Claude Rwaganje alifikaka Maine kutokea Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwaka wa 1996, karibu miaka ishirini na miwili tangu hapo. Wakati huo, wana Afrika walikuwa wachache wenye kuishi hapa Maine. Kwa hakika, nyuma ya hapo msemo ‘kutoka mbali’ ilitumiwa sana kama namna ya kusema kwamba umetokea sehemu tofauti na nchi ulimo, au kama ume toka nje ya nchi. Haikuwa kwenye rada ya mtu awaye yote kwa wakati ule kwamba Maine karibuni itageuka jimbo ya kukaribisha wakaaji wapya kutoka Afrika.
Bwana Rwaganje alilazimikaka kuondoka nchi yake na kutafuta usalama hapa kujikinga mwenyewe. Akiwa mwanaharakati tangu umri wake mdogo, hakuwa na aibu yoyote ile juu ya kuzungumza mambo yanayo husu haki na dhidi ya unyanyasaji, na hii ilimfanya awe lengo. Aliondoka nyumbani kwao munamo mwaka 1994, wakati wa vurugu wa Vita vikuu vya Ulimwengu vya Kiafrika.
Bado angali anaweza kukumbuka kwa fahamu mambo ya kuchanganisha aliyoyaona na jicho lake kabla ya kukimbia nchi yake – Nyumba zinazowaka moto, mabasi na malori yaliyokuwa yakichukua silaha na waaskari pia wanawake na watoto waliyomiminwa Bukawa, mji ambako alikuwa akihudhuria chuo kikuu, na ambao ulikuwa karibu na mipaka na Rwanda upande wa Congo. Marafiki wa chuo watatu ambao hawakuweza kuondoka, wakidhani kwamba mambo yatarudi shwari, waliaminika kuuwawa wakati wa vurugo ya wakati huo.
Bwana Rwaganje akisema juu yake mwenyewe na juu ya wahamiaji wengine wa Afrika wanaoishi sasa Maine, “Sisi si hapa kwa kutaka, ila kwa sababu ya yaliyotokea nyumbani kwa inchi zetu. Kwa bahati mbaya hatuwezi kuwa nyumbani, kwa sababu ya yaliyo tokea. Ningependa kuwa katika nchi yangu ili kutoa ujuzi wangu na maarifa ninayo kwa lakini siwezi kuwa huko kwa maana ni imekuwa mahali pa hatari sana. ”
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji rasmi wa Jumuhia ya Uandishi kuhusu mambo ya kifedha – wakati huu ukisherehekea kumbukumbu ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mradi huu na ambao umebadilishwa jina na kuitwa sasa ProsperityME – Bwana Rwaganje anakumbuka mawimbi ya awali wakati Wasomali na waSudan walio anza kufika Maine mapema mwaka wa 2000. Ame kumbuka pia wakati ambapo wakimbizi na watafuta hifadhi walianza kufika kwa idadi kubwa kutoka Burundi, Jamuhuri ya kidemocrasi ya Congo, Rwanda, na Angola mapema mwaka 2010, 2011, na 2012. Maisha yalianza kubadilika kwa kwa wahamiaji kutoka wa Afrika baada ya hapo, na pia akatambua kwa furaha kwamba kunako sasa uvumilivu wa kuwepo utofauti wa ma kabila jimboni wakati huu.
“Hatutaki kuwa wageni katika jimbo letu,” amesema. “Ninaipenda Maine, ninawapenda wakaaji wa Maine. Nataka kuijenga jimbo hili pamoja na wengine. Tupo hapa kuchangia katika uchumi wa Maine, jimbo ambalo limekubali kuwahifazi wale miongoni mwetu ambao walifika wakiwa katika hali ya muhitaji. “Rwaganje amesema ya kwamba idadi ya watu wa jimbo hili na umuhimu wa mchango wa wahamiaji wapya ambao wamejaza pengo zilizoachwa pale palipokosa watu kutokana na kuzeeka kwa wafanyakazi. “Tuko hapa kama wanaoleta mchango wetu. Hii ni hali mchezo wa faida kwa faida, amesema.
Kama maandishi ya upande, amenukulu kwamba mwaka huu umeonekana uhaba wa wahamiaji wapya kufika jimbo la Maine kwa sababu ya uamuzi wa Rais Trump kupunguza idadi ya wakimbizi.
Bwana Rwaganje ana mke na watoto, nao watoto wameingizwa kabisa na kuzoea ipasavyo maisha ya hapa. Kwa hakika, wao wameunganishwa sana kiasi wamekuwa na wasiwasi na sasa wanajitahidi kuwalinda watoto mbali na kusahau utamaduni wa Kongo kabisakabisa. Wanasema Kiingereza kikamilifu, na bwana Rwaganje anaongea vizuri sana Kiingereza. Pia anaongea Kifaransa, Kinyamulenge, Kiswahili, Kirundi, na kinyarwanda. Anasema kwamba asili mia 90 ya wahamiaji kutoka Afrika wanawasili katika jimbo hii wakiwa wenye kuchukuwa pamoja nao elimu nzuri. Yeye mwenyewe alipokuja nchini humu alikuwa akichukuwa mfukoni mwake majifunzo ya ki Biologia na ufundi wa duka la madawa. Baada ya kufika hapa, alirudi shuleni na kupata shahada katika Biashara na uongozi kunako Chuo Kikuu cha Kusini mwa Maine na baadaye ka pata shahada linguine juu ya shahada katika mafunzo yale yale.
