Na Jean Damascene Hakuzimana

Mnamo Machi tarehe 5, wananchi wa Maine wenye ukoo wa Tigray wameandamana hadi mbele ya Portland City Hall wakitaka kujulisha mgogoro wa miezi minne sasa tangu watu wao wamerejea nyumbani huko mkoani Tigray, nchini Ethiopia, ambako takriban watu karibu milioni tatu wanasemekana kuwa na shida na kuhitaji msaada wa kibinadamu. Kufuatana na ripoti nyingi, watu wa Tigray wana njaa, wengi wakifa, na wakimbizi wakikimbilia nchi ya Sudan

Karibu ya watu 80 wamefika kwenye maandamano hayo, wamoja wakitokea mbali kama vile mji wa Boston. Daniel Gebremariam, mkazi wa Maine mwenye asili ya mkoa wa Tigray amesema anahisi ni wajibu wake kufanya sauti ya Tigray isikilikane. Amesema kuhofia vita kati ya makundi mbalimbali nchini Ethiopia kusababisha kutoelewana vizuri kati ya waethiopia waishio ughaibuni.’Ninataka kujihisi kama muethiopia, na kutazama wenzangu waethiopia kama ndugu ijapokuwa umbambali wa makabila yetu”, ailsema Gebremariam. Amesema kwamba alikuwa mjinga wa kuwaza kwamba wandugu waethiopia hawangaliweza kupigana vita ya kuvusha dama, kama wenyewe kwa wenyewe, vita inayoendelea kati ya serikali ya muungano na chama cha ukombozi wa Tigray” (TPLF). “

Serikali ya muungano ya Ethiopia na TPLF wamekuwa wakipigana vita tangu Novemba 2020. Shirika la Amnesty International lilitoa habari kuhus mauwaji mkoani Tigray na limeitisha uchunguzi likisema kuna uwezekano wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu .Sarah Jackson, Naibu Mkurugenzi wa Afrika mashariki, Pembe la Afrika na Kanda la Maziwa Makuu kwenye Amnesty International, ametangaza: “Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonyesha kiwango cha chini cha ukali wa uhalifu unaotendwa na pande zote mbili kwenye mzozo wa Tigray, na ameharakisha umoja wa mataifa kutenda sasa hivi.Inapaswa kuanzisha uchunguzi wa kimataifa, usioegamia upande wowote, kwa kufuatilia na kuripoti juu ya hali jinsi ilivyo na kukusanya pamoja na kulinda ushahidi wa uhalifu unaofanywa na pande zote. Hakuna wakati wakupoteza- kazi inapaswa kuanza sasa hivi, kabla ushahidi haujaharibiwa na kumbukumbu hazijaanza kufifia”

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema kwamba hali jinsi ilivyo ni utakaso wa kikabila kwenye kamati ya mambo ya nje na waziri wa nje wa Ethiopia amejibu kupitia Twitter akiita mashtaki ya Blinken kuwa “hayana msingi wowote na ni uwongo dhidi ya serikali ya Ethiopia” Hata hivyo, mashtaki ya mauwaji dhidi ya vikosi vya serikali ya Ethiopia, kwa ujumla, ni yale yale mashtaki dhidi ya Tigray People’s Liberation Front, vikosi vya Eritrea, na Amhara Regional Forces pamoja na wanamgambo wenye kuwaegamia.Maelfu ya watu wameuliwa na ma mia ya maelfu wameshurtishwa kukimbia wakiacha makwao kipindi cha miezi minne iliopita. Ripoti kuhusu ubakaji na ukatili wa kijinsia zimesambazwa

“Dada yangu mwenye umri wa miaka 15 yuko peke yake na mwenye kuzingirwa hukoTigray, na mama pamoja nami tunahofia kuhusu hali yake” amesema Gebremariam, akisema pia kwamba mtandao umekatwa, na simu hupatikana masaha machache pekee. Aliongeza kuwa walipojaribu kumpata dada yake kwa simu, amewaelezea kwamba hali ilivyo huko ni ya kutisha na kutoaminika hapo watu wote wakisababishwa kufunguwa wazi milango ya nyumba zao usiku na mchana ili vikosi- vikiwemo pia vikosi vya Eritrea- viingie kuchunguza nyumbani saa yoyote.

