By Kathreen Harrison

  Oumalkaire Said Barkad alizaliwa huko Djibouti, kaelimishwa nchini Ufaransa, na sasa ameajiriwa kuwa mhandisi wa mitambo anayeishi humu Portland. Kichocheo chake kushirikisha hadithi yake ililenga kusahihisha hadithi tawala ambayo inawaonyesha wahamiaji kama wanao chota sana uchumi wa mtaa huu bila kurudisha. Ku chungua vizuri, ukweli mara nyingi ni kinyume kabisa, alifafanua kwa Kiingereza kamilifu kando ya kopo la kawa asubuhi moja kati ya majira ya baridi ya Jumamosi asubuhi kwenye nyumba ya kahawa ya eneo hilo.

  “Nimekuwa nikifanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya miaka mitano sasa, na ninalipa ya kutosha sana kwa kodi. Tayari nimelipa zaidi kuliko nilivyopokea, na sasa kodi yangu inasaidia watu wengine –miongoni mwao wakaaji wa Maine wa eneo hili. “Aliongeza kusema kwamba wageni wengi wanahitaji msaada wa kifedha wanapofika mara ya kwanza – Bibi Barkad ameipewa, kwa muda mfupi tu – na wengi, walio kama yeye, hawategemee musaada huo kwa muda mrefu.
Kulingana na Uchumi Mpya wa Marekani, mnamo mwaka wa 2016 kaya za wahamiaji zilichangia dola milioni 62 katika ushuru wa ndani wa serikali ya Maine, na pia dola bilioni 1.2 kwa (GDP)Uchumi wa Taifa ya eneo la jiji la Greater Portland(Eneo kubwa la Portland). Mara tu wazaliwa wa kigeni wanapo pata ujuzi fulani wa lugha ya Kiingereza na kupata sifa za kitaalam au mafunzo, walio wengi hutafuta kupata kazi haraka, huanza kulipa ushuru, kukodisha au kununua nyumba, kununua magari na gesi, pia kuchangia kwa njia nyingi kuinua uchumi.
Bi Barkad ametumika sana kwa kufika mahali alipo leo, na mwenendo wake katika kufanikiwa kupewa ajira ya kudumu na leseni ya kitaalam ni mafunzo kwa kile kinahitajika kufanyika kwa wahamiaji wapya ili kuji unganisha kwa haraka – ukiwa mchanganyiko wa uungaji mkono kifedha na kitaalam, pamoja na sifa za kibinafsi za uamuzi na uvumilivu. .
Stefanie Trice Gill, mmiliki wa IntWork, kampuni ya kimsingi ya Portland inayo waajiri wahandisi na wataalamu wenye ujuzi wa STEM kufanya kazi humu Maine, alimsaidia Bi Barkad kupata kusimamisha kwa mara ya kwanza – mazoezi ya kazi na ArchSolar, kampuni linalo ujuzi wa kuchapa na kujenga nyumba za kuoteshea mimea zinazo tii sheria ya mazingira na za kudumu kiuchumi. Bi Barkad alichukua mafunzo, badala ya kushikilia kazi ya kulipwa kipato cha juu, ili kujipa wakati wa kujizoelesha na mfumo wa wa Marekani kabla ya kuomba kazi inayolingana na mafunzo yake. “Nilikuwa tayari kuchukua mshahara wa chini kwa sababu nilijua kwamba nitaweza kujithibitisha kwa wakati,” Bi Barkad alisema.
Wakati akijizoelesha kazi na ArchSolar, alishikilia nafasi ya pili, pamoja na kuanzisha kazi ya kuondosha chunvi kwa kampuni la BeltaneSolar. BeltaneSolar ilimuajiri Bi. Barkad kama mwanafunzi, isiyo ya hatari kabisa. Shukrani kwa mpango wa Goodwill’s Make-it-in-America (MIIA), ambao ulilipa sehemu ya mshahara wa Bi. Barkad. MIIA pia ilisaidia Bi Barkad kuunda muandiko wa sifa za kazi yake na alama zake kuchunguzwa. Mnamo Aprili 2020, atapewa leseni kama mhandisi wa kitaalam.
David Jackson, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Jimbo la Leseni kwa Wahandisi wa Taaluma, aliyewasiliwa kwa barua pepe kwa wasifu wake, aliandika, “Tumevutiwa na bidii ya Oumal kwa kufanya kazi ili kuweka rekodi inayohitajika kufikia leseni kama mhandisi wa kitaalam humu Maine. Hii ni mafanikio makuu sana, na kama tafiti za kitaifa zinaonyesha kuwa karibu takriban 12-20% tu ya wahandisi wote, wanamilikiwa leseni kitaluma kulingana na nidhamu. Leseni ina saidia sana kwa wahandisi waliofunzwa na wageni, kwani inaonyesha wazi kwa waajiri maalum kwamba wame fikia kiwango kinachotambuliwa. Oumal amefanya bidii na amekidhi mahitaji yote ya leseni na ana kila sababu ya kujivunia matukio na mafanikio yake.”
Bi Barkad amesisitiza kwamba wahamiaji wapya wanahitaji usaidizi mara wanapo weka miguu yao humu Maine, na kwamba Goodwill ilikuwa rasilimali kubwa kwake. “Inasaidia sana kuweko na mipango ya kusaidia wahamiaji wapya. Mwanzoni nilihitaji msaada wa kazi na mafunzo, na Kiingereza changu kilikuwa kidogo, “amesema Bi Barkad. Wakati programu ya MIIA haikuwapo tena, Goodwill ikatoa mipango mingine kupitia Suluhisho la Wafanyakazi ili kusaidia watu kuanza kitaaluma.
“Kama Mtu anaingia na kutaka kazi nzuri, tutawasaidia. Ni muhimu sana kuunga mkono wakaaji wapya wa Maine wanaotaka kufanya kazi, Zaidi sana sababu biashara za Maine zinahitaji msaada. Kuna kazi nyingi ambazo biashara za kawaida zinahitaji kujaza, kwa hivyo ikiwa tunaweza kusaidia kuongeza ustadi wa mtu yeyote ule … hiyo ni ushindi kwa kila mtu, “alisema Heather Steeves, wa Goodwill Northen New England, aliyefikiwa kwa njia ya barua pepe kuhusu wasifu wake.
Stefanie Trice Gill anamwona Bi Barkad kuwa ni mwanzilishi. “Kilichosemwa juu ya Oumalkaire, siku zilizopita mnamo mwaka wa 2014 nilipokutana naye, mara tu baada ya yeye kufika Marekani, alikuwa hana woga na akitaka sana kujifunza, kuzoea, na hatimaye kuchukua kiwango cha imani na kujiweka tayari kufanya mafunzo yake, licha ya pengo la kitamaduni kati yake binafsi na waajiri wa Maine. Wakati huo, wakaaji wa Mainers waliwaajiri wahamiaji kwa nadra – na haswa sio wahamiaji ambao walivaa hijab. Lakini licha ya vizuizi vyote vilivyo onekana dhahiri, ali onekana kufunguka kupokea waziwazi maoni mapya kuhusu jinsi ya kuungana na wenzake, na aliazimia sana kuvumilia na ndipo akafanikiwa. ”
Bi Barkad anakumbuka kwamba wakati wa miaka yake ya mwanzoni huko Maine alifanya kazi kwa bidii kujumuisha katika jamii ya Marekani, pamoja na kukuza ustadi wake wa lugha. “Nilipokuja, lengo langu lilikuwa kuungana na Wamarekani. Mimi ndiye nilikuja hapa, kwa hivyo mimi ndiye ninastahili kuchukua, “alihoji. Mwanzoni kulikuwa na utani mwingi ambao hakuuelewa, na alihitaji kuuliza wenzake wanafunzi kumufasiria mambo mengi. Alisoma Kiingereza kwa kutazama sinema za Netflix, video za YouTube, na kumbukumbu mbalimbali, na wakati alifanya kazi za kujitolea kwenye Klabu ya Wavulana na Wasichana. “Watoto huongea sana!” Alicheka. Mwanzoni alisikia aibu, mwishowe alijifunza kutambua kwamba ni sawa kuuliza maswali na kufanya makosa kwa kiingereza. “Mwanzoni sikuelewa sinema, lakini nilikuwa nikisikiliza na kurudia, na kusoma maandishi ya kifaransa kwa kujua maana,” alisema.

