Watu kutoka jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanaoishi hapa Maine wanashukuru kwamba Rais mteule Tshisekedi aliyepishwa hapa karibuni ameamuru jeshi la Congo kuingilia kati dhidi ya kikosi cha Amirijeshi Mulumba Biloze Bishambuke. Mashambulizi ya Biloze Bishambuke kwenye eneo la Minembwe Kusini mwa Kivu ya Kusini imepelekea vifo vya watu 60 kwa mwezi uliopita na kuharibu vijiji 23, ikiwa ni pamoja na nyumba, bidhaa, na mashamba. Maelfu ya mifugo pia yameibwa. Kwa maagizo ya Rais Tshisekedi, jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo sasa linafanya kazi ya kushinikiza na kurudisha wanamgambo nyuma, pia kurudisha kwa mifugo iliyoibiwa, na kulinda mkoa wa Minembwe, ambao ulikuwa karibu na kuangukia kwa mikono ya wanamgambo. Wakazi wa Congo walio hapa Maine wanahimiza serikali yao, na serikali ya Marekani, na jumuiya nzima ya kimataifa kushutumu mauaji yote iliyo fanyika na vikosi vyote vya wanamgambo na kuwaleta viongozi wake mahakamani. Watu milioni sita wamekufa DR Congo tangu mwaka wa 1996 kama matokeo moja kwa moja ya migogoro hiyo.