Rais Museveni wa Uganda na Rais Kagame wa Rwanda wamekuwa na uhusiano wa upendo na chuki tangu walipokutana mara ya kwanza katika miaka ya 1980. Walipigana pamoja ili kukomesha mauaji ya kimbari nchini Rwanda, na vinyume vyao katika DR Congo mu miaka ya 1990. Hivi karibuni, mvutano kati ya viongozi hao umeongezeka, kutokana na kuwa kila nchi inamshtaki mwengine kwa mwenendo na tabia mbaya. Vyanzo vyetu vinaonyesha wasiwasi wao kutokana na huo mgogoro kati ya Rwanda na Uganda amabao inayochukua nafasi. Wanaonyesha kwamba mgogoro kama huo unaweza kuripuka na kusababisha maafa makubwa ya kijamii, kiuchumi, na kibinadamu katika Mkoa wote wa Maziwa Makuu ya Afrika, ambapo nchi zote mbili zimeinua uchumi wa kukua kwa kasi, na ambapo wote wanakuwa na majukumu muhimu ya kuimarisha.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Daktari Sezibera, ameshutumu Uganda kwa kulenga mamia ya wananchi wa Rwanda, na kuwafukuza nje ya nchi, na hapa karibuni amewahimiza Wanyarwanda ku acha kusafiri kwenda Uganda. Wanyarwanda sasa wanaogopa kwenda Uganda, na hata kuvuka kwa kupitia nchi hii njiani mwao kwenda Kenya au nchi nyingine katika kanda hilo. Kwa hiyo, watu wanapaswa sasa kutumia safari za ndege ili kuepuka Uganda, au labda kusafiri kwa ardhi kupitia Tanzania, ambayo inafanya safari kuwa ndefu zaidi. Rwanda imefunga mipaka yake kupitia Uganda bila kujulisha sababu tangu mwishoni mwa mwezi wa pili, wanadai kuwa kuwa wanafanya kazi kwenye miundombinu, na malori kutoka Uganda yalipigwa marafuku. Barabara hazitarajiwi kufunguka hadi ifikapo mwezi wa Mei. Vyanzo vyetu hapa Maine walio na familia na marafiki nchini Uganda na Rwanda wana matumaini kuona kupunguzwa kwa haraka kwa mvutano huu, hata hivyo hakuna mikutano iliyopangwa bado kati ya viongozi hawa wawili