by Jean Damascène Hakuzimana
Maadui wa miongo kadhaa, Eritrea inaweza kuwa inasaidia Ethiopia katika vita vyake dhidi ya eneo la Tigray, ikituma maelfu ya wanajeshi kuvuka mpaka ili kupigana pamoja na vikosi vya Ethiopia wenyewe katika harakati za kukandamiza uongozi wa Tigray. Hii ni kulingana na Reuters, ambayo vyanzo vyake ni pamoja na wanadiplomasia wa Marekani. Picha za setilaiti na ushuhuda zimethibitisha ripoti hiyo. Tigray ni mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia ambao umekaidi serikali ya shirikisho ya Abiy Ahmed.
The Guardian inaripoti kuwa ushiriki wa Eritrea utasumbua zaidi mzozo uliokwisha kubanwa, na unaweza kulazimisha Marekani, ambao ilikuwa hapo kitambo mshirika mmoja katika mkoa huo , kuchukua msimamo tofauti juu ya Ethiopia, ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali mbovu ya Eritrea. Mataifa yote mawili yamekataa ushirikiano huo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaka kukomeshwa kwa uhasama kati ya wapiganaji mnamo Novemba, lakini wito huo haujasikilizwa.
Eritrea wakati mmoja ilikuwa sehemu ya Ethiopia. Katika miaka ya 1970 chama cha Eritrean Peoples Liberation Front (EPLF) kilipambana pamoja na TPLF kumuangusha Mengistu Haile Mariam, dikteta wa wakati huo wa Ethiopia, kumnyatua madarakani mwishowe kulifanyika mnamo 1991. Mnamo 1990, Eritrea ilitangaza uhuru na ikawa taifa huru. TPLF ikawa yenye nguvu kubwa nchini Ethiopia, na hii iliendelea kwa karibu miaka 20. Wakati wa enzi zake, makabila mengine yalitengwa, hadi uasi wa 2018 ambao ulimtengenezea njia Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutoka kabila kubwa la Oromo kupaa madarakani. Mara tu alipozinduliwa, Tigray ilianza kugombana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed na ajenda yake ya kisiasa, na kugombana huko kumeongezeka hadi kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Karibu na mwanzo wa vita hivi vya silaha, TPLF, ikishambuliwa na serikali ya shirikisho, ilirusha roketi kwenye mji mkuu wa Eritrea wa Asmara. Mnamo Desemba 1, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alitangaza kwamba serikali ya shirikisho imechukua udhibiti wa mkoa wa Tigray, na kuahidi kujenga upya miundombinu yake iliyoharibiwa. Reuters inaripoti kuwa TPLF haijakubali, lakini badala yake imeapa kuzidisha mashambulio yake pande tofauti. Wataalam wana wasiwasi juu ya vita vya guerilla vinavyoanzishwa, ambavyo vinaweza hatarisha utulivu katika mkoa huo.
Wakati huo huo, maelfu ya wakimbizi wamekimbia mapigano na kuvuka kwenda Sudan.Mashirika ya kibinadamu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamezitaka pande zote mbili za mzozo kuruhusu ufikiaji wa usaidizi wa kibinadamu kwa watu wenye mahitaji. Guterres pia ameelezea wasiwasi wake juu ya uwezekano wa ukiukaji wa haki za binadamu na amehimiza kurejesha haraka sheria.