Naye Kathreen Harrison

Mnamo tarehe Mei 27, Kituo cha Maine cha Kudhibiti Magonjwa (CDC) kilisasisha data yao kuhusu viwango vya maambukizi ya COVID-19 miongoni mwa watu wa rangi kuwa zaidi ya asili mia 25 ya jumla ya kesi, ao zaidi ya mtu mmoja juu ya watu wane walio ambukizwa humu Maine. Wakati ofisi ya sense ya mwaka wa 2019 inao yesha kwamba watu wa rangi wana jumlisha tu asili mia 7 ya wakaaji wa Maine. Kwa wakati huo huo zaidi ya asili mia 20.07 wa jumla ya maambukizi ao zaidi ya mutu mmouja kati ya watano walio ambukizwa hupatikana miongoni mwa watu weusi ao wa Marekani wenye asili ya Afrika. Na kiwango hicho cha uambukizi kisicho sawasawa kiko kinaongezeka kwa haraka haraka. Mnamo Aprili 29, tarehe ya kwanza ambapo CDC ilitoa data kwa kila kabila na kabila, kiwango cha jumla ya maambukizi ya Watu weusi au WaMarekani wenye asili ya Afrika walinaoishi Maine ime simama kwenye asili mia 5.09. Kwa wakati huu, huo utofauti wa viwango vya maambukizi miongoni mwa kabila na makabila ulionekana kuwa mupana – na sasa imekuwa mbaya, tena mbaya sana.

Isitoshe zaidi, zaidi ya asili mia 16 ya jumla ya maambukizi miongoni mwa watu weusi au wa Marekani wenye asili ya Afrika wakaaji wa Maine, wakati hesabu zinaonyesha kwamba asilimia 1.6 ya wakaaji wa Maine ni Weusi au Wamarekani wenye asili ya Afrika. Na kwamba kiwango hicho cha maambukizi kinaendelea kuongezeka. Mnamo tarehe Mei 13, ilisimama kwa asili mia 11.82; wiki iliyopita ilikuwa asili mia 7.67; na Jumatano, tarehe Aprili 29, ambayo ilikuwa mara ya kwanza kwa CDC kutowa data kwa kabila na kabila, kiwango cha jumla ya maambukizi ya watu Weusi au cha waMarekani wenye asili ya KiAfrika wa Maine ilikuwa asili mia 5.09. Kwa wakati huu, utofauti wa viwango vya maambukizo kufuatana na kabila na makabila ulionekana kuwa mupana. Tangu hapo, Imeongezeka zaidi ya mara tatu.

Viongozi wa jamii za wahamiaji wa Maine na washirika wao hawashangazwi na utofauti wa athari isiyo sawasawa ya virusi kufuatana na kabila na makabila. Walikuwa walitabiri mapema juu ya hiyo kwamba COVID-19 ita wapiga zaidi jamii za wahamiaji katika jimbo hili kwa sababu ya hali duni ya kiuchumi na kijamii ambayo inakubaliwa sana kuathiri afya ya umma. Walihamasishwa haraka, katikati ya mwezi Machi, na juhudi hizo za mapema zimepata kuhifadhiwa.

“Tuliipatia kazi ya majibu yetu ya Covid-19 hisia za dharura tangu hapo mwanzoni. Kwa sababu ya utofauti uliopo katika upatikanaji wa huduma za afya na vizuizi kutokana na lugha, miongoni mwa mambo mengine, ilikuwa tu ni suala la ‘wakati’ jamii zetu zitakuya ku athirika vibaya, wala sio “ikiwa”, alisema Mufalo Chitam, mkurugenzi mtendaji wa Ushirikiano wa Haki za Wahamiaji wa Maine (MIRC), katika barua pepe. MIRC ni muungano wa mashirika 69.

Mufalo Chitam, Executive Director of Maine Immigrants’ Rights Coalition

“Tangu Machi, wakati virusi hivi viliporipotiwa mara ya kwanza humu Maine, watoa huduma wengi wapya wa Maine walihamasishwa kwa haraka kuungana katika mtandao, wakitoa mfumo wa utetezi, kukuza ushirika, kushughulikia mahitaji ya haraka iliyo jitokeza, pamoja na kutoa usaidizi wa lugha na utamaduni wa kipekee unayofaa kuhusu habari ya Covid-19”, alivyosema Fatuma Hussein, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Rasilimali cha Uhamiaji cha Maine, aliye hojewa kwa simu.

