Mfuko wa Kufufua Restorenti (RFF) ni sehemu ya sheria ya Mpango wa Uokoaji wa Marekani iliotiwa saini ya Sheria mnamo Machi 11, 2021, sheria hiyo ilichukuwa dola bilioni 28.8 kusaidia upokeaji wageni unaostahiki na biashara ya tasnia ya huduma ya chakula iliyoathiriwa na janga hilo. RFF inasimamiwa na Utawala wa Biashara Ndogo (SBA). SBA inaweza kutoa uhifadhi kutoka $1,000 hadi $ 5 milioni kwa kila mwombaji eneo la biashara, au hadi $milioni 10 jumla kwa kila mwombaji. RFF itaendelea kutumika hadi mfuko utakapoishiwa na pesa. Tuzo zinapaswa kutumiwa ifikapo Machi 11, 2023 kwa matumizi yaliopatikana kati ya Februari 15, 2020na Machi 11, 2023. Fedha ambazo hazikutumika zitarudishwa kwa serikaliya MarekaniNani anastahiki?
Restorenti nyingi, baa, mkate, upishi, lori la kubeba chakula au stendi, pombe , vilabu au nyumba za wageni zinazomilikiwa na watu binafsi na uuzaji wa chakula kwenye tovuti zinastahili kuomba. Waombaji lazima wawe wa aina zifuatazo za ushuru ili kustahiki

• C-Mashirika au Mashirika chini ya mashirika mengine
• Ushirikiano
• Kampuni ndogo za Dhima(pamoja na ushuru kama mashirika madogo na wamiliki pekee)
• Wamiliki pekee
• Watu waliojiajiri wenyewe
• Makandarasi wakujitegemea

Waomabji wote lazima wahakikishe kuwa kutokuwa na uhakika wa sasa wa kiuchumi hufanya ombi la ufadhili kuwa muhimu kusaidia shuguli zinazoendelea au zinazotarajiwa

Ni nani asiyefaa ?
Kusudi la RFF ni kusaidia wafanyabiashara wadogo, biashara za jamaa, na wajasiriamali. Ikiwa mwombaji ni :
Biashara inayoendeshwa na Serikali au serikali za mitaa;
Mmiliki au mwendeshaji wa zaidi ya maeneo 20 ya biashara, katika tasnia yoyote;

Kampuni iliyouzwa hadharani;
Imefungwa kabisa(hii haijumuishe kufungwa kwa muda sababu ya amri za kukaa nyumbani);
Shirika lisilo la faida

Basi mwombaji hana haki ya kufadhiliwa kupitia RFF.
Vizuizi vingine ni pamoja na kufungua jadala la kupitishwa kwa kufilisika kwa sura ya 7, au kufilisika kwa sura ya 11,12 au 13 isiofanya kazi chini ya mpango wa ulipaji ulioidhirishwa. Lakini, waombaji wa mpango wa kufilisika ambao wanakamilisha mpango uliodhinishwa wa kujipanga upya wanastahili kuomba RFF

Pesa hizo zitafunika nini?
Tuzo za RRF zinaweza kutumiwa kwa gharama zozote zifuatazo muhimu kwa kuendesha biashara ndogo. Baadhi ya gharama hizo ni:

• Mishahara, vifaa vya biashara, gharama za chakula na vinywaji, huduma na gharama za uendeshaji
• Gharama za ujenzi zinazohusiana na kudumisha huduma ya nje au kijamii
• Kulipa deni zozote zilizopatikana wakati wa janga hilo

Gharama zisizostahiki ni pamoja na:

 

• Gharama za upanuzi
• Malipo ya malipo ya kwanza juu ya deni zilizokusanywa kabla ya janga hilo

  Je! Pesa za ufadhili wa PPP za zamani zina changamoto gani kwa tuzo ?

 

Wote kati ya wafanyabiashara ambao walipokea mkopo wa Mpango wa Ulinzi wa Malipo mwaka 2020  watapunguzwa kiasi cha mkopo kutoka tuzo yao ya mwisho kupitia RRF. Waomabji wanathibitishwa kwa kutumia EIN(Nambari ya Kitambulisho cha Mwajiri) inayotumiwa kwa programu ya PPP.

Ikiwa mfanyabiashara anashirik katika programu zingine zinazosimamiwa na SBA itataathiri kustahiki kwake. Maswali yanaweza kuelekezwa kwa SBA ya Maine

 

 

How to apply

Unaweza kuombaje?

  • Moja kwa moja kupitia Jukwaa la SBA kwenye restaurant.sba.gov
  • Kupitia Muuzaji wa Uuzaji(ni akina nani hawa?)
  • SBA inatafuta kikamilifu kushirikiana na watoa huduma zaidi wa POS
  • Kupitia simu kwa (844) 279-8898
  • Programu za simu zitakuwa na nyakati ndefu za usidikaji

For more information and assistance:

Kwa  usaidiaji na taarifa zaidi

Tembelea SBA mkondoni kwa habari zaidi

https://www.sba.gov/funding-programs/loans/covid-19-relief-options/restaurant-revilitalization-fund