By Kathreen Harrison

Pamoja na tarehe ya Agosti 15 mwisho unaopewa kwa wote kuondoka kwa sababu ya kurudilia majukumu ya awali ya Jengo la Expo, na shida ya kutokuwepo makazi ya bei rahisi ambayo imekuwa ikiongezeka kwa miaka kote katika Maine, viongozi wa mtaa wa Portland na viongozi wa jamii kadhaa wame kusanyika katika muungano wa nguvu ili kugundua palipo makazi kwa waomba hifadhi ambao wameanza kuwasili Maine mnamo 9 ya Juni.
Kristina Egan, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza Kuu la kiSerikali la Portland (GPCOG), aliitisha muungano huo. Bi Egan alisema wafanyikazi wake wameweka kando miradi mingine ili kuzingatia hali hii ya juu, ya dharura ya umma.
“Tumefurahishwa kufanya hivyo,” alisema. Kikundi hiki kiko kinazindua “Nyumba za Kukaribisha,” mkono mmoja muhimu wa mpango wa jumla wa makazi ambayo pia ni pamoja na kuhamisha baadhi ya familia takriban 70 kwenye vyumba vya kukodisha katika wiki chache zijazo, na vile vile wakati nyumba za mpito kama ilivyokuwa kale zitakapo acha nafasi ya kufunguliwa mwishoni mwa msimu wa kiangazi. Wenyeji nyumba watalinganisha waomba hifadhi na familia za wenyeji nyumba walioko katika mkoa wa Portland Mkuu, na kutoa nyumba hizo kwa muda mfupi kwa familia chache.
“Tunapanga kuanzisha mpango wetu Julai tarehe 19 na familia moja ya mwenyeji, kama jaribio, ili kupata mazoezi ya kufanya kazi pamoja kama timu kabla ya kuikabilisha kikamilifu kwa wiki ijayo,” alisema Tom Bell, mpashaji habari kwa umma katika GPCOG.
Mpango huo ilitengenezwa na kikundi cha washirika wa jamii ambacho ni pamoja na viongozi wa wahamiaji, mashirika ya imani, wawakilishi kutoka Jiji la Portland, Baraza la Kimataifa juu ya Kubadilishana Kielimu (CIEE), Makazi ya Maine, Makazi ya Avesta, na Carla Hunt, kutoka Mpango wa Makazi ya Huruma huko Yarmouth. Viongozi wa wahamiaji wanaohusika katika ufundi wa ujenzi wa Nyumba za Makao wakiwemo Pious Ali, Deqa Dhalac, Papy Bongibo, Mufalo Chitam, Claude Rwaganje, Micky Bondo, Nsiona Nguizani, Baby Ly, na Claudette Ndayininahaze. Viongozi hawa watakuwa wakitekeleza ulinganisho halisi wa familia za upokezi na wageni
Bwana Bell alisema, “Watu ambao wanaolinganisha familia ni watu wanaofahamika tayari na watafuta hifadhi tayari. Ni viongozi wahamiaji. Watakao na haya mawasiliano itakuwa ni viongozi wa wahamiaji. ”
Kila mtu anayehusika katika Nyumba za mapokezi amejitolea kuhakikisha ustawi wa wapokezi na wageni. Wakati wavuti iliyopangwa itakuwa hai angani wiki ijayo, itakuwemo pia na ombi itakayo jazwa na familia zinazo pokea zikiwa pamoja na orodha ya matarajio ambayo familia za upokezi lazima zikutane nazo – kama kwa wageni kupata nafasi jikoni. Fursa za mafunzo ya kitamaduni zitatolewa kwa familia zote za mwenye kupokea kama vile za wageni wanaotafuta hifadhi. Claudette Ndayininahaze na Mick Bondo, waanzilishi wa shirika in Her Presence “Katika uwepo wake”, pamoja na viongozi wengine wa wahamiaji, watatoa utaalam wao katika mafunzo haya ya kitamaduni
“Ni lazima tuhakikishe kuwa familia zinazotoka na kwenda inje ya Expo zina mashirika fulani mahali ambapo zinaenda, kwamba familia za mapokezi zinajua nini cha kutarajia, na kwamba waombaji hifadhi wanajua jinsi ya kuwa wageni katika nyumba za Amerika”, amesema Bibi. Egan.
Heather Dallas, ambaye aliye tumika sana na wanaotafuta hifadhi zaidi ya 800 huko Portland kwa kiwango cha miaka mitano, alisisitiza kwamba mwelekeo wa kitamaduni utakuwa wa muhimu kwa ajili ya kufanikiwa kwa mpango wa uenyeji wa nyumba. Aligundua kuwa watu wanaishi katika nyumba tofauti, kulingana na asili yao, na mwelekeo wao wa kitamaduni pamoja na mifano halisi inayoweza kusaidia familia kuishi wakati wanapoishi chini ya paa moja.
