Mpaka wa Canada unafungwa
Katika mabadiliko makubwa ya sera, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alitangaza mnamo Machi kuwa Canada itawaondoa watafutaji wa hifadhi ambao walijaribu kuvuka mpaka kutokea Marekani. Uamuzi huo unasemekana kuwa hatua ya kinga dhidi ya uambukizi wa COVID-19. Mnamo Juni 16, agizo hilo lilipanuliwa kwa mwezi mwingine, hadi angalau Julai 21. Ikiwa watafutaji wa hifadhi wanawasili kwenye mpaka kabla ya Julai 21 na wanawasiliana na Polisi toka Royal Canadian lililowekwa tayari, watakuwa kwenye hatari ya kupeanwa kwa ICE huko Marekani, na kutumwa mara moja kwa vituo vya ulinzi(jela). Na kutoka hapo wanaweza kurudishwa nchini walikotoka.

Tangu Machi idadi ndogo ya watafutaji hifadhi – kimsingi hasa Watoka Haiti – wamefukuzwa kwenye mpaka, ikiwa ni pamoja na walio fika kwa njia panya ya barabara inayojulikana kama Roxham Road kuvukia New York, ambayo iko umbali wa maili tano kutoka kivuko halali kwa mpaka. Hapo awali maafisa walikuwa wameruhusu wanaotafuta hifadhi kuvuka kupitia Barabara ya Roxham, na pia katika bandari rasmi za kuingia, kama vile Niagara Falls na Champlain-St. Bernard de Lacolle.

Katika miaka ya hivi karibuni, raia wengi wa Kiafrika wanaoomba hifadhi huko Canada wametoka Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani, Eritrea, Angola, na Burundi. Maneno vinywani mwao yanaonyesha kuwa watafutaji wa hifadhi hawa walianza kupima uzito wa faida ya kuondoka Maine kwenda Canada mnamo mwaka wa 2017, wakati harakati za utawala wa sasa kupambana na uhamiaji zilionyesha kwamba mfumo wa maombi ya hifadhi wa Marekani ulivunjwa. Baadhi ya waombaji wa hifadhi ambao walifika Maine majira ya joto ya 2019 kutokea mpaka wa kusini waliendelea hadi Canada waki tokea Portland wakati huo.

 

.