Kama vile familia za vijana wavyofahamu, gharama kuhusu kuzaliwa kwa motto zinaweza panda juu haraka sana Kwa bahati nzuri kuna zana na mipango ya kusaidia jamaa kupata muda wa kuwajali watoto wao wachanga.na pia kuimudu gharama za kabla na baada ya kuzaa.

Nchini Marekani, ikiwa mtu hufanya kazi kwenye kampuni ya wafanyakazi 50 au zaidi, Family and Medical Leave Act(FMLA) inashurtisha mwajiri kuwaruhusu wamama kuchukua wiki 12 ya likizo isiolipwa kila mwaka baada ya kuzaa ama kupokea nyumbani mtoto ambaye hana wazazi. Muda huu wa kupumzika ni wa ajabu, lakini vipi kuhusu kupata pesa wakati huu?
Kuna njia chache za kupata mapato karibu ya wakati wote ama wakati wote mtu yuko nje wiki 12 Kwa mfano muda huu wa kutolipwa hauhitaji kutumiwa tu kwa likizo. Ingawa ni muhimu kujitenga na mwajiri wa mfanyakazi kuhakikisha kuwa sera zinatekelezwa, , PTO yoyote ilioifadhiwa inawezakutumika kwa likizo la uzazi wa mama au wa baba. Vilevile siku za mtu binafsi ama za ugonjwa zinaweza tumiwa hivyo hivyo.Ulemavu wa muda mfupi unaweza tumiwakwa hadi wiki 6 baada ya kuzaliwa motto kati ya asilimia 50 na asilimia 100 ya mapato ya kawaida, kufuatia kipindi cha kuondoa kilichowekwa.Mara faida zote zinapotumiwa, mzazi anaweza kubaki nje ya kazi kama atakavyo, hadi wiki 12 zilizowekwa na FMLA

Jimboni Maine waajiri hutoa bima kwa wafanyakazi, bima hizo huhusika na gharama za uzazi. Kama si hivyo, MaineCare hutoa bima ya afya kwa bure ama kwa gharama nafuu kwa wale ambao hujaza vigezo. Medicare, Medicaid, Children’s Health Insurance Program pamoja na bima kupitia sokoni wanaweza pia kusaidia jamaa kupata bima ikiwa mwajiri hatowi huduma hiyo ama ikiwa mtu hafanyi kazi yoyote.

Pamoja na programu na zana hizo, kutakuwa kila mara gharama zingine za matibabu kutoka mfukoni.. Ndio maana wazazi wanapaswa kuwekeza pesa zao iwezekanavyo Aina Fulani za akaunti kama vile Flexible Spending Accounts(FSA) na Health Savings Accounts (HAS)hazisaidie tu wazazi kuwekeza kwa ajili ya matibabu, lakini pia zina faida ya ushuru vilevile… Kwa FSA, mchango wa pesa kwenye akaunti hiyo hutolewa kutoka kwa mapato kabla ya ushuru, na hivyo kupunguza ushuru kwa mapato yake.Hata hivyo,pesa zote zinapaswa kutumiwa mwisho wa mwaka, kama si hivyo zinapotezwa. Pamoja na HAS pesa zinaweza kusonga kwa mwaka hadi mwaka na pia kukatwa kutoka kwa mapato kabla ya kutoa ushuru. Kuchangia kwenye HAS lazima mtu ajiandikishe kwenye mpango wa afya wenye kupunguzwa sana

Ingawa wakati mwingine inaweza kuwa ya bei kali na yenye changamoto, wazazi wengi husema kuwa kupata motto ni uzoefu kamili zaidi maishani mwao. Kujifunza kuhusu zana inaweza kusaidia kurahisisha uzazi