Naye Kathreen Harrison
Warsan Shire: Hakuna mtu anayeondoka nyumbani isipokuwa kama nyumbani ni kinywa ya papa

Moving out of the Expo Photo | KGH

  Kwa mtu kutoka DR Congo, ukilaza mkono uliofunguka juu ya ngumi, ishara hiyo inamaanisha:”Unaongea saana.” Ikiwa unamwita mtu mwingine kwa kuchezesha kidole chako cha shahada, ishara hiyo ni dharau. Hizi zilikuwa zingine ya vidokezo vilivyoshirikiwa na wale waliohudhuria mafunzo ya kitamaduni na kikao cha habari kilichofanyika Jumamosi, Agosti tarehe 10, katika Huduma za Jumuiya ya Gateway huko Portland.
Kikao hicho cha masaa mawili kiliongozwa na Family Promise of Greater Portland, Catholic Charities Refugee and Immigration service, na Yarmouth Housing Initiative, na iliandaliwa kwa malengo ya kusaidia kutayarisha jamaa za makaribisho ao zinazofikiri kuwa karibisha wakimbizi waomba hifadhi majumbani kwao.
Pamoja na tarehe ya mwisho ya kuondoshwa kutoka Jengo la Expo lililowekwa kuwa kama Alhamisi, Agosti 15 kwa sababu ya majukumu walio patana, Expo hiyo ilifungwa kwa upokezi wa wageni wapya waliofika hadi tarehe Agosti 10. Kwa Familia yoyote mpya ambayo ilifika Portland baada ya tarehe hiyo ilipelekwa kwa Makao ya kuchangia ya Familia. Kulingana na Jessica Grondin, Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Jiji la Portland, na kwa kuwa tangu Agosti 12 Makaazi ya Familia hayo yalikuwa yamejaa, kila mutafuta hifadhi yeyote ambaye hakuwekwa katika nyumba zingine hadi tarehe Agosti 15 alihamishwa kunako Ghala la kufurika.
Sehemu kubwa ya wakaaji wa Maine husumbuliwa na uhaba wa nyumba, nao wanenaji kwenye kikao cha mafunzo ya kitamaduni na habari walifasilia kwamba watu wengi wasio na makazi katika eneo kubwa la Portland hulala usiku kwenye malazi ghala ya kufurika, kwa sababu Shelter Family ya Portland imeshindwa kwa muda mrefu kutoshelea watu wote wanaohitaji msaada tangu sasa miaka nne iliyopita. Walakini malazi ya kufurika hutumiwa tu wakati wa usiku, na mpangilio wa kulala ni kutandika mkeka kwenye sakafu ya Salvation Army-hali ngumu kwa mtu yeyote, aliye pekee kama familia pamoja na watoto wadogo.
Dana Totman, Mukurugenzi kunako Avesta Housig, amesisitiza kwamba kupata suluhisho la kudumu la nyumba kwa wale wanaotafuta hifadhi wa hivi karibuni ni changamoto. “Tayari tunao watu zaidi ya 2000 kwenye orodha ya kusubiri. Ikiwa ilikuwa rahisi kupata nyumba katika miji jirani hatungekuwa na watu 2000 kwenye orodha letu. Hali hii ina leta mwanga kwa shida ya kupata nyumba za bei nafuu inayopatikana katika Maine. ”
Watu wa Maine kutoka popote jimboni wamejibu kwa mwito wa kutoa makazi salama, ya muda mfupi kwa familia zinazotafuta hifadhi kwa kuwafungulia nyumba zao. Kutoka Kennebunkport hadi Fort Kent, familia zimepiga hatua mbele. Orodha ya miji iliyohusika kwa wakati huu ni pamoja na: Arrowsic, Auburn, Avon, Bingham, Blue Hill, Brunswick, Cape Elizabeth, Cape Neddick, China, Cumberland Foreside, Falmouth, Fort Kent, Freeport, Gardiner, Gorham, Grey, Hallowell, Holden , Kennebunkport, Lincolnville, New Harbor, North Yarmouth, Portland, Pownal, Saco, Scarborough, Sedgwick, China Kusini, South Portland, Westbrook, na Yarmouth.