Wataalam wa magonjwa ya kuambukizwa na wataalam wa afya ya umma hawakushangazwa na tofauti kubwa katika viwango vya maambukizi miongoni mwa tofauti za makabila. Kulingana na wavuti ya kitaifa wa CDC, “Historia inaonyesha kuwa magonjwa mazito na vifo vingi huwa zaidi kwa vikundi vya watu walio wa kabila chache wakati wa dharura za afya ya umma.” Tovuti hii inalaumu hali ya kiuchumi na kijamii waliomo kama vile hali ya kazi, ikiegemea msingi wa hali ya kiafya, inayo onyesha wazi utofauti wa kufikia huduma za afya, na hali tofauti ya maisha katika vikundi mbalimbali.

Idadi ya vikundi vya wafanyakazi vilivyoundwa katikati ya mwezi wa Machi ili zingatia mahitaji ya jamii za wahamiaji huko Maine wakati wa tatizo hili. Vikundi hivi walikutana kwa njia ya mtandao, wakiwashirikisha mawakilishi wa vikundi visivyo vya faida na vikundi vya ngazi za misingi kutoka pande zote za jimbo. Baadhi ya vikundi walihusika na mada maalum. Kwa mfano, walio wengi wamezingatia tatizo la kiafya lenyewe, mwanzoni sana ili kufikia mapema hitaji la COVID-19 kupimiwa, habari kutafsiriwa na wafanyikazi wenye ujuzi wa lugha nyingi na wa mambo ya afya na utamaduni, na wengine kukutana na kufuatilia ndani ya jamii wahamiaji wanapoishi na wanapofanya kazi kabla ya mukurupuko huu kujitokeza.

Vikundi vingine vime zingatia jinsi ya kupunguza pengo la fursa ya elimu iliyoko na inayoenea kati ya wanafunzi waliofaidika kidogo na wale ambao hawakupungukiwa na chochote kile. Bado wengine wamefanya kazi ya kuunganisha watu walio na maohitaji na rasilimali za utoaji chakula. Vikundi fulani ni maalum kwa mkoa, hushughulikia changamoto kitofauti katika kata tofauti. Kulingana na wanachama wa vikundi vya wafanya kazi, walio wengi wamefanya kazi katika kuanzisha hatua bora ya mawasiliano na uongozi katika idara tofauti kwenye utawala wa Mills, na washirika wao, pamoja na uongozi wa serikali za miji.
Kikundi cha New Mainers Working Group kimeendesha mkutano wa kawaida jimboni kwote ikilenga na kufanya kazi kama kikundi cha mwavuli kwa wengine wengi, pamoja na wawakilishi kutoka Kaunti ya Androscoggin, Bath / Brunswick, na Augusta, na pia eneo kubwa la Portland. Kikundi hicho kinajumuisha Chitam, Hussein, wawakilishi kadhaa kutoka Catholic Charities Huduma za ukimbizi na uhamiaji, pamoja na wengine wengi, kwa jumla ya wahudhuriaji wa kawaida wa watu15-20.

Kikosi cha New Mainer’s Emergency Response Task Force kiliundwa mwezi wa Machi ili kutumikia jamii wa Lewiston. Kikosi hicho cha Kazi kina mashirika wanachama10, pamoja na mawakilishi kutoka misikiti miwili na makanisa mawili, alieleza Abdulkerim Said, mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa New Mainers Health Initiative (NMHI), aliye zungumuzwa kwa simu. “Jamii kadhaa katika Kaunti ya Androscoggin zimepuuzwa na kuwa na changamoto ya rasilimali, kwa hivyo tulichagua kuzingatia Lewiston na Androscoggin,” alisema Said.

Abdulkerim Said, Director of New Mainers Public Health Initiative

Mnamo Machi tarehe 13, kikundi cha watu zaidi ya 80 wanaowakilisha mashirika mengi, na kulenga mahitaji ya kiafya ya jamii za wahamiaji wakati wa shida hii, walikutana na Daktari Nirav Shah, Mkurugenzi wa Kituo cha Maine cha Kudhibiti Magonjwa (CDC), kwa ombi lao. Mikutano na Kristine Jenkins na Jamie L. Paul, mijadala ya jamii kwa CDC, imeendelea tangu wakati huo, pamoja na mikutano mara kwa mara hivi karibuni, ili kujibu wasiwasi mkubwa ulio juu ya milipuko katika maeneo ya kazi ambapo wahamiaji wengi hufanya kazi, kama vile kiwanda cha chakula Tyson, na Bristol Seafood, na maambukizi ya jamii katika kaunti za Cumberland na Androscoggin. Daktari Shah amekutana nao mara kadhaa tangu Machi tarehe 13 na viongozi wa jamii ya wahamiaji na washirika wao wa mashirika yasio tafuta faida.

