Baada ya karibuni miaka 50 ya vita vya utumiaji silaha na machafuko mengi ya kiraia yasiokoma, hatua za hivi karibuni za kurudisha tena mamlaka ya kiserikali, zimeambatana na ongezeko la juhudi za kimataifa za ulinzi wa amani katika mkoa huo, ambazo zimeleta utulivu mdogo kwa Somali. Wakichukua fursa hii ya utulivu mdogo ulioko, nchi inachunguza njia ya uchimbaji wa mafuta na gesi kwa pwani iliyo nje ya nchi, huko ikitazamia kuvutia uwekezaji uchumi kwa wageni, kulingana na offshore-technology.com, ambayo inaripoti kwamba Somalia imo miongoni mwa maeneo mabaki machache ulimwenguni iliyo bado na uwezo mkuu wa rasilimali ambazo bado hazijashughulikiwa.

Mnamo mwezi wa Mei, Wizara ya Somalia ya Petroli na Rasilimali za Madini ilitangaza zabuni ya leseni ya pwani ifikapo Agosti 2020 kulingana na matetezi ya ukaribu wake na Yemen ambayo ni taifa lenye utajiri wa mafuta, Somalia inaweza pia kuwa na utajiri wa mafuta na gesi. Serikali imeridhia sheria mpya ya mafuta, ambayo imeanzisha Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Somalia. Kabla ya machafuko ya ki raia ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilianza mwaka wa 1960, nchi ilikuwaka ikiwekezwa uchumi wake katika uchimbaji wa visima vya mafuta kwenye pwani kwa kushirikiana na ma kampuni kama vile ExxonMobil, BP, Texaco, na Shell. Kampuni hizi zina matumaini ya kupata msingi wa pamoja na Somalia ya karne ya 21 na kulea hii roho mpya ya uchunguzi.

Walakini, licha ya maendeleo ya kiuchumi ya Somalia, wataalam wanaziona changamoto hapo mbele. Somalia iko kwenye Pembe la Afrika, na pia ni jirani ya Kenya na Ethiopia, vivyo hivyo na Yemen isiyo na utulivu ikiwako hapo ngambo kwenye Ghuba ya Aden. Tena sio vyama vyote vinavyo angalia kwa jicho nzuri kuanzishwa upya shauku katika mafuta na gesi – Somalia inakabiliana na vinyume vya mapigano kutoka Puntland na Jubbaland. Na zaidi ya hayo, Somalia na Kenya zimo katika mabishano juu ya mpaka wao baharini. Juu ya changamoto zingine, COVID-19 imepunguza mwendo wa biashara, wakati ambapo Somalia inakabiliwa na kuongezeka kwa kesi za COVID-19. Na Al Shabab, ambalo ni shirika la wanamgambo, bado linaendesha shughuli zake nchini Somalia, nalo limewauwa watu wengi.