Ramadhani ni mwezi kipekee wa kiroho hasa kwa Waislamu. Mwaka huu, Ramadhani ilianza Marekani jioni ya Mei 5 na kumalizika tarehe 4 Juni, wakati wa mwezi uliopungua. Kalenda ya Kiislam niyaegemea mwezi, hivyo siku hubadilika mwaka kwa mwaka.
Wakati wa mwezi wa Ramadhani, Waislamu wanajaribu kuimarisha uhusiano wao na Allah (jina la Kiarabu kwa Mungu) na kuishi kama Uislamu unavyofundisha. Ukumbusho wa Ramadhani ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu – Ni mojawapo ya majukumu makuu zaidi yanayohusishwa na mutu kuwa Muiislam. Uislamu inasisitiza umuhimu wa kuwa na moyo wa usaidizi kwa wengine, na Waislamu wanaamini kuwa kufunga wakati wa Ramadhani huwasaidia kujifunza kuwa wenyewe kuwa na moyo wa usaidizi
Kwa mujibu wa Mohamed Awil, makamu wa katibu tendaji mkuu wa Gateway Community Services, ambaye amekuwa katika saumu ya Ramadhani tangu akiwa na umri wa miaka 13, “Ramadan ni kuhusu shukrani, kuwa kama katika viatu vya watu wasio na chakula chochote kwa masiku kadhaa . Wale ambao wanaokula kila siku wanabahatika kuwa na kile tulicho nacho. ”
Wakati wa Ramadhani Waislamu wengi wanahudhuria msikiti mara nyingi, wakijaribu kusoma Qur’ani anzia mwanzo hadi mwisho (kwa wamoja zaidi ya mara moja), ili kukuza hali yao ya utoaji wa misaada, na kwa ujumla hujitahidi kujizuia. Wazo ni kuzingatia sana uhusiano wa mtu na Mungu. Kulingana na Uislamu, Ramadhani inaadhimisha mwezi ambapo Qur’ani, Kitabu Kitakatifu cha Uislam, ilifunuliwa mara ya kwanza kwa Waislam kupitia Malaika Gabriel kwa Mtume Muhammad. Kwa hiyo, inachukuliwa kuwa mwezi mbarikiwa, na kwa Waislamu wengi, ni mwezi wa furaha.
Wale wanaofunga hawakule chochote kwa ajili ya miili yao kutoka jua kupambazuka hadi jua kutwa kila mwezi, wakiamini kuwa njaa na kiu wanayopata wakati wa kufunga huwafundisha kuwa na huruma. Makundi fulani ya watu huruhusiwa kutofunga, Ni kama vile watoto ambao hawajafikia ujana, watu wazima ambao ni wagonjwa, na wazee. Wakati wa jua kutwa kila siku Waislamu wanafungua kwa muda, kwanza kwa chakula kidogo kabla ya sala, na baadaye kwa chakula kingi na kikubwa – kinachoitwa Iftar (Futuru) – kinachoshirikiwa na marafiki na familia. Milo ya jioni ni kama ya sherehe na yenye ukarimu
Gavana Mills alihudhuria chakula cha kwanza cha jioni cha Iftar (Futuru) kunako Blaine House ilipokuwa Jumapili, Mei 19, kwa niaba ya viongozi wa jumuiya ya Waislamu wa Maine. Tukio hili lilipata sifa kubwa kutoka kwa jumuiya ya Kiislamu huko Maine kwa sababu ilionyesha hatua ya kujitoa kwa Gavana kukuza ushirikishwaji.
Inza Ouattara, Mratibu wa Afya kwa Wakimbizi wa Maine kunako kikundi cha misaada ya ki Katoliki pa Maine akiwa pia kiongozi ya wazaliwa wa Ivory coast wanaoishi Maine, alikubaliana na bwana Ahmadov. “Mimi mwenyewe nilifurahishwa sana na mwaliko wa Blaine House,” Bwana Ouattara alisema. “Tukio lilikuwa la kugusa sana. Ninashukuru sana kuwa Gavana Mills huwa anajaribu kujenga jumuiya ya umoja wa makabila katika Maine. Chakula cha jioni cha Iftar (Futari) kilikuwa na tukio/athari kubwa katika jumuiya ya Kiislamu. ”
