Gavana wa Nairobi kashutumiwa ulaji rushwa Mfano kwa Bara?

Ijumaa, Desemba 6 Vyombo vya habari vya Kiafrika vimedondoza habari kwamba Mike Sonko, Gavana wa Nairobi, mji mkuu wa Kenya amewekwa kizuizwini kwa tuhuma za rushwa, baada ya kuendesha vema kampeni ya uchaguzi kwa muhula wa pili wa Rais Uhuru Kenyatta mwaka wa 2017 alipoahidi kuongoa mizizi ya ufisadi kunako kila ngazi ya serikali. Gavana Sonko anatuhumiwa kuondoa pesa taslimu bilioni 3.5 za fedha za serikali kwa matumizi yake binafsi. Kukamatwa kwa mwanasiasa wa kiwango cha juu sio kawaida barani Afrika, ambapo ufisadi umejaa kati ya viongozi wa serikali wa ngazi za juu.
Transparency International, shirika linalolenga kufuatilia kwa makini hali ya rushwa, imeipanga Kenya kuwa kwa nafasi ya 144 miongoni mwa nchi 180. BBC imeripoti kwamba tangu uhuru wa Kenya kutoka kwa Uingereza mnamo mwaka wa 1964, Kenya inaweza kuwa imepoteza dola bilioni 66 kwa ufisadi. Mnamo Februari 2019, BBC na vyombo vingine vya habari viliripoti kwamba Kenya ilikuwa imelipa $ milioni 210 kwa mabwawa ya umeme na umwagiliaji ambao hauyajawahi kujengwa. Kesi inayo husiana na kashfa hii ya rushwa bado inaendelea.
Shida ya Kenya na ufisadi katika serikali sio ya kipekee. Utafiti wa Jumuiya ya Afrika wa mwaka wa 2002, uliojulikana na kurejelewa sana, ikiwa ni pamoja na Baraza juu ya Mahusiano na nchi za nje, unakadiria kwamba rushwa inagharimu bara hilo takriban dola bilioni 150 kila mwaka. Rushwa imekuwa ikihusishwa na kudhohofisha maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.
Angola, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, na Jamhuri ya Congo ziko kati ya nchi zenye rushwa zaidi ulimwenguni, kulingana na kielelezo cha mtazamo juu ya Ufisadi, iliyochapishwa na Transparency International. Maine ni nyumbani kwa wahamiaji wengi kutoka nchi hizi. Wasomi hugundua kwamba rushwa na upendeleo ni kama nguvu zinazopelekea uhamiaji kuelekea nchi zisizo na ufisadi. Marekani ina pangwa kuwa nchi ya 22 kati ya 180 kwenye kiwango cha rushwa, nyuma tu ya Ufaransa. Denmark imeorodheshwa kama taifa lenye idadi ndogo sana ya rushwa ulimwenguni.

Waaskari 13 wa Ufaransa wamekufa huko SAHEL
Kanda kubwa inaibuka kuwa kitanda moto
cha ugaidi barani Afrika.

Waaskari kumi na watatu wa Ufaransa walikufa kwenye mgongano wa helikopta tarehe 26 Novemba wakati wakipigana na vikundi vya ugaidi vya Kiislamu vilivyopata bandari salama katika mkoa wa Sahel wa Mali. Zaidi ya askari wa Ufaransa 4,500 wanafanya kazi ya mapambano nchini Mali na nchi zingine za mkoa wa Sahel. Sahel ni eneo ambalo linajulikana kama ukanda ulio kati ya Sahara kuelekea kaskazini na kusini mwa Africa iliyo kusini mwa Sahara. Mali, Burkina Faso, Niger, Chad, na Mauritania wameunda G5 muungano wa Sahel ili kupambana na ugaidi na kutumika pamoja kwa malengo mengine ya ushirika.
Baada ya mapinduzi ya kijeshi iliyo fukuza rais wa Mali Amado Toumani Toure mnamo mwaka wa 2012, Ufalme wa kale wa Mali ulishuka kwenye machafuko. Mkoa huo, unasumbuliwa tayari na ukosefu wa utulivu, umegawanyika tayari kati ya vikundi vingi zaidi kama wanamgambo wenye silaha wakiua na kusababisha mamilioni ya watu kuhama makao yao.
Karibu na Mali ni Burkina Faso, ambayo pia inalinda vikundi vya magaidi, kulingana na duru za BBC. Vikundi hivi ni pamoja na Jamuhuri la Kiisilamu (IS) na tawi la al-Qaeda lijulikanalo kama Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM). Zaidi ya watu 500 wameuawa, na 500,000 wametoshwa kwenye makao yao ndani ya nchi kwa mashambulizi ya wa jihadi tangu mwaka wa 2015.
Jamuhuri la Kiislamu lina endesha shughuli zao nchini Mali, Nigeria, Niger na Burkina Faso. Bandari za Nigeria Boko Haram, kundi cha kigaidi kinachojulikana kuwa kime wauwa watu na kuteka nyara wanafunzi wa kike huko Nigeria, Chad na Cameron. Askari wanne wa Marekani walikufa huko Niger mwaka wa 2017 katika shambulizi la Jamuhuri la Kiislamu.
Mwandishi alisafiri nchini Chad akitumika kandokando ya mpaka kati ya Nigeria na Niger, palipokuweko nyumba nyingi za ukimbizi kwa watu waliohamishwa kwa shughuli za kikundi cha ugaidi. Wakimbizi hao wanaonyesha kutokuwa na matumaini ya wakati gani matisho hayo ya wagaidi yatakapomalizika. Wakimbizi walio wengi katika kambi walipoteza waume, wake, au watoto kabla ya kukimbia makazi yao. Vikundi vya magaidi mara nyingi huingia kwenye miji mikuu kama Nd’jamena ya Chad, ambapo wana tegea mabomu kwenye nafasi za umma zilizojaa watu.