Chini ya sheria ya shirikisho, watu ambao si raia wa Marekani, lakini wanaojiandikisha kupiga kura AU wanaopiga kura katika uchaguzi wowote wa Marekani (ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa eneo, jimbo na shirikisho) wanaweza kufukuzwa nchini. Sheria haiwasamehe wasio raia ambao hawakuelewa sheria za kustahiki, au walioambiwa au kusaidiwa na wengine kujiandikisha au kupiga kura. Inatumika hata kwa wale waliofaulu mtihani wao wa uraia na mahojiano lakini bado hawajaapishwa kama raia wa Marekani