Mratibu wa Misaada ya kiKatoliki kwa Wakimbizi wa Jimbo la Maine Tarlan Ahmadov, aliye kuwa wa muhimu sana katika kupanga chakula cha jioni, alisema, “Gavana yuko anaunganisha jamii na kujenga hali imara ya jimbo kwa siku zijazo. Kiongozi wa kweli na mwenye busara daima huwaleta watu pamoja, na kuimarisha amani na maelewano. ”
Idadi ya waislamu wa Maine ni ya kawaida. Reza Jalali, mwandishi na profesa, anafikiria kwamba Waislam kati ya 7,000 na 8,000 wanaishi Maine kwa sasa. Anasema wanatoka Somalia, Iraq, Sudan, Ghana, Afghanistan, Iran, Kenya, Bosnia, Kosovo, Bangladesh, Syria, Lebanon, India, Pakistan, Misri, Uturuki, Jamhuri ya Azerbaijan na Malaysia. Anakadiria kuwako na msikiti 10 humu Maine, na kwamba vyuo vikuu vyote vya umma na vya kibinafsi nchini huwa na vyama vya mwanafunzi wa Kiislam. Aina mbalimbali za mashirika yaliyohifadhi chakula cha Iftar (Futari) wakati wa mwezi wa Ramadhani. Kwa mfano, huduma za Jumuiya za kiHifadhi zilihudhuria chakula cha Iftar(Futari) kwa Waislamu na wasio Waislamu sawa na siku ya Juni 1 ambayo ilionyesha “chakula, imani, na utamaduni,” kwa maneno yake Abdullahi Ali.
“Uislam unaunganisha Waislamu wote, bila kujali wanatokea nchi gani,” alisema Bwana Ouattara. “Kwa mimi, kuwa Mwislamu huko Maine ni kama kuwa Mwislamu popote pale. Uislamu hufundisha kwamba popote unapoishi, unapashwa kufuata na kutii sheria za mahali unapoishi, kwa hivyo kama Waislam tunazingatia na kutii sheria za Maine. Kwa mfano, hapa unapaswa kwenda shambani ili kuchinja kondoo mume kwa ajili ya Ramadhani. ”
Waislamu duniani kote humaliza Ramadani kila mwaka na sherehe ya Eid-al-Fitr, siku kuu tatu ya sherehe, wakati ambapo wanaadhimisha utoaji wa misaada kwa watu maskini (nyingine ya nguzo tano za Uislamu), kuomba, kuvaa mavazi mazuri, kutembelea marafiki na jamaa, na kusherekea sikukuu. Mamia walikusanyika kwenye jengo la Expo la Portland asubuhi ya Juni tarehe 4 kuomba na kusherehekea. Karibu watu 175 katika eneo la Augusta walifurahia chakula, marafiki, familia, na furaha katika Mradi wa Sherehe ya Eid kwenye maeneo makuu ya Eneo Mupya ya watu wapya wa Maine tariki 7 mwezi wa Juni. Kunako Juni tarehe 8, Ushirikiano wa Vijana wa ukoo wa Somalia na Sudan walishirikiana na kuhudhuria sherehe ya Eid inayoongozwa na vijana . Shirika la New American Arab American (NEAAO) lilifanya sherehe ya Eid Juni 9 ambapo iliburudisha kwa muziki ulio hai, vyakula vya ki Mediterranea, na pia shughuli za kufurahisha kwa ajili ya watoto.

Samar Ahmed, Suzan Ali, Maryan Bashir, Eklas Ahmed Photo by John Ochira

Adam and Diana Lee celebrate Eid with New England Arab American Organization. Photo by Hamid Karimian @OpenVisionstudios

Iftar dinner at Blaine House with Governor Janet Mills

Fun at the Capital Area New Mainers Project’s Eid celebration in Augusta

Iftar dinner at East End Community School hosted by Samar Ahmed and Suzan Ali of Sudanese Roots Photo by John Ochira

Hanna Tallan, Ekhlas Ahmed, and Samar Ahmed. Photo by John Ochira

Zoe Sahloul, President and Founder of New England Arab American Organization and Jenn McAdoo, board member. Photo by Hamid Karimian @OpenVisionstudios

Mohamed Khalid and Yusuf Muse Yusuf at Iftar dinner at Gateway Community Service

Kids have fun at Eid celebration at Riverton School – Hosted by Sudanese Roots and Somali Mainer’s Youth Network.