Gebremariam amesema kwamba nyumba ya familia yake iko karibu na mpaka wa Eritrea, karibu na Mekele, mji mkuu wa Tigray. Ameeleza kwamba hali ni yenye kupinduka saa yoyote pamoja na vikosi vya serikali, vya Eritrea, wanamgambo wa Amhara wakiwinda siku baada ya siku kila yeyote aitwae mwenye ukoo wa Tigray.

. Si kila mtu mwenye kuamini kuwa mzozo wa Tigray ni mzito, Chemere Zewdie, mwenye kuishi Addis Ababa amesema: “hali mkoani Tigray si mbaya kama inavyosemekana huko ughaibuni. Hata jana, nilipoongea kwa simu na rafiki yangu jijini Mekele, nimeelezwa kwamba yanayotangazwa nje ni totauti na jinsi hali ilivyo huko. “Anadhani kwamba kuna propaganda kubwa kuhusu mgogoro huu

Imetangazwa sana kuwa vikosi vya Eritrea vimevuka mpaka kwa kuvisaidia vikosi vya Ethiopia kuponda Tigray. Gebremariam amesema kuwa Eritrea ilikuwa ikichunga muda mrefu kulipiza kisasi dhidi ya Tigray baada ya miongo ya uhasama na mzozo wa ardhi kati ya Eritrea na Tigray ikiongoza Ethiopia. Tigray na Eritrea zamani walikuwa washirika waliopigana pamoja kumuondoa madarakani dikteta Mengistu Haile Mariam. Walipofauli mnamo mwaka wa 1991, Eritrea ilikimbilia haraka kujitenga na kuunda inchi yao wenyewe, wakati huo watu wa Tigray pamoja na makunndi mengine ya kikabila wakiunda serikali ya muungano ya Ethiopia.

Mbele ya mzozo huu na mvutano uliotangulia, Gebremariam alieleza kwamba alikuwa amefurahishwa sana kuona Waziri Mkuu Abiy Ahmed alikuwa kwenye njia ya kuboresha uhusiano na Eritrea.”Ulikuwa mpango mzuri kufungua mipaka kati ya nchi kwa rejesha biashara kati ya wandugu” Hata hivyo, waki dada yake mdogo alimwambia kwamba vikosi vya Eritrea vilikuwa mkoani Tigray vikiuwa, vikipora na kubaka, tathmini yake imegeuka.

Serikali ya watu kutoka Tigray imeongoza Ethiopia kwa miongo miongo, mpaka kifo cha Waziri Mkuu Melez Zenawi mnamo 2012- na hiyo ijapoluwa watigray ni kabila ya wachache takriban 6% pekee ya wakaazi wa Ethiopia. Baada ya kifo cha Meles Zenawi,wasomi wa Tigray walianza kupoteza mkono wao juu ya madaraka, lakini wameendelea kudhibiti nafasi muhimu kwenye serikali na jeshi. Malalamiko dhidi ya haki za binadamu, mauwaji ya vikosi vya serikali dhidi ya wandamanaji, hayo yote yamemfungulia njia Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutoka kwa kabila la Oromo kufikia utawala mnamo 2018.Baada ya siku chache, Abiy Ahmed kaanza ugomvi na viongozi wa Tigray waliompiganisha na kukataa kujiunga naye katika serikali ya muungano aliyokuwa akiunda.

Gebremariam amemuita Waziri Mkuu Abiy kusikiliza wakaazi wa Ethiopia wote, na kukomesha mgogoro. Amelaumu serikali ya muungano, ambao inasimama kama baba wa taifa lakini mwenye kuwakatili kwa wamoja kati ya watoto wake, badala ya kuwaleta wote kwenye meza moja, na kuwasikiliza wote kwa nia ya kutafuta suluhisho ya haki kwa kumaliza mapambano. Suluhisho haipaswi kuwa chini-juu, na njia ingine pande’, amehitimisha.