“Kuongezeka ni hapa. Chukua hatua sasa. Kwa ajili yako, na kwa ajili ya familia yako na jamii, vaa barakoa na kaa kando. Jambo hili ni zito. ” – Tweet kutoka Dkt  Nirav Shah, Mkurugenzi wa CDC Maine mnamo 10/30

Kesi mpya za maambukizi ya COVID-19 mia tatu na sitini na tisa zimeripotiwa Maine tangu Oktoba 25, na data za asubuhi ya Oktoba 30 zinatoa mwangaza mkali zaidi wa mripuko wa siku moja katika maambukizo mapya tangu janga hili lilipoanza. Chumba cha kudhibiti magonjwa cha Maine (CDC) kimeonya kuwa kaunti zote za Maine zinakabiliwa na maambukizi ya hali ya wastani hadi kwa jamii, na kwamba virusi hivi vina uwezo wa kuongezeka nje ya udhibiti wake. Idara ya Elimu iliripoti kuweko visa 128 katika mashule za Maine kwa Oktoba 29. Kuna ripoti zinazoonyesha kuugua katika vikundi vyote vya umri, wakiwemo watu wenye umri mdogo kama wa miezi nane. Kesi asilimia hamsini na tisa zilizo Maine ziko kwa watu walio na umri chini ya miaka 60.

 

Watu weusi ao wamarekani wenye asili ya kiAfrika wanahesabiwa kuwa 17% ya kesi zote za jimbo, ila wao ni 1.6% tu ya idadi ya wakaaji wa jimbo. Sababu zilizotajwa mara kwa mara za tofauti kubwa kati yao zimo ubaguzi wa rangi pamoja na sera za kibaguzi ya rangi ambazo huchangia kuwazuia watu weusi na wa marekani wenye asili ya kiAfrika kutoka hali ya umaskini na kufikia maisha ya watu wa kati. Kupitia uhitaji wa kiuchumi, wakati wa janga hili, Wakaaji wa Maine Weusi au Wamarekani wenye asili ya kiAfrika wengi wao wakiwa ni wahamiaji – wamekuwa wakifanya kazi za kuwaweka kwenye mustari wa mbele, na kazi za kibinafsi ambazo wengine hawawezi hata kuzifanya; wakitumia njia za usafiri wa umma ili kufika kazini; wakiishi katika makazi yenye watu wengi, ambayo huinafanya mtengano wa kijamii kuwa mgumu sana, au kutowezekana. Humo Maine, watu weupe wapo 94.4% ya idadi ya watu, na wanakufa kwa kiwango cha vifo 10 juu ya kila hesabu ya watu 100,000. Watu weusi au Wamarekani wenye asili ya kiAfrika wanahesabiwa vifo 22 kwa kila hesabu ya watu 100,000. Kitaifa, Watu weusi wanakufa kwa kiwango cha mara 2.3 zaidi ya kiwango cha watu weupe.

 

Katika mabadilishano ya Oktoba 28 Wataalam walibashiri kwamba kuongezeka kwa uambukizi wa COVID-19 kunaweza kwa swhwmu kuwa kumesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguka kwa joto iliyo endesha watu kukaa zaidi ndani ya nyumba. Waliwahimiza Watu wa Maine kubaki macho wazi, na wasikubaliane na “uchovu wa COVID” Wanawaonya dhidi ya kuamini uvumi wa habari za uwongo ambazo hazitegemei sayansi. Mabarakoa mtengano wa kijamii, pamoja na kunawa mikono bado ni hatua muhimu sana Watu wa Maine wanaweza kuchukua kwa kujilinda wenyewe, familia zao, na jamii, walisema. Virusi hivyo vinaendelea kuwa vya hatari sana, na ma barakoa husaidia kuzuia kuenea kwa coronavirus. Chumba cha kudhibiti magomjwa (CDC) cha Maine kimewaomba watu wa Maine kujibu simu ikiwa wataona pokea simu kutoka kwa wafanyikazi wafuatiliaji wa CDC Maine. Ufuatiliaji kwa njia ya mawasiliano ya simu unabaki wa muhimu kwa kudhibiti kusambaazwa kwa virusi.

Gavana Mills na Daktari Nirav Shah, mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Maine, wameonya wote kwamba watu wa Maine wanahitaji kuepuka – au angalau kupunguza – mikusanyiko ya ndani na watu wa nje ya nyumbani mwao. Wameonyesha wasiwasi wao ya kwamba watu wanatia chini hatua za ulinzi wao, na wanakusanyika ndani. Viongozi wamoja wa jamii wameripoti kuwa hatua ya kiserikali kuingia katika Awamu ya 4 ya mpango wa kuingilia mara tena mpangilio umewachanganya watu kadhaa. Wanawahimiza wanajamii wao kuchunguza kwa makini nambari, na kutambua kwamba kesi za COVID-19 zinaongezeka haraka.

Daktari Shah alisema, “Watu wanaoingia ndani huonekana kuwa kama wameweka ulinzi wao chini.”

“COVID-19 ni adui mkimya anayesitawi na kidokezo kidogo cha kutoridhika,” alisema Gavana Mills.

Chumba cha kudhibiti magonjwa cha Marekani CDC kimesasisha mwongozo wake kuhusu mawasiliano ya karibu. Mtu ambaye amekuwa umbali wa futi sita au chini kwa dakika 15 za kufuatana au zaidi kwa kipindi cha masaa 24 sasa inachukuliwa kuwa mawasiliano ya karibu na mtu aliyegunduliwa kuwa na COVID-19. Daktari Shah anawahimiza watu kuzingatia athari endelevu za mwingiliano mara kwa mara wa mda mfupi, na vile vile wa muda mrefu. Hata wakati amevaa barakoa, mtu bado anafikiriwa kuwa mtu wa karibu baada ya jumla ya dakika 15 alizokaa na mtu aliyeambukizwa.

Hadi sasa, janga la COVID-19 limeua zaidi ya watu 229,000 nchini Marekani pekee, na watu milioni 1.18 ulimwenguni. Huko Maine, watu 146 wamekufa kutokana na COVID-19. Wataalam wamoja wanatabiri kuwa idadi ya sasa ya vifo 225,000 Marekani itaongezeka mara mbili kati ya sasa na Januari, ikiwa itifaki za tahadhari zinazotegemea sayansi zinaendelea kupuuzwa.
Gavana Mills alionyesha wasiwasi wake mkubwa mnamo tarehe Oktoba 28 juu ya mwenendo wa ongezeko za kesi humo Maine. “Swali ni – je, tunaweza kuidhibiti? Haya, Jibu linategemea na kila mmoja wetu. ”