“Hakuna matunda ambayo huanguka isipokuwa imeivya, lakini mbele ya tufani ya historia, kuivya wala kusipo ivya, huanguka.”
“Tunda halianguki chini hadi limefikia kuivya kabisa, ila ikisukumwa na tufani na dhoruba ya historia, iwe imeivya wala sivyo, itaanguka tu.”
Alhamisi, Aprili 11 ili kanusha mwisho wa utawala wa udikteta wa muda mrefu na wa kikatili huko Afrika wakati Rais Omar Hassan Ahmad al-Bashir wa Sudani ya Kaskazini alipofuturushwa baada ya miaka 30 kwenye madaraka kwa nguvu. Bashir alitekeleza mamlaka katika mapinduzi mwakani 1989 na utawala wake ulikuwa unajulikana kwa ukatili wake. Mahakama ya kimataifa ya jinai imetoa vibali viwili vya kukamatwa kwa al-Bashir, ikimshtaki uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu, na mauaji ya kimbari huko Darfur. Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, inasemeka kwamba watu elfu mia tatu (300,000) wamesemeka wamekufa mjini Darfur.
Rais Bashir alishambuliwa na wasomi wa kijeshi, ambao walitiwa moyo na kushinikizwa na raia. Maandamano yalianza Desemba tarehe 19, 2018 wakati utawala wa al-Bashir ulipandisha beyi mara tatu kwa mkate, wakiwa wame fanywa maskini na kusumbuliwa kiasi kikubwa. Ongezeko hilo la bei limewasha moto harakati ambazo zimeleta mamia ya maelfu ya maandamano mitaani kwa kipindi cha miezi minne. BBC inakadiria kuwa asilimia 70 ya waandamanaji walikuwa ni wanawake. Mnamo Aprili 11 wasomi walimkamata al-Bashir na kumtia kizuizini. Jemadari Ahmed Awad Ibn Auf, aliye kuwa waziri wa zamani wa ulinzi wa Sudan, alitangaza habari ya kuangushwa kwa Bashir juu ya vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali. Kuondolewa kwake kumetuma mshtuko ulimwenguni kote. Habari hiyo ilipokelewa kwa furaha na msamaha na watu wa Sudan, ambao hatimaye walifadhaika kusikia kwamba mwishowe al-Bashir ameondolewa.
Bwana Mustasim, katibu wa jumuiya ya waSudan humu Maine, aliiambia Amjambo Afrika kwamba Aprili 11 ilikuwa mojawapo ya siku bora zaidi maishani mwake. Alifurahishwa na habari ya kwamba Rais wa zamani Bashir, aliye julikana kuwa nyuma ya mauaji ya watu wake wengi huko Darfur, mwishowe ali futwa madarakani kwa nguvu. Anafuatilia kwa karibu habari kutoka Sudan. Ijumaa, Aprili 12, alikuwa amefadhahishwa na maendeleo mapya ya mambo, iliyo kuwa imesema kuwa Jemadari Ahmed Awad Ibn Auf, waziri wa zamani wa ulinzi, ameelekea kuchukua nafasi ya Bashir. Watu wanaona Jemadari Ahmed Awad Ibn Auf kama mufuasi hakika wa Bashir, na kwa haraka wakaanza kuita kwamba aondolewe. Siku ya Jumamosi, Aprili 13, Jemadari Abdul Fatah Burhan alichaguliwa kuongoza serikali ya mpito, na aliagizwa kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia, ambao ina nia ya kurudisha madaraka kwa raia, na kurudisha serikali ya kidemokrasia.
Mheshimiwa Mustasim, ambaye amefunzwa kuwa mwanasheria huko Sudan, na anayekuwa pia na shahada ya Masters katika sayansi ya kisiasa pia, alionya kwamba watu wa Sudan wange pashwa kuwa makini sana nchi isije ika anguka katika machafuko ya kijamii na kisiasa. Alibainisha kwamba nchi kadhaa za Afrika ambazo zimewafukuza wa dikteta wa muda mrefu zimesumbuliwa sana wakati walipokuwa wakijaribu kujenga mfumo mpya wa kisiasa. Anasema kwamba hali nchini Sudan inaweza kugeuka kwa haraka kuwa ya machafuko ikiwa watu hawafanyi kazi pamoja. Kuna familia zaidi ya 200 kutoka Sudan hapa Maine. Wote pamoja wamo katika maombezi ajili ya utulivu na mabadiliko ya mpito ya amani nchini Sudan.