Maana kufadhili elimu inaweza kuwa na gharama kali, mara nyingi watu wanahitaji msaada ili kulipia gharama za masomo ya vyuo vikuu. Shule zinatoa misaada ya kifedha ili kufanya uhudhuriaji wa taasisi yao iwe rahisi zaidi kwa waombaji wanaostahili. Mifundo ya kawaida ya misaada ya kifedha inajumuisha chaguzi kadhaa ambazo hukuruhusu kusoma na kisha ulipe baadaye ukisha hitimu. Katika nakala hii, tutafafanua tofauti zilizopo ili kukusaidia kuamua ni zipi zinazofaa kwako. Kwa bahati nzuri, kuna chaguzi kadhaa ambazo zinaweza kusaidia kufungua njia ya kufuata utimilifu wa ndoto zako pamoja na elimu nzuri.

Ruzuku na udhamini
Hii ni pesa uliyopewa ambayo kwa kawaida haiitaji kulipwa. Ruzuku inaweza kutoka moja kwa moja kutoka kwa shule au kutoka kwa jamii au mashirika ya serikali. Hizi husaidia watu wanaofanya kazi kwa bidii au wanafunzi wazuri kupata elimu ya juu. Kwa sababu pesa hii hai hitaji kulipwa, kwa hivi kutafuta misaada na udhamini ni hatua nzuri ya kwanza ya kulipia kupata digrii yako. Ongea na shule unayotaka kuhudhuria, mashirika ya jamii unayohusika nayo, au mshauri wa shule ya secondari kuhusu jinsi gani ya kuomba ruzuku au udhamini.

Mikopo ya Shirikisho kwa Wanafunzi.
Baada ya kuchunguza kwa makini chaguzi zilizopo za udhamini na ruzuku, tuma ombi lako la Mkopo ya Shirikisho. Mkopo huu wa serikali umeundwa ili kuweka njia rahisi za ulipaji na viwango vya chini vya riba. Kwa kawaida, malipo ya mkopo hutokea baada ya kuhitimu. Kwa kuomba, chungua kwa https://studentaid.gov/ baadaye ujaze fomu ya FAFSA (Ombi ya Bure kwa Msaada Shirikisho kwa Wanafunzi).

Mikopo ya kibinafsi kwa Wanafunzi.
Unaweza kupokea mikopo hii kutoka kwa taasisi ya kifedha kama shirikisho la mikopo, benki, au mkopeshaji mkondoni. Mikopo hii ya kibinafsi kwa kawaida huwa na viwango vya juu vya riba na inapaswa kuwa ya mwisho katika aina ya kutafuta fedha, kiisha kutafuta ruzuku, udhamini, na mikopo ya shirikisho kwa wanafunzi.

Mikopo ya shirikisho na ya kibinafsi hailazimishwi kulipwa hadi utakapohitimu, lakini bado inaendelea kuongeza riba ambayo huanzishwa siku hiyo ambayo unapokea mkopo. Ikiwezekana, ni vizuri kulipa sehemu ya riba hii wala salio ya mkopo huo mapema uwezavyo. Hii itapunguza kiwango cha riba ambayo hatimaye utadaiwa kwa mkopo mzima.

Baada ya kuhitimu, unaweza kurahisisha mchakato wa ulipaji kwa njia kadhaa tofauti ili kuifanya iweze kuwa yenye kudhibitiwa zaidi. Ukiwa una mikopo mingi ya wanafunzi ya kulipa, unaweza kuimarisha mikopo yote pamoja na kwa hivyo unahitajika tu kufanya malipo moja kila mwezi. Hii inaitwa ujumuishaji wa mkopo.
Chaguo jingine la kuzingatia ni kufadhili tena mkopo wako wa mwanafunzi au mikopo. Unapobadilisha mkopo huo, unaweza kupata mkopo wa kiwango cha chini cha riba, ambacho kinaweza kupunguza malipo yako ya kila mwezi na inaweza kuokoa pesa yako kwa kipindi chote cha ulipaji.

Ikiwa una maswali, anza na mshauri wako wa masomo, idara ya misaada ya kifedha shuleni kwako, au afisa wa mkopo katika taasisi ya kifedha ambayo inatoa mikopo ya wanafunzi. Watafurahishwa sana kukusaidia kupanga kwa hatua hii muhimu ya safari yako ya elimu.