Daktari. Abdullahi Ahmed, makamu msaidizi wa kiongozi mkuu wa Shule la Sekondari la Deering, pa Portland, alichukua muda kwa Ijumaa hapa karibuni iliyo kuwa yenye kazi nyingi ili kugawanya mawazo na wale ambao anaamini wangekuwa msaada kwa wasomaji wa kikaratasi  hiki – kwa kipekee  wasomaji ambao ni wahamiaji wazazi kutoka nchi zilizo na shule zenye mifumo tofauti na hizi za hapa kwetu Maine.

Akiwa muzaliwa toka Somalia, utafiti wake wa ki daktari wa Ahmed ulihusika na uhusiaji wa wazazi wakimbizi katika mfumo wa shule za Marekani, pia alikuwa na maslahi maalum katika elimu kwa watoto wahamiaji. Ametambua  kwamba elimu ni muhimu katika maamuzi ya mwendo wa maisha, na kwamba katika mfumo wa shule za Marekani, uhusiaji wa wazazi katika elimu ya mtoto ni muhimu. Amesema kwamba nafasi ya mwanafunzi kuachana na janga la umaskini ume boreshwa sana na wazazi kuhusika ipasavyo katika elimu ya mtoto.

Daktari Ahmed anasisitiza kwamba katika nchi nyingi, shule na maisha ya nyumbani huonekana kama sehemu mbili tofauti sana. Wazazi wanatarajiwa kutunza watoto nyumbani, wakati ambapo waalimu na waongozi wanahusika nao  huko shuleni. Katika nchi hizi mtazamo wa jumla zidi ya shule ni  ‘Hamna habari ni habari njema!’ Mara nyingi hakuna vitu kama vile maonyesho ya wazi ya wazazi, mikutano kati ya wazazi waalimu, kuendesha safari za mashambani, kufuatilia maendeleo ya kitaaluma alama kupitia mifumo ya kompyuta, jioni za upashaji wa habari za viuo vikuu, na pia kupenda.

Daktari Ahmed anasema kwamba wahamiaji wapya hapa Maine hawaelewi papohapo kwamba mahali hapa wazazi wanatarajiwa kushiriki sana katika mafunzo ya watoto wao. “Hapa wazazi wanapaswa kuhudhuria matukio, kuhakikisha kuwa kazi za nyumbani zimefanyika, kutetea mahitaji ya watoto wao kwa waalimu, wasimamizi, na kwa bodi la shule.” Amesisitiza hasa umuhimu wa wazazi kuchungua zaidi kuhusu mahudhurio shuleni

Amesema kwamba wazazi wanahitaji kuhakikisha kuwa watoto wao – zaidi watoto wao walio kwa shule za sekondari – wanahudhuria shule mara kwa mara. Amesema kuwa ikiwa simu ya robot inakuja kutoka shuleni kumjulisha mzazi kuwa mtoto amekosa shule, mzazi anapaswa kuwasiliana na shule. Amewashauri wazazi wasikubali mtoto kuhakikisha kwamba sio shida ni sawa hata wakati yeye hakukuwa shuleni. Humu Maine kunazo sheria juu ya mahudhurio ya shule – watoto wanalazimishwa kuwa shuleni isipokuwa tu wameombewa ruhusa na mzazi. Zaidi ya hayo, mafanikio ya kitaaluma huhusiana sana na mahudhurio shuleni.  Daktari Ahmed anasema kuwa ikiwa njia ya mawasiliano ni tatizo kwa sababu ya kutosema Kiingereza zaidi, mzazi anaweza kuomba mtafsiri. Humu Portland Kituo cha Lugha na tamaduni tofauti (Multilingual and Multicultural) kinaweza kutoa mtaalamu wa mawasiliano ipatikanayo katika lugha ya mzazi. Daktari Ahmed anasisitiza kwa dhati kwamba simu ya robot ifikapo haipaswi kamwe kupuuzwa.

Jumla ya ujumbe Daktari Ahmed aliotaka kuachia wasomaji ni kwamba ni muhimu wazazi kujua jinsi ulivyo mfumo wa shule humu Maine ili waweze kuwasaidia watoto wao katika kufanikiwa nchini Marekani. Wazazi hawapaswi kudhani kwamba mfumo huo ni sawa sawa na ule ulio katika nchi yao ya asili – kwa kweli, inawezekana ni tofauti kwa njia muhimu sana.