Wakazi wa Maine wenye asili ya Sudan wameeleza hofu kubwa kuhusu hali ya sasa nchini Sudan. Zaidi ya mwezi uliopita maelfu ya watu wameandamana kyenye barabara ili kupinga utawala wa Rais Omar Hassan Ahmad al-Bashir. Wanamwomba kujiuzulu, wakisema kuwa wamechoka na utawala wake. Wa Sudan wanaoishi nchini Marekani wako wanazungusha ombi la pendekezo linaloita serikali ya Marekani na jumuiya ya kimataifa kushinikiza Rais Bashir ajiuzulu.
Ombi la pendekezo hilo linasema kwamba Rais Bashir amekuwa madarakani kwa muda mrefu – zaidi ya miaka 30 – na kwamba serikali yake imekuwa mbaya kwa nchi, kisiasa, kijamii na kiuchumi, na kwa ajili ya hiyo lazima ajiuzulu. Wale wanaoripoti kutokea Sudan wanasema kwamba jibu la Rais Bashir zidi ya uasi huo umekuwa huna huruma na wa ukatili,pamoja na mapigano yanayosababisha vifo, kufungwa, na utesaji mkuu. Moja ya vyanzo vyetu huko Maine umeripoti kifo cha jamaa wake mmoja wakati wa mgogoro huo. Wote wanahuzunika sana kuhusu hali ilivyo sasa nchini Sudan na wanatumaini kwamba utawala wa mamlaka wa Rais Bashir utaisha hivi karibuni, ukitumaini kufuatiwa na mfumo mpya, wa kidemokrasia kwa ajili ya Sudan.