Wakati Kristina Egan, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mikoa mikuu ya Portland (GPCOG), alipoarifiwa kuwa kulikuwa na wimbi la watafiti wa hifadhi waliofika Maine msimu huu wa majira ya joto, aliita kwa furaha muungano wa mashirika inayoegemea imani na mashirika ya kimataifa, kwa lengo la kupata maoni yao ajili ya suluhisho la makazi ya muda kwa kufunga pengo lililo kati ya wakati Expo inahitajika kufungwa, na makazi ya majira ya joto yalifunguliwa. Umoja huo uliunda mpango wa familia za mapokezi. Viongozi wa wahamiaji walihusika katika umoja huo tangu mwanzo, na wale viongozi walipendekeza kwamba ikiwa mpango wa familia za upokezi ungefanikiwa, mafunzo ya kitamaduni kwa pande zote yangehitajika. Kipindi cha Jumamosi kilikuwa mafunzo ya kwanza ya kitamaduni yaliyolenga kukaribisha familia. Waombaji hifadhi walianza kupata mafunzo ya kitamaduni wakati walikuwa bado wanaishi katika Jengo la Expo.
Wale waliohudhuria mafunzo hayo waliuliza maswali wakati wote wa unenaji, kwa uwazi walitaka kujifunza yote wanayoweza kufanya ili kuwakaribisha wageni wao namna ipasavyo. Mada zilizopangwa tokea nyama za ufugo, usafirisaji, kuandaa chakula, mikakati ya mawasiliano, hadi mitindo ya uzazi. Waliohudhuria walikuwa kama 80 na miaka yao ilikuwa inaogelea kati ya watoto wadogo hadi watu wazee. Madalali wa kitamaduni (kimsingi wanaoenda) kutoka kwa jamii ya wahamiaji, ambao kazi yao ni kujenga ulalo kati ya tamaduni – na ambao wanajua ni nini ina maanisha mara ya kwanza kujitengenezea njia katika nchi mpya – Hu saidia kuwa andaa wanao hudhuria kwa jukumu lao kama wakaribishaji.
Ingawa mwanzoni juhudi za kupata familia za kupokea wageni zili lenga kwanza maeneo ya mji mkuu, mwishowe, watafutaji hifadhi wengine wali wekwa katika nyumba zilizo mbali zaidi – wengine vijijini. Bwana Ly alisema kuwa shirikisho la wageni wao na ulimwengu wa asili unaweza kuwa tofauti sana kuliko ile iliyo ya wakaaji wa Maine. Barani Afrika, misitu hua na wanyama ambao wanaweza kuwa tishio kwa binadamu. Pia, wakati wa safari kwenda Marekani, wahamiaji hao labda walilazimika kuvuka Amazon, au misitu mingine kwa mwendo wa miguu. Kwa hivyo, wageni hapa watahitaji kuhakikishiwa kuwa maeneo yetu ya vijijini ni salama.
  Ushauri muhimu uliyopewa na wanenaji wote ulilenga kuwa nyeti kwa kutokana na machungu ambao waombaji hifadhi walipitia. “Ikiwa wamefanya safari hii, kuna uwezekano mkubwa kwamba wanahitaji kuponywa na mambo mengi kabla watapata nafuu,” alisema Sara Ewing-Merrill wa Family Promise of Greater Portland. Courtney Tabor, ambaye pia ni wa kikundi hicho hicho alikubali : “Labda wanaweza kuwa wameathirika katika nchi zao, kama vile pia kwenye safari yao ya kufika hapa” Makubaliano likuwa kwamba wanao pokea wata pashwa kusikiliza kwa makini ikiwa wageni watachagua kuelezea hadithi zao, na kuepukana na kuwauliza maswali juu ya safari ngumu, sababu za kukimbia, na kutaka kujua hali gani ya familia zao huko nyumbani.
