Abusana Michael Bondo – anayejulikana kwa walio wengi kama ‘Micky’ – alikimbia nchi yake ya Zaire (iliyoitwa baadaye kwa jina la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) pamoja na mume wake na watoto mnamo mwaka wa 1996 ili kuepuka vita vya kwanza vya Congo. Wakati huo hakujua ya kwamba pamoja na kupoteza nchi yake alikuwa pia akipoteza kazi aliyo kuwa nayo katika utafiti wa kisayansi. Sasa, baada ya miaka ishirini na miwili, amestarehe imara katika Jimbo la Maine kiisha kushinda vikwazo vikubwa, Micky ametangaza kuwa mgombea wa bodi ya shule katika Wilaya ya 1 huko Portland. Hadi sasa amekusanya saini, pia ame shinda kutekeleza tarehe ya mwisho ya kutangaza mgombea, na hivi atakuwa katika kura kwa uchaguzi wa Novemba. Micky anasema kwamba yeye ‘anapenda Maine’ na pia anataka kurudishia kwenye inchi iliyo mu pokea kama mwana wa kupanga. “Nipo hapa kurudisha, na sio tu kuchukua. Elimu ni ufunguo kwa mafanikio ya kiuchumi ya Portland Jimboni mwa Maine, na nina nafasi nzuri ya kusaidia Portland kwa kutumikia kwenye bodi ya shule. ”
Mzaliwa mnamo familia inayozungumuza Kifaransa na Lingala huko Kinshasa, Bibi Bondo alipata elimu nzuri kwa sababu baba yake, ambaye ni mwandishi wa habari na mwanasiasa, muamini sana katika thamani itokanayo na elimu. Alizidi kumtia moyo binti wake kusema haitoshe tu kwenda kwenye chuo kikuu lakini ya maana ni kuhitimu shule. Baada ya kumaliza shahada kuu katika biochemistry, alifanya kazi ya utafiti juu ya ugonjwa wa seli ya sungura. Alikuwa amefanya kazi katika maabara/chumba cha majaribio ya sayansi kwa miaka kumi na tano na kuanzisha familia wakati vita vilipoanza na ambavyo vingebadili maisha yake daima.
Baada ya kukimbia DRC, familia hiyo ilikaa kwanza huko Atlanta, Georgia ambapo mume wa Micky alikuwa na kazi iliyopatana na elimu yake, ambalo ilikuwa ya kilimo. Wakati wa marekebisho ya maisha awali wakiwa huko Atlanta Micky aliyambua kuwa mafunzo na shahada yake ya kisayansi haijawahi kutambuliwa nchini Marekani. Kwa hiyo, alitumia wakati wake kufanya kazi kwa McDonald kwa malipo ya $ 4.75 kwa saa, “… akipiga hamburger bora kuliko ile mtu yeyote anayeweza kufanya!” Palikuwapo na siku Micky alipoteza tumaini, kiasi akijiuliza kama asingeli paswa kurudi Afrika, ambako angeweza kutumia elimu yake. Hata hivyo, baba ya Micky alikuwa amemfundisha mara kwa mara kwamba ‘kuwa na ujuzi, na elimu, bila kujali yanayo tokea unaweza kusimama juu ya hatua ya dunia na kufanya bora’.
Micky aliamua kufikiria kimkakati kuhusu hali yake. Akaangalia kando kando yake kwenye soko la ajira huko Atlanta. Akatambua kazi ambazo zinazolipa mshahara bora zaidi. Ndipo akarudi tena shuleni,akiingia kwenye kiwango cha shahada ya washirika. Alijifunza kwa miaka miwili, mwaka mmoja katika uongozi wa biashara, na mwaka mmoja katika elimu ya maadibisho. Baada ya kupata shahada aliajiriwa na Soko la Wakulima wa Dekalb, ambako alitumika kwa miaka kumi na miwili. Uwezo wake ulitambuliwa haraka na hapo yeye alipandishwa daraka na kuwa na nafasi muhimu ya uongozi.
Uharibifu wa benki uliotukia mwakani 2007 ulipiga sana Kusini, na mara tena hapo Micky na familia lake walilazimika kuchukua hisa na kubadili mwendo bila shaka. Marafiki wa familia ambao waliokuwa wakiishi Maine waliwahimiza kuchunguza Portland, Maine. Waliangalia kwenye ramani, wakamkuta Maine, walijifunza kwamba kuna wakazi wa lugha ya Kifaransa huko Portland, na wakaamua kujaribu. Mara nyingine Bibi Bondo alijikuta kutafuta kazi nzuri ambayo ingeweza kutumia elimu yake. Baada ya kujitolea sana katika shule za Atlanta, alipitia mfumo wa shule kwa niaba ya watoto wake watano kwa miaka, na kujifunza elimu, aliamua kuweka background hiyo kutumia. Alielewa kuwa alikuwa na nafasi ya pekee ya kusaidia Portland kusaidia wanafunzi wake wapya na wazazi katika safari ya shule. Alianza kwa kufanya kazi kama mkalimani na mtafsiri katika mfumo wa shule.
