kituo cha Maine cha Udhibiti wa Magonjwa kilipendekeza hatua za kinga ambazo tumezoea sasa – utengamano wa kijamii, kunawa mikono mara kwa mara, kufunika kikohozi na chafya, pia na takasa maeneo yanayoweza kuguswa. Zaidi ya yote, kukaa nyumbani ilipendekezwa sana kama njia bora zaidi ya kukaa salama mbali na virusi.

Kwa bahati mbaya, kukaa nyumbani ilikuwa vigumu sana kwa watu wengi wenye rangi. Ingawa mashirika na taasisi nyingi, za kibinafsi na za umma, zilichukua hatua kali kwa kufunga milango yao, na kuwaomba wafanyakazi wao waanze kufanya kazi wakiwa nyumbani, biashara muhimu kwenye mstari wa mbele – huduma za afya, maduka ya mboga, nyumba za kikundi, viwanda vya utengenzaji chakula – vilibaki bila kufungwa. Na katika Maine, biashara muhimu hivyo huhudumiwa sana na watu wenye rangi.

Wakati kesi ya kwanza ilipotangazwa huko Maine, kila mtu – watu wa rangi kama vile na watu weupe – waliambiwa na Gavana Mills na Mkurugenzi wa CDC Daktari Nirav Shah, kwamba virusi havikubagua awaye yote ule. Na katika siku za mwanzoni, watu wengi waliamini kuwa hiyo ni kweli. Hatukujua wakati huo kwamba virusi vita shambulia watu kutoka kwa jamii zetu isivyosawa. Halafu, virusi vilipo pandisha mvuke wake huko Maine, na visa vingi zaidi vilipogunduliwa, data kutoka kwa Maine CDC ilianza kufunua tofauti za kutisha ya jinsi watu weupe na watu wa rangi wamepigwa na virusi.

Katika Maine, watu wa rangi, ambao huwa tu asilimia 7% ya idadi ya watu, sasa wanahesabiwa kuwa zaidi ya asilimia 32% ya jumla ya idadi ya kesi za Covid-19. Sababu za athari hii isiyo na kipimo ni pamoja na hali ambayo watu wengi wa rangi waishi ndani kwa sababu ya hali ngumu ya kifedha,inayo wa fanya kutengwa ao kujifungia nyumbani kuwa vigumu; upatikanaji duni wa huduma za afya, iki sababisha hali mbovu ya matibabu; hali wakiendelea kufanya kazi katika huduma za mstari wa mbele licha kuwa tia hatarini kwa sababu ya mahitaji ya kifedha. Kwa namna ingine, matokeo haya yanahusiana na sera za ubaguzi wa rangi.

Viongozi wa wahamiaji, viongozi wa waLatino, viongozi wa Kikabila, na viongozi kutoka jamii ya Wamarekani wa asili na jamii wenye asili ya KiAfrika wote wana wasiwasi kubwa sana ajili ya afya na usalama wa watu wao. Hivi majuzi viongozi hao walishiriki mkutano wa waandishi wa habari, ambapo walielezea wasiwasi wao mkubwa, ikiwemo pamoja na maeneo muhimu ambayo huwaathiri kijamii na kiuchumi na ambayo ni lazima ibadilishwe, na walimuoba Gavana Mills kufanya kazi pamoja nao ili kuzuia uharibifu zaidi hapo mbeleni.

Hivi karibuni, nilijadili kuhusu ubaguzi wa rangi, na jinsi gani ya kubadilisha mfumo huo, na Rev Kenneth I. Lewis, Jr., Mchungaji Mwandamizi kwa Kanisa la Green Memorial African Methodist Episcopal Zion huko Portland (kiunga na mahojiano kwenye wavuti), ambaye aliteuliwa na Gavana Mills mnamo Juni 30 kwa Tume ya Kudumu ya kuchunguza Hali ya Makabila, ya kiAsili, na Mataifa ya kikabila ya Maine, ambayo inalenga kushughulikia ukosefu wa kutendewa sawasawa uliomo Maine. Mchungaji Lewis alizungumzia juu ya hitaji lililoko la viongozi weusi kutoka jamii tofauti huko Maine – wakiwemo wahamiaji na wa Marekani wa Asili ya Kiafrika – kuungana, akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi pamoja kwa niaba ya jamii nzima kusemesha ukweli ili ku pinga kwa nguvu ubaguzi wa rangi huko Maine.

Ninawasihi watu wote wa rangi kuungana na kutumia sauti yetu ya pamoja kutetea kwa sauti ajili ya mabadiliko tunayoyahitaji kuona yanatokea katika jamii yetu ya Maine.