
Flag of Ghana
Jumuiya yawa Ghana wa Maine ni ndogo, ila waMainers wazaliwa wa Ghana waliozungumza na Amjambo Africa! mwezi huu wametoa taarifa kwamba kundi la wenye silaha lilipiga massasi wakati wa uchaguzi wa mwanamemba mpya wa bunge. Haya yalitokea kunako kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi cha La Bawaleshie katika mji mkuu wa Accra ilipokuwa Alhamisi, Januari 31, 2019. Watu 8 kutoka chama cha upinzani, cha National Democratic Congress (NDC), walijeruhiwa, na wawili wao wako katika hali maututi. Sehemu ya wa raia wameripoti kwamba watu wanne walifariki kutokana na majeraha yalisosababishwa na kufyatuliwa masasi. Pamoja na hiyo, siku ile ya kupigwa masasi, idara ya polisi ilitoa ripoti kusema kwamba hakuna walio jeruhiwa. Iddi Yire, wa Shirika la Habari la Ghana, aliandika, “Ghasia, iliyotokea karibu na Kituo cha uchaguzi karibu na shule la msingi lawa presbuteri La-Bawaleshie jimboni la Ayawaso Magharibi mwa Wuogon, haihusiani kwa lolote lile na kura iliyofanyika kwa uchaguzi wa Bunge. Chama cha upinzani kimesema kama wafyatura masasi walitenda hivyo kwa ruhusa ya serikali, na hata wakamshitaki Rais Nana Akufo-Addo kusema kama alikuwa na nia ya kutisha wapiga kura kutoka chama cha upinzani. Vyanzo vyetu vinayo matumaini kwamba uchunguzi wa haki utaendeshwa ili kutambua wahalifu hao na kuwaleta mahakamani, kwa nia ya kukatisha tamaa kwa siku za usoni vitendo vya ukatili nchini. Wanaogopa kwamba matukio ya namna hii yanaweza kudhoofisha sifa ya Ghana, ambayo inaonekana kama nchi moja yenye kuwa imara na tulivu kisiasa miongoni mwa nchi nyingi katika kanda. Kikundi cha wanasheria wa Ghana kilishutumu unyanyasaji huo, wakiuita “kuwa mbaya sana juu ya sifa za kidemokrasia ambazo Ghana imepata kwa jasho na hili pia ni kama tishio kwa utawala wa sheria na demokrasia yetu.” Ushirika wa vyama vya Usimamizi wa Taifa uliongoza maandamano Februari 7, ili kupinga lile wanalo sema kuwa ni kuongezeka kwa kiwango cha juu cha usalama mdogo katika nchi. Wamesema kwamba usalama mdogo upo una hatarisha demokrasia ya nchi. Mamia ya raia waliungana na walio andamana. Zaidi ya wasiwasi hizo juu ya vurugu, vyanzo vyetu vinasumbuliwa pia kuhusu pengo kubwa lililoko kati ya “wanao” na “wasio” nchini Ghana. Wametambua kuwa bei za huduma na bidhaa hubadilishana kwa mwendo wa bei ya mafuta nchini Ghana – kila wakati bei ya mafuta ikikwenda juu, gharama za bidhaa na huduma pia huenda juu – ila, wakati bei ya mafuta inashuka chini tena, gharama za bidhaa na huduma zinabaki papo hapo kwenye ngazi ya juu.