“Ni jambo la kusumbua kuombwa kuelezea hadithi mara tena na tena. Tupo tunaunda nafasi ya usalama kwa watu hawa ambao wamepitia mengi sana. Ikiwa wageni wako wanagawanya hadithi zao, sikiliza tu – na ikiwa hadithi za kipekee zinashirikiwa, jiwekee hizo kwako pekee. Hadithi zao sio zako wewe kusemasema – na haswa sio kwa wapasha habari, amesema Carla Hunt wa YCHI. Wanenaji walisisitiza kwamba hadithi zozote zile za watu ambazo zinaambiwa kwenye vyombo vya habari hatimaye zitajumuishwa na kuwekwa kama ushahidi katika kesi za kuomba hifadhi za wageni wao, na ikiwa makosa yana fanyika katika huo hutangazaji wa mara tena, kesi za ukimbizi zinaweza kuhatarishwa.
Waombaji hifadhi wa hivi karibuni wako hapa kihalali, lakini njia ambayo kesi zao zitashughulikiwa haijulikane. Wakati wakimbizi hao walipovuka mpaka wa Kusini, wakitafuta usalama kutokana na mateso na unyanyasaji, mawasiliano yao ya kwanza humu Marekani ilikuwa na kituo cha Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE), badala ya kituo cha Marekani cha kazi za Uraia na Uhamiaji (USCIS), ambayo ndio kawaida. Kawaida USCIS inaongoza “kuhojiwa kuliko aminika” kwenye mipaka, ila waliofika hivi karibuni huko Maine hawakupewa nafasi ya mahojiano hayo – na kukosekana kwa mahojiano hayo ya kuaminika hufanya kesi zao kuwa kama jambo jipya kwa Wanasheria wa mradi wa Uhamiaji halali na Utetezi wa kiSheria (ILAP) . “Hii ni hali ngumu, na hatujui hii mchezo itachezewa je,” alisema Bi Ewing-Merrill. Wanasheria katika (ILAP) wanafanya kazi katika kusuluhisha hatua ya kuomba hifadhi kwa wageni hawa wapya. Kwa wakati huo huo, hadi ombi yao itakapo jazwa na kutumwa, na hii ni baada ya siku 150 na hapo, watafuta hifadhi hawawezi kufanya kazi. Muda wa kungojea hadi kesi za wakimbizi huchukua mara hata myaka.
Baba Ly, wa Catholic Charities na huduma kwa Wakimbizi na Wahamiaji aliongoza watazamaji katika hafla ya jukumu iliyotekelezwa ili kuwasaidia kutafakari kuhusu mambo ya utamaduni wao. Waliohudhuria walishirikishwa kwa hamu, na chumba kilijazwa na uwingi wa mazungumzo. Baadaye, Bwana Ly alisaidia kueleza yaliyo tukia, na akagawanya nao ujuzi wake kuhusu tamaduni.
“Humu Marekani, kujitambulisha binafsi kwa kuelezea kazi yako ni kawaida – lakini sio kweli kwa kila tamaduni,” amesema. “Na kawaida hatuzungumzii hali ya uchumi hapa, ambayo nayo sio kweli mahali pote ulimwenguni.” Bwana Ly alishauri wenyeji nyumba za upokezi kuwasiliana na mjuzi wa kitamaduni aliyetolewa kwa familia yao kwa msaada wowote unapohitajika. Zaidi ya yote, alisisitiza umuhimu wa “ujenzi wa uhusiano, ambao utafanyika kwa fadhili, uwazi, na kufanya utafiti wako mwenyewe juu ya utamaduni wa wageni wako.” Alikumbusha wahuzuriaji kwamba wako katika nafasi ya madaraka katika uhusiano na wageni wao, na isishangaze ikiwa wageni wanahisi kutaka kusema “ndio” kwa kila kitu wanachouliza.
