Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon alirudi nchini Januari 15 wiki moja baada ya kushindwa kwa jaribio la kumupindua madarakani lililofanyika Januari 7 na kikundi kidogo cha maafisa wa ulinzi wa rais (Republican Guard). Rais Bongo alikuwa nje ya nchi kwa miezi kadhaa, huko Rabat, kwenye makao ya Mfalme wa Morocco akipata nafuu kutokana na kiharusi.

Alimtaja waziri mkuu mpya, Julien Nkoghe Bekale, ambaye ameapa katika serikali mpya, inaonekana kama jaribio la kutaka kuimarisha nchi. Waafisa waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa; wamoja wameuawa. Madhumuni yao yaliyotajwa katika jaribio hilo la kumuondoa rais ilikuwa ni kurejesha demokrasia kufuatia uchaguzi wa mwaka wa 2016, wakati ambapo Rais Bongo alishutumiwa sana kwa udanganyifu wa uchaguzi na uwizi wa kupiga kura.

Vyanzo vyetu vimeonyesha wasiwasi wao mkubwa kutokana na utupu wa madaraka unaosababishwa na magonjwa ya Rais Bongo na kutokuwepo kwake nchini. Wametambua katika kurudi kwake kwamba ameonekana kwenye picha akiketi kwa kiti cha magurudumu. Wanahofu kwamba hawezi tena kuongoza nchi hapo mbeleni.

Gabon ni nchi tajiri yenye rasilimali za asili, na ina idadi ya watu milioni 2 tu. Pamoja na faida hizi, hata hivyo, imesumbuliwa kiuchumi wakati wa utawala wa Rais Bongo. Watu wa Gabon wanaomba ajili ya siku bora zijazo.