Licha ya elimu yake hiyo, alipofika nchini humu kila kitu kilionekana kwake kuwa kigeni. Akawa anahamia hapa na pale katika uchumi wa msingi wa fedha. Huko akikata na kurudilia hadithi alizo tumia ili kuonyesha ginsi gani maisha katika nchi mupya yanaweza kuchanganyikisha mutu na zaidi kwa mfumo wa benki. Hadithi hizo zinaelezea pia nini kilichomsababisha kuunda CFL (kwa sasa ProsperityME). Kwenye mkutano na mwajiri mpya wakati ule, mara tu alipofika, la muhimu ni kwamba mwajiri huo aliendelea kumumaanishia ‘fomu 401K’, kwa kuwa hakushinda kuelewa yale yaliyokuwamo. Hatimaye alielezwa kuwa hii inahusiana na ‘kustaafu’ – ila pia ilikuwa dhana yeye hakuzoeana nayo. Akiwa hawezi kuamua mpango gani achague, alifunga tu macho na kuchagua kwa upofu. Licha ya hayo aligundua kuwa kama ikiwa amechanganyikiwa kiasi hicho, wengine bila shaka wanaofika nchini humu watachanganyikiwa vivyo hivyo bila shaka.
Hadithi nyingine ilihusisha habari ya mtu kusainiana pamoja na mtu asiye na kibali ya ya kupata mikopo na ambaye aliomba msaada wake kwa kununua gari. Hakujua ya kwamba kwa kusainiana pamoja naye alikuwa akiwajibika kwa muswada huo. Alikwama kwa mara ya kwanza kwa sababu mnunuzi alitoka jimbo hilo na kwenda mahala pengine bila kulipa, nyuma ya hapo alipata njia halali ya kisheria ili kukabiliana na hali hiyo, lakini alitambua kwamba kuna wengine waliopaswa kuwa na uharibifu wa kifedha kwa sababu hawakuelewa mfumo wa ki fedha wa Marekani.
Kwa mwaka wa 2008 aliamua kuanzisha shirika lisilo la faida lililotarajiwa kuwa elimisha wahamiaji wa kizazi cha hapo mwanzo kuhusu jinsi ya kujenga maisha bora. Alitaka sana kuwasaidia watu kuwekeza kwa siku za usoni, hadi kufikia ndoto yao ya ki-Marekani, na pia kuijenga jumuiya ya wenye kufanikiwa zaidi. Kwa miaka mingi, CFL imewasaidia watu wengi kwa njia tofauti, kama vile kupitia akaunti za Maendeleo ya mtu binafsi (kwa kushirikiana na CEI) ambazo zimesaidia kugaramia ongezo la elimu, kuanzisha biashara ndogo ndogo, manunuzi ya nyumba, na ununuzi wa gari; kupitia kozi ya kujifunza matumizi ya fedha; na warsha za moja kwa moja ofisini kuhusu matumizi ya fedha, hii ni kutaja mifano michache tu. CFL imehudumia hasa wakimbizi, wahamiaji, na walio pewa hifadhi, lakini pia watu kawaida wenye kipato cha chini.
Bwana Rwaganje mara ameeleza kwamba hakulijenga shirika hilo pekee na wala asingeliweza kuitekeleza yeye binafsi. Ila washirika na mjongoni mwao Mamlaka ya Makazi ya Portland, ambao imeipa hili shirika nyumba yake ya kwanza; Avesta Housing, ambayo kwa sasa hugawia nafasi maridadi; Mamlaka ya Makazi ya Jimbo la Maine; Shule la watu wazima la Portland. Na kwa nyongezo, CFL imekuwa na bodi bora la uongozi, ambao wanamemba wake wametekeleza kazi ya maajabu kwa miaka, pia timu lenye nguvu la wafanyakazi. Kwa sasa shirika linalo watumishi watatu wa wakati wote, mtu mmoja mfanya kazi kwa muda, na mshauri zaidi ya Claude. Kunatarajiwa ku ajiri watu wawili wapya munamo siku za usoni.
Mei 8 imekamilisha kumbukumbu ya miaka 10 ya shirika lisilo la faida. Wanachama wa jumuiya hiyo walikusanyika kunako Thompson Point kusherehekea kwa muziki, chakula, vinywaji, tuzo – na kufunguliwa kwa jina jipya, ProsperityME. Zaidi ya miaka shirika limeongezeka sana. Hapo mwanzo lilikuwako tu Portland, na sasa lina eneo la pili Lewiston. ProperityME sasa inaangalia mbali zaidi ya ujuzi wa kifedha na kuendea njia ya starehe ya ya jamii. Kuna mikono mine kwa maono ya shirika: elimu ya kifedha, Kazi na ujuzi wa ki maendeleo, msaada kwa biashara ndogo ndogo na wajasiriamali, pamoja na msaada kwa wale wanaotafuta kupata elimu ya juu.
“Tupo hapa kama wachangiaji,” Claude Rwaganje amesema kuhusu ProsperityME. “Tunatumikisha Wamarekani pamoja na wahamiaji. Tunasaidia watu kuja kuwekeza katika Maine. Tunatumika. ”