Hivi sasa yeye ni Mzazi Mratibu kiongozi wa mradi wa uhimizaji huko Portland, mpango kutoka Shule la Muskie ya Huduma za Umma kunako USM, unaofadhiliwa na Foundation ya Nellie Mae. Mpango wa uhimizaji wa Portland huanzisha ushirikiano na hujenga mipango iliyopangwa ili kuzuia mapungufu kati ya shule za umma za Portland na familia za wahamiaji wapya na wanafunzi. Kwa mujibu wa mtandao huo, Waongozi mashupavu ni ma balozi walio na uwezo wa kufanya uhusiano kati ya shule na wazazi wengine au wanamemba wa jamii, baadhi yao hawazungumzi Kiingereza au walio na uhaba wa elimu. Bibi Bondo pia ametumika katika Kituo cha shule kiusikacho na Mchanganyiko wa lugha na mchanganyiko wa utamaduni kama Mkalmani na Mtafsiri, huko akiwa katika bodi ya Opportunity Alliance huko akiwa mwenye kuhusishwa na United Way pamoja na Thrive2027, na tena ni mwanzilishi pamoja na Claudette Ndayininahaze wa kikundi kiitwacho IN HER PRESENCE, shirika ongozi la vikundi vya wahamiaji wanawake.
Micky Bondo anatarajia nini angeweza kukamilisha kwenye bodi ya shule. “Ningependa kusaidia kuleta masuala na makundi mbalimbali ya watu kwenye meza ili kuimarisha jitihada za mji kuelekea kuziba pengo kati ya shule na wazazi.” Utaalamu wake ni zaidi ajili ya wazazi wapya, lakini huwa anataka kufanya kazi kwa niaba ya watoto wote pamoja na wazazi. “Kuna bado mengi ya kufanya jimboni Maine. Tunahitaji kuunda ushirikiano wenye nguvu wa watu – kusema mamoja – kutumia ujuzi na utaalamu wote wa wazazi, watendaji, walimu, mashirika yasiyo ya faida, pamoja na wenye kujitolea kwa kuboresha ma shule, ambazo mwishowe zitaimarisha Portland. ”
Malengo muhimu ni pamoja na: kupanua mipango ya awali ya PreK ili kwamba watoto wote wawe wametayarishwa kuingia kwa shule la msingi; kuongeza idadi ya wafanyakazi na waalimu tofauti ili watoto wahamiaji waone watu wengi zaidi walio kama wao wenyewe shuleni; kuendelea kutengeneza mipango ambayo itahimiza zaidi ushirikiano wa wazazi wahamiaji kunako mikutano ya wazazi na waalimu katika mfumo wa shule kwa ujumla. “Baada ya madhabuha zote za ajabu ambazo wazazi wahamiaji wa Portland wamefanya ili kuwaleta watoto wao katika mji huu na kwenye mashule haya, wanahitaji kuja pamoja kwenye meza ili kuhakikisha kwamba watoto wao wanafanikiwa shuleni. Watoto kwa upande wao wanahitaji ushirikishwaji wa wazazi wao katika ma shule, hasa hasa walio katika miaka ya ujana. Shule haiwezi kuitekeleza peke yake. Ni lazima wazazi wawekwe penye meza ya uamuzi.
Micky ana lenga kuwapa changamoto wazazi wahamiaji ambao mara nyingi hawa shiriki katika mambo ya shule. Walio wengi hufanya kazi nyingi tofauti, wakihitaji kutumia wakati usio mchache kwa usafirisaji, hawawezi kuwasiliana kwa sababu ya vikwazo vya lugha,wengi wao bado hawajapona na matatizo waliyoyapata kutokana na mateso waliyoyapitia bado wakiwa nchini, hawawezi kuogelea katika mifumo kama vile jukwa la ufuatiliwaji wa the Infinite Campus au ujuzi wa msingi, walio wengi katika wanao husika na madai ya kuomba hifadhi, wenyewe wangeweza kuwa na elimu nzuri ya msingi, na bado hawajajenga mawazo yanayoweza kuwaelimisha wenyewe wapate kupanga wa kutafuta elimu ya juu ili hatimaye waweze kupata kazi ambayo hulipa zaidi ya mshahara wa chini. “Wazazi ni lazima watumie ujuzi wao na uwezo wao wa kushinda changamoto. Ni kwa kila mtu, “amesema Micky Bondo. “Ikiwa ninachaguliwa, najua siwezi kuwa shujaa wa ajabu,”Hata hivyo, anaamini kwamba uzoefu wake na umaarufu wake vinaweza kufanya mpango mkubwa kusaidia ma shule za Portland kwa kuziba pengo lilioko kati ya ma shule na jumuiya ya wahamiaji. Uchaguzi utafanyika Novemba tarehe 6.