“Furaha yangu ni kwamba mazungumzo yameanza kuhusu kuwakaribisha watu wageni kwa Bangor,” amesema Angela Okafor, mwanasheria wa uhamiaji na mmiliki wa Tropical Tastes na Styles International Market. “Kuna kitu kinachoanza hapa.” Akiwa mwanainchi kutokea Nigeria, Bibi Okafor alihamia Bangor na mumewe munamo mwaka wa 2008. Wakati huo alikuwa amekamilisha Majifunzo ya mwanasheria nchini Nigeria. “Katika Nigeria, kujifunza sheria ilikuwa vigumu. Jamii inatarajia mambo fulani kwa wanawake. Lakini mimi si mtu wafuatayo! “Sasa, miaka minane baadaye, ana watoto watatu wadogo, alianzisha kazi ya mwanasheria yake mwenyewe mwezi Agosti 2016, na hivi akajiunga na bodi ya Muchnaganyiko wa Utamaduni mbalimbali wa Maine (Maine Multicultural Center) wakati huo huo.
“Usiseme kuwa nina wazimu,” anakumbuka akiwaambia marafiki zake mwishoni mwa mwaka wa 2016, “lakini ninafikiri pia kuanzisha soko la kiAfrika.” Baada ya kutafakari alirekebisha wazo lake kidogo. “Ilionekana Kuna ubaguzi wa kutosha wa jamii katika hali hii. Nitafanya basi soko la kimataifa! “Alifanya hivyo tu, akiongeza ‘mwenyezi biashara’ kwenye orodha yake ya mafanikio. Soko hilo lilifunguliwa mwezi Januari 2017 na sasa ipo imara katika mji wa Bangor.
Katika saa niliyopitisha katika duka siku ya Jumamosi biashara ya mchana ilikuwa nzuri. Pamoja na kuwa mara kwa mara ununuzi wa bidhaa za chakula, wanandoa wachanga wenye mtoto mdogo aliyekuwa wamehamia hapa Brewer mawiki matatu hapo awali, na ambao walitafuta mahsusi soko la kimataifa, walikagua duka, wakiwa na furaha kujaza kikapu na bidhaa. Mykayla Hoggard, mkaaji kijana mdogo wa Bangor, ameketi kwenye kiti cha mtindo wakati Bibi Okafor, aliyejifunza kuandaa kiafrika ili aweze kutoa huduma ifaayo kwa wateja, aliongeza upanuzi wa nywele za Hoggard
Maisha katika Bangor haijakuwaka rahisi kwa Bibi Okafor, hasa katika miaka ya mwanzoni. kutoka sasa hivi kwenye shule ya kisheria, alikuwa na hamu sana ya kupata kazi kama mwanasheria. Hata hivyo, aliona kuwa haiwezekani kwa mara ya kwanza kupata mguu uingie kwenye mlango katika taaluma ya kisheria mjini Bangor. “Kila kitu kilichonihusu mimi kilikuwa kiulizo,” alisema, na pia ujinga wa wale waliomhoji mara nyingi ulimshangaza. Aliulizwa kama kuna kitu kingine chochote Afrika isipokuwa Sahara; wahojiwa walielezea kwamba waliamini Afrika ilikuwa nchi, badala ya kuwa bara. Waajiri wanaotarajiwa hawakuchukua elimu yake ya nchini Nigeria kwa uzito. “Niliombwa kuendeshewa huko Maine.” Aliambiwa hawezi kukaa kunako mutihani kuingia kongamano lile la wanasheria bila kuchunguza kwa uangalifu wa maudhui ya kila kozi aliyopata katika shule ya sheria juu ya kipindi cha miaka sita. Hatimaye, alichukua mtihani wa New York Bar badala yake, na akapita. Kampuni yake, inaitwa Okafor Law Practice, inategemea sheria ya uhamiaji, ambayo ni sheria ya shirikisho.
“Unaweza kuchagua matatizo ya kukutengeneza au kukuvunja,” amesema akionyesha anafanya kazi kwa nywele za Mykayla. “Kila kitu ni kuhusu tabia.” Kwa wazi mtazamo wa Bibi Okafor ni chanya – unaweza kujisikia nguvu zake katika salamu yake yenye nguvu wakati unatembea kwenye mlango wa Tropical Tastes na Styles International Market. Nishati yake ni ya kuambukiza na hisia katika duka ni furaha. “Ninapenda kukutana na watu na kuwazungumza,” anasema, akisisimua sana, “na hii sio tu biashara kwangu. Ni mahali ambapo ninasaidia watu kukutana, kuunganisha watu kwa kila mmoja. Ili kulinda familia humu jimboni Maine wanawake wanahitaji kuwa na furaha. Wanahitaji upatikanaji wa huduma – huduma za nywele, chakula wanachopenda, nyenzo za Afrika na nguo. “Okafor anaamini kuwa kufanya Bangor mahali pa kukaribisha kwa wageni itafufua uchumi. Anasema mfano wa hivi karibuni wa wanandoa wakizingatia kuhamia kutoka Boston kwenda Bangor kwa kazi. Mke hakutaka kuja, lakini mume akaingia katika duka na akaangalia kote, na hilo liliwafanya kuwa na maono tofauti wote wawili.
Duka ni kimataifa, na bidhaa kutoka Asia yote, Caribbean, Amerika ya Kusini, Afrika. Yeye anajaribu kuwasaidia wateja kupata bidhaa na bidhaa ambazo wana kosa toka nyumbani. Kwa mfano, yeye hutoa aina moja tu ya curry, lakini badala yake kuleta curries kutoka India, Caribbean, na Afrika. Bi Okafor alipotambua kwamba wateja wake hawapati nguo za Kiafrika, alinunua mashine ya kushona na kujifunza kushona papo hapo. Kwa sasa ana mstari wa bidhaa unaojumuisha vitambaa vya rangi vya Afrika vyenye rangi mbalimbali, suruali, sketi, na kofia ya vichwa. Wakati Mykayla alihitaji nywele za ziada kwa hairstyle aliyochagua, Okafor aliamuru kwa ajili yake. Kwa njia ya Tastical Tastes na Styles LLC – Soko la Kimataifa kwenye ukurasa wa Facebook Okafor hupokea mahitaji maalum. “Nipeni kwangu na nijulishe nini unachohitaji,” anasema. “Nitajaribu kupata, na wakati ninapofanya nitakutumia ujumbe kwamba bidhaa hiyo iko.”
Okafor anasema kuwa wateja wake ni pamoja na wenyeji. “Watu katika eneo la Bangor wanao hamu ya kujaribu vitu vipya. Wanataka kujaribu vyakula na ladha nyingi. Na chakula yetu ni kikaboni, “anasema. “Hatutumii kweli kemikali katika Afrika. Kuna kitu kwa kila mtu hapa. ”
Mutandao wa kampuni ya kisheria ya Angela Okafor ni www.okaforlaw.com na soko lake ni kunako 347 Harlow Street, Bangor. Anaona wateja wa kisheria asubuhi na soko lake linafunguliwa baada ya mchana, Jumanne – Jumamosi