Wakati wote wa utoto wake, Belyse Ndayikunda alijuwa kwamba familia yake itakuwa naye siku zote. Basi, alipofika umri wa kuwa kijana katika nchi yake ya Burundi, wazazi wake waliamua kumpeleka yeye na kaka yake mkubwa huko Marekani kwa ajili ya usalama. Alipofika Portland, alipelekwa kwenye makazi, na akapewa godoro kulala. Anakumbuka alivyo hisi huzuni, na kujisikia kama kuwa hatarini. Mwaka huo ulikuwa wa 2012, alipokuwa mbali na kile alichokiita “kijiji cha msaada” – yaani wazazi wake, marafiki zake wa utoto, na jamii – hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha yake. Bi Ndayikunda alikuwa na na umri wa miaka 18.
Huko kwenye makazi, mtu mmoja asiye na makao alimusogelea. Aka mwambia huyu mgeni wa miaka 18 makosa yote aliyoyafanya maishani mwake, hata kufikia kupoteza kazi, familia, marafiki, na ukoo wake kwa sababu ya ulevi na kutumia dawa za kulevya. Yale Bi Ndayikunda aliyoyaona kandokando yake siku ile ya kwanza ilikuwa tofauti kabisa na yale aliyo yaona katika sinema kutoka Amerika, na alipata shida kupatanisha kile alichofikiria anajua kuhusu Amerika na yale aliyokuwa anayapitia akiwa kwenye makazi. Bi Ndayikunda alisema kuwa siku hizo nne alizo kaa kwenye makazi zilikuwa kama simu ya kumuamsha. Aligundua kuwa ikiwa hatakuwa mwangalifu kufanya maamuzi sahihi, anaweza kuishia katika hali mbaya sana. Baada ya siku nne, akapewa msaada kutoka (GA) kwa kupata chumba kwenye Bayside village, ambapo wanafunzi wengi waliishi. Walimsaidia pia ndugu yake kupata chumba, na mara wakawapa voucha kwa ajili ya chakula, na maelekezo nafuu kuwaongoza mahali pa kupata huduma mbalimbali.
Rafiki mmoja wa familia anayeishi Portland alimchukua na kumupeleka hadi Deering High School, pia akamsaidia kujiandikisha shuleni. Papo hapo alishangazwa na vitu vingi vilivyomo katika mfumo wa shule ya Amerika: huko Burundi, walimu ni wenye mamlaka, na wanafunzi huogopeshwa nao. Hapa, aligundua kwamba wanafunzi wana karibia waalimu wao, na wanahusiana nao kwa urahisi. Kunako Deering, kulikuwa na wanafunzi kama 10 hadi 15 darasani, wakati nchini Burundi amezoea kuwaona wanafunzi 40 kwa darasa moja. Huko Deering wanafunzi wanahama kutoka darasa kwenda darasa lingine. Wakati huko Burundi wanafunzi walikaa, na waalimu wanawajia. Na kisha kulikuwa na kiasi kikubwa cha maelekezokinacho patikana kwa wanafunzi na walimu hapo Deering. Kwa kila kitu kuhusu shule hiyo mpya ilionekana ya kushangaza.
Mwanzoni, kiwango chake cha kuongea Kiingereza cha chini kilifanya shule iwe ngumu sana, lakini alijikumbusha kila wakati kwamba ilimu bidi afanye vizuri, na hivi alisoma kwa bidii. Polepole, alifanya maendeleo. Akijua kwamba wanaotafuta hifadhi hawastahiki kupata misaada ya kifedha ya kwenda chuo kikuu, basi aliomba, na alikubaliwa. Alipojua kwamba hangeweza kuhudhuria, tumaini na ndoto zake zilianguka. Washauri wake hawakujua jinsi ya kumsaidia. Halafu ndipo mtu mmoja alisema kwamba Chuo cha kiJamii cha Maine cha Kusini (SMCC) kilikuwa na programu inayoitwa Njia ya Kuendea mahitimu kwa wanafunzi walio tayari kwenye vyuo, na akapewa udhamini wa $500. Wakati akichukua madarasa huko, alikutana na Kristi Kaeppel, mshauri ambaye alijitoa kumtetea, na kumuunga mkono, na kumsaidia kupata mali ya kuendelea na shule. Bi Kapper aliendea kuhitimu shule yake mwenyewe, lakini sio kabla ya kuunda uhamasishaji katika SMCC zaidi juu ya changamoto zinazowakabili waombaji hifadhi. SMCC ilijibu kwa kuanzisha mfuko pesa maalum.
Belyse Ndayikunda alihitimu kutoka SMCC baada ya miaka mbili, na kwa msaada wa Margaret (Maggie) Loeffholz akahamishiwa Chuo Kikuu cha Maine ya Kusini (USM), ambapo alipata udhamini wa $2500 kwa sababu ya alama zake bora. Wakati akiwa USM, alitafuta – na kupata – pesa kutoka kwa wafadhili wa kibinafsi mbalimbali, wengine walimfahamu, na wengine la. Kwa miaka mitatu alisoma na kufanya kazi, na mwishowe mnamo 2018 alihitimu na digrii ya bachelor kwenye Hesabu na mkusanyiko wa takwimu. Bi Ndayikunda sasa anafanya kazi kwa UNUM. Yeye anatarajia kupata digrii ya Master, na ameomba kwa mpango wa masomo, mkopo wa kurudishwa unaotolewa na UNUM kama msaada.
Kutumika wakati mtu anakwenda shuleni ilikuwa ngumu sana, alisema, lakini aliegemea imani yake, watu wazuri aliokutana nao, na azimio lake, kwa mafanikio yake. Ushauri wake kwa wengine, zaidi wanaoomba hifadhi ya ukimbizi, ni kutokukata tamaa. Ni kushikilia ndoto kila yule, kufanya kazi kwa bidii, kutumia mitandao, na kugonga kila mlango unaowezekana, zote saidia majukumu muhimu kumwezesha kupata elimu. Aliongeza kuwa Wamarekani ni wakarimu na wenye moyo mwema, na ikiwa unashirikisha wengine hadithi yako, watu wengi wako tayari kusaidia. Alikumbuka tukio aliyohudhuria ambapo alieleza hadithi yake kama sehemu ya jopo. Baada ya hapo tu, mtu alimkaribia na kumpa cheki ya $2000 ili aendelee na masomo yake.
Bi Ndayikunda alisema alishikwa na huzuni wakati anaposikia juu ya vijana ambao huacha shule. Baadhi ya wanao acha shule wamo wataalam ambao wanastahili msaada wa kifedha – hasa hasa wanaotafuta hifadhi – na anafikiria kwamba wanakosa nafasi kubwa kwa kutofuata masomo ya juu. Anafurahishwa kuona kwamba watu kadhaa na mashirika mengi sasa wanajua vizuizi vya misaada ya kifedha inayo wakabili wanaoomba hifadhi, na amebaini kuwa programu maalum sasa zinaundwa. Alisema kuwa mahitimu yake kutoka USM ilikuwa moja ya siku bora za maisha yake. Alielewa hivyo kwamba ikiwa angeweza kupata digrii ya bachelor chini ya masharti aliyolazimishwa kuwemo uzoefu, angeweza kufanikiwa kwa kitu chochote kile hapa Amerika. Kuchapa kazi kwa nguvu kunalipa, alisema.