Jumamosi, Februari 16, 2019, ni siku ya uchaguzi nchini Nigeria, uwanjani wamehorozeshwa wagombea 69. Wagombea tawala, hata hivyo, ni wenye umri wa miaka 77, Rais Buhari, na Atiku Abubakar, mwenye umri wa miaka 73 ni tajiri mwenye bilioni nyingi. Rais Buhari ni mgombea wa All Progress Congress (APC) na meja jemadari mkuu mstaafu ambaye alishinda uchaguzi mwakani 2015 na sasa anagombea uchaguzi mwengine. Abubakar ni mgombea wa People’s Democratic Party (PDP). Aliwahi kuwa makamu wa rais wakati wa urais wa Olusengun Obasanjo, tangu 1999 hadi 2007.

Wazaliwa wa Maine wenye ukoo wa Nigeria waliozungumza na Amjambo Africa! walisema kuwa miongoni mwa wagombea hawa wawili kwa hii hatua ya msingi, wanaunga mkono Rais Buhari. Wamesema kwamba Buhari ametumika kwa bidii kubwa ajili ya kudhoofisha harakati za kikundi cha ugaidi cha Boko Haram, kupambana na rushwa, na kuboresha miundombinu ya taifa. Wanasema kwamba udhaifu wake mkubwa umekuwa kwa kushughulikia changamoto za kiuchumi. Wanahofu pia juu ya afya ya Rais Buhari – kwa miaka kadhaa iliyopita, amekuwa akipiganisha hali ya afya yake, na wanaogopa kwamba kama hali yake ikiendeleakuharibika itakuwa tatizo kubwa kwa taifa.

Vyanzo vyetu vimeonyesha kuwa na wasiwasi mkubwa ajili ya mgombea Atiku. Wakati wa umakamu wake wa urais, alishutumiwa kwa kuchukua ma milioni ya dola na kuyahamishia kwenye hazina ya mke wake wa nne, Jennifer Douglas, ambaye kwa sasa ni raia wa Marekani anayeishi Marekani. Imesemwa kuwa alikuwa amezuiliwa kuingia Marekani tangu 2005 hadi mwaka huu, wakati alipopigwa picha alipokuwa kwenyi Hoteli ya Trump International huko Washington, DC, tarehe 17 Januari na ambapo alikuwa amepangwa kukutana na mwenyekiti wa Baraza la Bunge aliye musimamizi wa kamati ndogo ya Mambo ya Nje ya Afrika. Watu wa Nigeria wanaogopa kwamba kama Bilionaire Atiku atashinda uchaguzi, anaweza kurudisha tena Nigeria katika kipindi kipya cha rushwa – jambo ambalo nchi imekuwa  ikipiganisha kwa miaka mingi.

Jumamosi, Februari 9, moto uliojitokeza kwenye ofisi ya tume la kitaifa ihusikayo na uchaguzi pa Qua An Pan uliharibu masanduku iliyomo kura, pamoja na vifaa vingine vinavyohusiana na uchaguzi ujao. Watazamaji walidhani na kujisemesha kwamba moto huo unaweza kuwa umewekwa ajili ya kudhoofisha sera za uchaguzi. Hata hivyo, umma umehakikishiwa kuwa uchaguzi utaendelea kwa wakati, na kwamba vifaa vyote wilivyoharibiwa vitabadilishwa kwa wakati ulio faa. Uchaguzi wa Nigeria umeharibiwa na vurugu vurugu kwa miaka mingi. Kulingana na International Crisis Group, watu 108 waliuawa katika vurugu zilizo husiana na uchaguzi wa mwaka wa 2015, na watu 800 waliuawa mwaka wa 2011. WanaNigeria wana matumaini ya kuona hapa karibuni uhamisho wa madaraka kwa amani wakati huu.

Tume la Uchaguzi la Taifa liliahirisha uchaguzi kwa wiki moja tu saa tano tu kabla ya uchaguzi uliopangwa kufunguliwa. Wengi wa waNigeria walikuwa tayari wamesafiri hatua ndefu kufikia ma nyumbani kwao, ili wawe hapo ifikapo siku ya uchaguzi. Wengi wao labda hawataweza kurudilia safari kama hiyo ili kuja kupiga kura. Sababu iliyotajwa kwa kuahirishwa ilikuwa ya kivifaa. Wiki za hivi karibuni zimeharibiwa na kuungzwa kwa vifaa vya kupigia kura, hali mbaya ya hewa, na vurugu vurugu za mauwaji. Mgombea Raisi Buhari amesema kwamba amefadhaika kuona kwamba uchaguzi umeahirishwa, na Atiku Abubakar ameshutumu kuahirishwa huko. Wagombea wote wanaita watu kwa hali ya utulivu. Endelea kushikamana na Amjambo Africa kwenye ukurasa wa Facebook  ajili ya matokeo mapya zaidi.