   “Watu humu Maine hutiana moyo. Huku Marekani, ni sawa kufanya makosa. Kwa mwanzo, sikuongea na mtu yeyote, ila baadaye nikagundua kwamba hakuna haja ya kuhisi aibu au kuogopa. Watu wana urafiki sana. Wanasema ‘Hi’ wakati unapo pishana nao barabarani. Nimeona watu wakisema, ‘Karibu katika nchi yetu’ hapo IHOP! ”
Bi Barkad alifanya kazi kama mhandisi wa usanifu wa mitambo tangu mwaka wa 2016 kwa BaselineES, iliyopo huko Yarmouth, nayo ni “mtoaji kimataifa wa muundo na uhandisi wa kubuni na huduma zinazohusiana na kituo.” Tena, kampuni hiyo ilikuwa na motisha ya kumuhajiri. “Mara tu nilipopata kazi ya wakati wote kwa BaselineES, Programu ya Goodwill TOPS ililipa 50% ya mshahara wangu wiki 12 za mwanz wa kasi yangu,” alisema.
“Wahamiaji wenye ujuzi wanawasili Maine wakati wote,” alisema, na angepaswa kujua – kuwa ana familia kubwa inayoishi hapa. Mara tu kila mtu mzima katika familia alipopata vibarua vya kazi, waliingia kwa kikundi cha wafanyakazi. “Wakati ambao vijana, walio wazaliwa wa Maine wana ondoka, nalo jimbo linazidi kuwa mzee, Maine inahitaji hawa watu wapya.”
Bi Trice Gill anayakubali. “Oumal, kama wataalamu wengi waliopewa mafunzo ya kigeni wanaoishi Maine, wana ujuzi ambao tunahitaji kwa kudumisha uchumi wa Maine. Ninawaalika waajiri ambao wanahisi kutetemeka juu ya kuajiri wenye vipaji vya mafunzo ya kigeni ambao wamehamia Maine kukutana naye. ”
Bi Barkad ana ushauri kwa wahamiaji wapya: “Kwanza lugha. Ni jambo la muhimu zaidi. pia upate uzoefu fulani. Usifikirie sana juu ya mshahara mwanzoni. Ukishapata uzoefu, watu watakutaka. “Kwa ma kampuni, amesema,” Waajiri wahamiaji. Wala hamutasikitishwa kamwe! “Na kwa wenzake wakaaji wa Maine, anasema,” Usiogope kutuuliza maswali juu ya vitu kama vile Uislamu, vifuniko vya kichwa – ni bora kwa sisi sote kuwa wazi. “