Bibi Ndayininahaze alikubali kwamba mwelekeo wa kitamaduni ni ufunguo wa mafanikio ya wenyeji nyumba za kupanga. kuwepo kwake, Misaada ya kiKatoliki, na Jiji la Portland tayari zimeanza kuongoza mwelekeo wa mwelekeo. Bi Ndayininahaze alisisitiza kwamba mwelekeo wa vikundi vidogo vidogo hufanya kazi vizuri. Mpango ni “kufuatilia familia wakati zikiwa zinaelekea kwenye jamii ziki endelea kupata usaidizi kitamaduni, kuhusisha shule na vitongoji, ili kujenga uhusiano na uaminifu. Rasilimali ni jambo moja, lakini sehemu ya kijamii ni muhimu sana,” alisema. Bibi Ndayininahaze ameongeza ya kuwa majifunzo ya lugha ya Kiingereza yameanza, na kwamba watu 75 walikuwa wamejiandikisha tayari kwa madarasa ifikapo Julai 19
Baraza Kuu la Serikali la Portland limepokea tayari maombi 115 kutoka kwa watu wanaotaka kuwakaribisha majumbani mwao waombaji wa hifadhi ambao kwa sasa wana hudumiwa katika Jengo la Portland Expo – na hiyo ilikuwa kabla ya tovuti ya wenyeji wa ma nyumbani bado kuzinduliwa. Baadhi ya maombi hayo yametoka kwenye vijiji vilivyomo katika Jimbo. Nsiona Nguizani, Msimamizi wa Chama cha waAngola cha Maine, alisema kuwa changamoto kubwa kwa wale wanaotafuta hifadhi inaweza kuwa “kutengwa, na hofu ya kutokujulikana. Hii ni kwa sehemu sababu ya kuwa jamii ya wahamiaji inajitahidi kufanya kazi ili kuunda mfumo ambao baadaye utafanya kazi katika nchi nzima ili kushughulikia changamoto za kijamii zinazohusiana na kuwa mtu anayeomba hifadhi akiwa vijijini katika jimbo. ”Hii ni sababu nyingine inayofanya kwamba, hadi mfumo huu utakapowekwa, viongozi wa wahamiaji watakuwa wana weka kipaumbele kutia ma nyumbani kwanza familia kutoka Jengo la Expo katika maeneo na mazingira ya Portland kubwa.
Wakati kuwaweka manyumbani jamii za waomba hifathi pamoja na familia katika maeneo ya vijijini hayajakuwapo kwenye mipango wakati huu, miji na miji nje ya Portland wanaweza kutaka kuchukua jukumu katika suluhisho la kudumu. Meneja wa Jiji la Portland Jon Jennings alisema, “Miji na miji katika Maine wataonekana kuwa kama na maono mafupi kwa kutokuona hii kama fursa ya kuimarisha uchumi wa Maine na kukuza nguvu ya wafanyakazi. jamaa hizo ziko hapa kihalali, zina ustadi na mafunzo, na ziko tayari kutoa mchango wao kwa jamii wao wapya. ”
CIEE itaongoza uchunguzi wa kwanza kurudilia maombi yote kutoka kwa wapangishaji ajili ya mpango wa nyumba za kupanga. Huu uchunguzi hakiki wa awali utajumuisha ukaguzi wa chini wa kiwango. CIEE baadaye itatoa habari kwa viongozi wa wahamiaji, ambao watalinganisha familia zinazotafuta hifadhi na wenyeji nyumba waliokamilika.
Mnamo tarehe Julai 18, Gavana Mills alitangaza kwamba ameviboresha vikwazo vilivyo kuwa juu ya ustahiki wa kupata Msaada wa Jumla. Wakati fedha hizo zitawaruhusu watafuta hifadhi wengi kupata vocha kwa nyumba, kununua chakula, na dawa, uhaba wa nyumba bado unabaki, na kwa hivyo ndivyo hitaji ya makazi ya muda yanahitajika.
“Fedha mpya ya (GA) haibadilishi hitaji la kupata makazi ya muda,” alisema Bwana Bell. “Kuna uhaba wa nyumba katika jimbo. Itachukua muda mwingi kwa kupata makazi ya kudumu kwa kila mtu aliye huko kwenye Expo. Nyumba hiyo ya muda itaendelea kuhitajika ili kutoa makazi kwa familia wakati ambapo jiji, Avesta Housing, na wenzi wengine wata pata makazi ya kutosha kwa wanaotafuta hifadhi. “