From the Desk of Dr. Ahmed 

Kuzunguka kati ya mfumo wa shule ya Amerika ni changamoto kwa wanafunzi na familia wasio wazaliwa wa Marekani. Shule zina wafanya kazi wengi wanao jukumu la kusaidia maeneo yote yanayohusiana na elimu. Changamoto kwa wale walio wapya kwenye mfumo hiyo ni kutafuta nani wa kuongea naye na kwa suala gani. Kwa mfano, familia inaweza kuwa na matatizo kupata usafirishaji kwa mtoto wao kwa kwenda na kutoka shuleni. Ao mtoto wao anaweza kuhitaji msaada kwa mchakato wa maombi ya chuo kikuu. Shule zina wafanyikazi tofauti kwa kusaidia na kila moja ya maeneo haya – na kwa mengine mengi zaidi.
Kwenye safu yangu ya mwezi wa Mei (inayopatikana kwenye mtandao: amjamboafrica.com) nilifasiria kwamba shule zina wafanya kazi wa kijamii ambao huduma yao ni kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji msaada. Kwenye safu yangu niliwahimiza wazazi kuwasiliana na mfanyikazi wa kijamii wa shule ya mtoto wao kwa ajili ya wasiwasi wowote ule kuhusu jinsi anavyoendelea.
Shule pia zina washauri wa mwongozo, na kila mwanafunzi katika shule ya secondari hupewa mshauri wa mwongozo mwanzoni mwa mwaka. Mshauri huyu wa mwongozo hufanya kazi na mwanafunzi mwaka wote. Katika shule zingine, wanafunzi hubaki na mshauri huo huo kwa miaka kadhaa. Washauri wa miongozo hutoa huduma kama vile ushauri wa kitaaluma, ushauri wa kazi, na ushauri wa kibinafsi.
Ifuatayo hapa chini ni huduma kadhaa ambazo washauri wa mwongozo hutoa kwa wanafunzi wa shule ya secondari:

• Washauri wanatumia zana na mbinu za msingi wa utafiti
ili kuwasaidia wanafunzi kugundua uwezo na maslahi yao.
• Washauri huwafundisha wanafunzi mikakati ya kusu
luhisha shida inayo wasaidia kufanikiwa darasani na shuleni.
• Washauri wanatumika na wanafunzi pamoja na familia kwa
kuunda programu na ratiba za wanafunzi. Wanawaongoza
wanafunzi katika kuchagua kozi zinazolingana na maslahi yao na kiwango cha utaluma. Washauri wa mwongozo
wanaweza pia kusaidia wanafunzi kuchunguza mbinu ao
biashara kadhaa.
• Washauri huwasaidia wanafunzi kujiandikisha madarasani
katika vyuo vikuu vya jamii na vyuo vikuu wakati bado
wako katika shule ya sekondari. Hii inaweza kuwa chaguo
nzuri kwa wanafunzi walio na nia ya kusoma.
• Washauri wanakutana na wanafunzi mmoja mmoja na
katika vikundi ili kuwasaidia na mchakato wa maombi ya
chuo kikuu.
• Washauri wanashughulikia maombi ya vyuo vikuu kwa
wanafunzi. Wanayatuma maandishi ya alama za wanafunzi
na vifaa vingine vya kusaidia ikiwa ni pamoja na barua za
pendekezo kwa ofisi za uandikishaji wa vyuo vikuu.
Ushauri wa mwongozo unaweza kuchukua jukumu muhimu sana katika elimu ya mtoto wako. Wazazi na wanafunzi wanapaswa kuhakikisha kuwa wame jitambulisha kwa mshauri wa mwongozo wa mwanafunzi mwanzoni mwa mwaka wa shule