Kwa alasiri fulani kila wiki, vyumba vya jumuiya kwenye maktaba ya Umma ya Lewiston pamoja na maeneo kadhaa jirani ya Lewiston na Auburn hujazwa na watoto, sanaa ya kuona, muziki. Watoto wakiwa wanaunda sanaa na ku athiriana na wataalamu wa sanaa tabibu na kufunza wasanii wa Lori sanaa. Shirika sabili la tiba kwa usanii, Lengo la Lori sanaa ni kutoa mazingira ya ubunifu na ya ushirikiano kwa vijana wenye ufikiaji mdogo au la kwa sanaa. Shughuli za Lori sanaa linawahimiza vijana kueleza wazi fikra za ubunifu wao, mahusiano, na uzoefu ndani yao, miongoni mwa wenzao, na katika jamii zao. Watoto walio wengi katika mipango ya Lewiston na Auburn ni wa asili ya Afrika, hasa kwa Somalia.
Mkurugenzi Mtendaji Jamie Silvestri ni mtaalam wa sanaa ya tiba ambaye alianza lori sanaa tiba katika muji wa Bath, Maine, mnamo mwaka wa 2004, kama ushirikiano na Ofisi ya Maendeleo ya Jiji la Bath. Lengo lilikuwa ni kutolea maeneo ya chini ya upendeleo ujirani bora, mpango wa sanaa za matibabu ili kuimarisha maisha ya vijana ambao hawakuwa nafasi kwa huduma za kijamii na shughuli za burudani. Waki himizwa na viwango vya juu vya uhudhuriaji, washiriki wenye shauku, na wazazi walio jaa shukurani, Lori sanaa liliendelea na huduma zake kwa miaka 15, wakiwa na msaada mkuu wa jamii na msaada wa wafadhili. Lori sanaa linafanya kazi pasipo malipo baada ya saa za shule na wakati wa ratiba za majira ya joto katika Bath, Biddeford, na Brunswick na, tangu mwaka wa 2006, imekuwa kwenye Maktaba ya Umma ya Lewiston na ” ujirani wa eneo la mtaani ” pia imekuwa katika eneo ya Maendeleo ya Familia la Auburn na Broadview tangu mwaka 2008. Lori sanaa pia ina mpango katika Shule za Umma za Lewiston na kwenye mashirika mengine kandokando ya Maine ya kusini.
Ingawa sanaa tiba ni jukumu kubwa, usoni mwa nchi, vikao vya lori la sanaa ni zaidi ajili ya kujifurahisha. “Tulikuwa tukifanya mradi wa kufanya vyombo na mmoja wa wanafunzi wetu kutoka Chuo cha Bowdoin ni mwanamuziki,” Bibi Silvestri anasema. “Sisi daima huchukua ngoma zetu nasi. Watoto walianza kufurahia muziki. Juma lililo fuata, mkufunzi wetu alileta gitaa yake. Ikawa tulifikia kuwa katika kupiga muziki, na watoto kwenye ngoma, na kujenga papo hapo picha ya usanii unao onekana. Ilikuwa hivyo tu na furaha ya pamoja. Watoto walihisi kuwa wameunganishwa kwa aina zote za sanaa. “Watoto wanavutiwa na ngoma,” Bibi Silvestri anasema. “Na wakati mwingine tutageuza pazia la takataka chini juu, na wakati mwingine tutashirikisha wengine. Ni majira ya kujifurahisha na kila mtu atakaye anaweza kujiunga. ”
Lori sanaa linafanya kazi kwa kanuni kwamba kujenga sanaa inalenga kuhimiza hatua za kutafakari binafsi, kujitambua, kujieleza, na kujitolea, yote yana msingi katika haja ya binadamu ya kuwasiliana na kujua. Programu zinawatumikia wote wavulana na wasichana, wenye umri wa miaka 3-18, kwa wenye uwezo wote na jinsia zote. Kupitia sanaa, vijana wanaweza kugundua maana mapya ya mahusiano kwa sababu sanaa hutoa bandia salama na yana yoonekana kwa mawazo na hisia za msingi. Kwa mandhari yenye maana kama Nani Mimi, Ni nini Inaniletea Amani, na Je, Ndoto Zangu, Lori sanaa inahimiza vijana kushiriki malengo na matumaini na kikundi. Kila wiki, ArtVan huleta mandhari mpya ya mradi na mbinu, na anawaambia watoto, “Unaweza kutumia wazo hili au kufanya chochote unachotaka.” Watoto wanafurahi juu ya uhuru wa kuchagua jinsi ya kufanya mradi, na hii inawasaidia kupata kujiamini kama Lori sanaa inaadhimisha uwezo na ubunifu. Programu ya Lori sanaa husaidia vijana kuanza kujiona wenyewe, wenzao, na jamii zao kwa njia tofauti. Kufanya kazi ya kujenga picha, ngoma, utendaji, au kipande cha kuandika inahitaji kujidhibiti na kuwasiliana na wengine, na inahitaji kuchukua hatari ya kujaribu jambo jipya au la ajabu
Mchana mmoja katika kitongoji cha Broadview Acres huko Auburn, watoto walikuwa wakifanya kazi na udongo. Kama kijana wa Euro-Amerika aitwaye John alibadilisha udongo wake kutoka kiumbe mmoja hadi kingine, alizungumza kuhusu kujifunza Yemen katika darasa lake la nne. John alihuzunika kujua kwamba watoto wa Yemen walikuwa na njaa. Kiumbe cha udongo ambacho hatimaye alicho kiumba kilikuwa cha nyani ya kuruka kichawi ambayo ingeweza kuwaletea chakula.
Siku ile ile, wakati mvulana mmoja aitwaye Abduramon alijiunga na kikundi hicho, alizungumza Kiarabu kwa kaka yake ambaye alikuwa amemfukuza. John mara moja akaangalia juu akiuliza, “Unasema nini?”
Abduramon akajibu, “Kiarabu.”
“Ndio maana watu wa Yemen wanasema,” alisema John.
Wakati sanaa ya kila mtu ilikuwa imekamilika na watoto waligawana uumbaji wao, Abduramon alijaza mfuko wa begani wa John na “chakula” cha udongo alichokifanya. John akaruka nyati yake juu mbinguni ili kutoa chakula kwa watoto wenye njaa huko Yemen. Kisha John akasema, “Wanakuletea chakula kwa wewe kujaribu.” Katika chumba, watoto walishiriki chakula, na kila mtu akatabasamu na akacheka.
Hadithi kama hizi hutokea kila siku katika vikao vya lori sanaa. Watoto wanaungana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja. Kupitia Lori sanaa, wanajifunza ujuzi wa kuelezea hisia zao kwa njia za kipekee inayowasaidia kutafakari na kushughulika na mambo yanayojitokeza katika maisha yao binafsi na katika ulimwengu pana.