Nsiona Nguizani, ambaye anafanya kazi kama mjuzi wa kitamaduni huko Brunswick, alisema, “Ni vigumu kwa wageni kusema ‘hapana’ kwa sababu ya hali waliyomo. Alisisitiza maoni ya Bi Hunt kuhusu media. “Watu wengine wanaweza pima kujificha ili kulinda familia nyumbani. Wengine wanataka kuzuia unyanyapaa wa kutokuwa na makao – wengi wa watu hawa walikuwa na hali nzuri huko nyumbani, na kutokuwa na makao ni ngumu kwa hali yao. ”
Luc Samuel K. Kuanzambi, kiongozi wa kitamaduni wa CocoMaine, Jumuiya ya watoka DR. Congo wa Maine, alishirikisha wengine mabadiliko ya nguvu yaliyo jitokeza kwa wanandoa ambao familia zao zinahama kutoka Afrika kwenda Marekani. Katika Afrika, mwanaume hutumiwa “kupiga risasi”, alisema. Hapa wanaume hugundua kuwa watoto na wanawake wana haki. “Hakuna kilicho waandaa kwa kupindua huko” alisema, na kusisitiza kuwa marekebisho ya kitamaduni huchukua muda usio mchache.
Sababu za kufungua nyumba za makaribisho zilitofautiana kutokana na wale walio hudhuria. Margaret Minister, kutoka Cumberland, alisema, “Nilizoea kuwa na watu wengi karibu yangu. Watoto wangu wawili wameenda kwa chuo kikuu, na hawa watu wana mahitaji, basi.… ”Gerri Sauer na Russ Cowles, wa Durham, wali fafanua ya kwamba wapo na ghorofa ya chini ambayo imetayarishwa kutumika kama ya kuleta hewa. Bi Sauer alishikwa na wasiwasi. “Nilihisi hii ilikusudiwa kuwa,” alisema. Mnamo tarehe Agosti 10 walikuwa wakisubiri kwa hamu kutembelewa nyumbani na ujumbe kutoka kwa Halmashauri ya Ufundi wa Kimataifa wa Kielimu (CIEE), shirika ambalo lilifanya uchunguzi wa msingi kwa wale wote ambao waliojaza kikartasi cha ombi ya kuwa mwenye kukaribisha wageni, na wame hojiwa moja kwa moja pamoja na majeshi yote ya wale wanaopatikana nje ya eneo la Greater Portland. Wale wenyeji katika eneo la mji mkuu walihojiwa na washiriki wa kikundi cha kiongozi wa wahamiaji. Ili kusaidia familia zinazo karibisha wageni na wageni walio nje ya mji, GPCOG imeanzisha orodha ya ma dereva wa kujitolea kwa usafirishaji kwenda kwa miadi na kwa ununuzi wa chakula.
Jen McAdoo, Mkurugenzi Mtendaji wa Furniture Friends, alizungumza kwa wale walio kuwepo wakati akiwashukuru wanenaji na viongozi wa wahamiaji kwa juhudi zao. Philip Walsh, Mkurugenzi Mtendaji wa Maine Initiatives, aliahidi mipango ya Maine Initiatives kuendelea kusaidia uhisani wa mashirika yanayosaidia mashirika inayoongozwa na wahamiaji.
Mufalo Chitam, Mkurugenzi Mtendaji wa Ushirikiano wa Haki za Wahamiaji wa Maine (MIRC), alionywa kupitia simu mapema mwezi wa Juni kwamba watu kadhaa wanaotafuta uhifadhi wa KiAfrika walikuwa wakielekea Portland. Tangu
wakati wakati huo, wahamiaji 437 wamewasi.
Bi McAdoo alibaini kwamba watu wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu zaidi karibia miezi miwili kukaribisha wakimbizi, ikiwa ni pamoja na kuunda mradi wa “Nyumba za makaribisho” kama suluhisho kwa muda la makazi.
Bibi Chitam alionya, “Nyumba za makaribisho ni mpango mpya. Kila kitu kiko katika mchakato. Tunakuomba utuwe radhi wakati tunapo kusanya rasilmali. ”Majifunzo yalimalizika kwa umakini mkubwa, na wakaribishaji wakikusanyika katika jozi na vikundi vidogo vya kushiriki maudhuri kutoka kwenye kikao na pamoja na juhudi za kujijulisha mmoja kwa mwengine.