Hali ilikuwa ya sherehe na nauli ya ladhaa sana ilipofunguliwa Isuken shirikisho la mlimo la wasomali bantu kwenye meza ya lori la chackula hapo Lewiston ilipokuwa tarehe 29 septemba. Pamoja na chakula kingi na vinywaji tele, sherehe hilo lililenga kukatwa ribbon, shukurani na maombezi yaliyo ongozwa na Imam Haji Mayow Haji
Hii ni ya kwanza ya aina hii katika taifa, chakula kilichogawanywa kutokea kwenye lori imetengenezwa kwa wiungo vilivyokuzwa kwenye mashamba tatu ya shirikisho ya waSomali bantu – Shirikisho la walimaji Isuken, shirikisho la New Roots/mizizi mipya na shamba Liberation. Ulimaji, mapishi, matumizi, uendeshaji gari, na shuguli za ki-biashara zimefanywa na wenyeji sita wa Isuken,
Isnino Ibrahim, Ghali Farrah, Isaack Gawo, Sarura Deqow, Habiba Hussein, na Malyun Negeye.
Kwenye orodha ya viakula kulikuwako sambusas – chapati tamu ya Afrika ya Mashariki iliyotengenezwa kwa mchuzi tamu iliyokaangwa, supu, kitoweo, saladi, injera – chakula cha kiasili iliyo tengenezwa na unga wa mkate, na Chai ya Kisomali. Kunako aina nne za sambusa – ya samaki, ya kuku, ya nyama ya ngombe, na ya vi mboga mboga au vegan.
‘Isuken’ maana yake ‘umoja’ na ‘ sote pamoja’ katika lugha ya kiSomali bantu, na ni tumaini ya wenyeji wa shirikisho kwamba pamoja na kuwa kampuni ya mafanikio ya biashara, Isuken inalenga kusaidia kuleta pamoja tamaduni na jamii hapa Maine. Mohamed Dekow, kutoka Shirika la maendeleo, ambayo imesaidia kuundwa na maendeleo ya wafanya biashara binafsi, amebainisha kwamba maslahi ya chakula ni ya watu wote ulimwenguni. “Watu wamekuwa wakiuliza aina mbalimbali ya maswali kuhusu chakula – namna gani kukanda unga, namna gani kutengeneza sambusa – na kila aina ya mazungumzo yanayo lenga kujenga uhusiano, na hatimaye kuaminiana.” Lori la chakula ni wazo la mwanzoni la wanamemba wa shirikisho Isuken, ambao walikuwa wakifikiri kwamba kupika chakula na kuuza vyakula kungeleta kuongezeka kwa thamani ya mlimo wao. Mwanzoni, wali fikiria kuanzisha mgahawa wa chakula. Baada yaku waza zaidi, wakaamua kuwa na lori la chakula.Ndiposa wakaizindua kampeni iliyofanikiwa kukusanya dola elfu 14 kutokana na ununuzi na upakiaji wa lori. Kwa sasa, lori la chakula la Isuken iko tayari kukuwa kama kwenye masoko na mikusanyiko ya wakulima. Lori hilo tayari limetembelea soko la wakulima la Yarmouth na maonyesho sanaa ya Lewiston na kwa sasa iko tayari kukodeshwa kwenye maonyesho maalum, ikiwemo na ajira ya upishi. Maagizo yanaweza fanyika kupitia [email protected]
New Roots (mizizi mipya kwa kiswahili), shirikisho la kwanza la wahamiaji wenye shamba la kipekee nchini Maine, huendesha kazi zao kwa ma saa kawaida mahali lori litakuwa limeegemeshwa iwapo halip barabani kunako 966 Sabattus Street huko Lewiston. Hema la onyesheo litajumulishwa pamoja na lori la chakula wakiuza mbogamboga nzuri kama vile boga, caroti, maharagwe, pilipili, kabichi, na nyanya ya kupeleka nyumbani baada ya kufurahia chakula kitamu kwenye hema la chakula.
Shirikisho la wakulima wa somali bantu lina bidhaa ya mpango wa jumuiya ya wakulima kunako chama cha jumuiya ya wa somali bantu cha Maine. Kupitia mradi huo, walimaji hupewa mafunzo na kuwa na nafasi ya kulima. Somali bantu wana historia kubwa ya ulimaji na kwa vizazi wana ujuzi wa juu ambao wanaleta kwa kazi zao nchini Maine.Kabla ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeiharibu nchi yao, na kuwapeleka kuhama nchi yao, wa somali bantu, ambao ni kabila ndogo lililo onewa, walio kuwa wakiishi kwa ulimaji wa udongo. Ijapo kuwa hali ni tofauti hapa Maine, ujuzi wa ukulima waliofunzwa Somalia umeonekana kuhamishwa na kuja hapa Maine.
Walioshiriki kikao hicho cha ufunguzi walifurahia ladhaa ya chakula kitamu kilicho andaliwa na Isuken. Yona Ferting Burd, mtaalamu wa shirika la maendeleo pamoja na taasisi ya maendeleo ambao husaidia wakulima, wavuvi na watumiaji kuendesha biashara ya chakula – wlijiunga wengine walio towa neno kwa mkutano kunako sherehe hiyo ya ufungulifu. “Nafurahia sana kuona chakula cha wasomali – mapishi ya wasomali – imegawanywa kwa watu kwenye sherehe na matukio. Tunaweza unganisha tamaduni kupitia chakula” mmoja wa wenyeji shirika____alikubali. “Hakika ninafurahi sana” alisema kwa kingereza kamilifu.
Ukarasa wa facebook wa Isuken : isukencoop; barua pepe : [email protected]; mtandao : www.isukencoop.com