Kuongezeka, kwa kufikia urahisi wa kupimwa, kumepatikana kwa kupanua mawasiliano haya kwa wanamemba wa kuaminika wa jamii tofauti, na ushiriki na wafanyakazi wa afya hayo yakiwa mahitaji matatu yaliyotolewa mara kwa mara na viongozi wa jamii katika shughuli zao za uteteaji tangu Machi. Kadhalika, wamehimiza kwa nguvu ushiriki wa wafanyikazi wa kuwaendea jamii (CHOWS) katika kufikia jamii za wahamiaji walio katika uhitaji wa msaada.

Nélida R. Berke, mratibu wa Minority Health Program (Programu ya Afya ya Wachache), iliyoko ndani ya Idara ya Afya iliyo ndani ya Huduma za Afya ya Binadamu ya Jiji la Portland, alielezea kwa njia ya maongezi ya Zoom kwamba Wafanyakazi wa kuwaendea jamii (CHOWs) wanaelewa sana matatizo ya wagonjwa wao, mara nyingi hushirikisha maadili ya sawasawa, uzoefu wa kimaisha, ukabila wa kimsingi, hali ya kijamii na kiuchumi, na lugha. “CHOWs ni wanamemba wa jamii tunazo zihudumia,” alielezea. “CHOWs huokoa muda na pesa kwa mfumo kwa sababu watu watazungumza nao kwa urahisi, na wanapeana nao habari za kibinafsi ambazo hawawezi kuambia kwa urahisi kwa mtu ambaye si kutoka kwa jamii yao. Kwa wengine inabidi kwanza upange jinsi ya kufikia jamii, kuunda uhusiano – na hiyo inachukua muda mrefu. CHOWs tayari wanajulikana na wanaweza kuendesha na kumaliza kazi kwa haraka. ”

Lisa Tapert, Mkurugenzi Mtendaji wa Maine Mobile Health Program, alisema kama angependa kuona vituo vya kupima vimewekwa bila kuwaka katika jamii za wahamiaji, ili waweze kufikiwa na watu bila shida ya usafiri, wale ambao wanaweza kuwa hawajaunganishwa na ma daktari. Amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi na wa CHOWs na viongozi wa jamii za wahamiaji, ili kuhakikisha athari kubwa. “Ningependa kuona CDC inafanya kazi na mashirika kama Mano na Mano, Maine Access Immigrant Network, New Mainers Public Health Initiative, na wengine ili kujua ni wapi vipimo hivyo vinahitajika.” Akitarajia kutokea kwa mikurupuko ambayo imekuwa ikitokea katika wiki za hivi karibuni kwenye kazi za mashamba na mahali pengine, alisema kwa simu tarehe Mei 14, “Eti “ni suala tu la muda kabla ya kuzuka mipurupuko nyongezo ikiwa upimaji hautakuwapo.”

Fatuma Hussein, aliyeulizwa kwa njia ya simu tarehe Mei 20, alionyesha kwamba baada ya wiki kadhaa za mikutano na ujenzi wa ushirika ili kukuza muundo, Lewiston Auburn imo njiani kufikia jibu la pamoja iliyoratibiwa kwa ajili ya jamii zao.
“Tunao ushirikiano mzuri mahali hapa, na mawasiliano yanafanyika kwa ngazi za chini. Sote tunashirikiana katika jinsi ya kuzuia mikurupuko isiyo na maana, na ninataka kushukuru mifumo na washirika wetu”, alisema Hussein.

Wavuti ya Maine CDC umeorodhesha kesi chanya 1009 zilizopatikana katika Kaunti ya Cumberland, 337 katika Kaunti ya York, na 227 katika kaunti ya Androscoggin. Kazi za mishahara ya chini katika mahospitali, nyumba za wazee, nyumba za uuguzi, duka za mboga, na mahali pa kutengenezea mimea mara nyingi huwa mahala palipo patikana kazi kwa wahamiaji, ambao wengi wao hufika humu Maine kama wakimbizi au watafutaji wa hifadhi, bila leseni na shuhuda za kitaalam. Na kazi hizo, ambazo huchukuliwa kama ‘muhimu,’ ni za hatari kubwa kwa maambukizo. “Watu walio katika kazi hizi wako kwenye mstari wa mbele kwa virusi hivi. Hawawezi kukaa nyumbani, “Shah alisema katika mkutano na waandishi wa habari tarehe Mei 22.

Mikurupuko imetokea katika utengenezaji wa mimea kama vile Tyson Foods, Bristol Seafood, ambao huajiri wahamiaji wengi, na pia katika nyumba za wazee katika kaunti kadhaa.

Hali ya kuishi kwa vikundi vya watu wengi pamoja inatajwa na CDC kama inachangia kuongezeka kwa magonjwa kwa vikundi vya watu wenye shida wakati wa mikurupuko ya afya ya umma. Kwa sababu malipo ya nyumba ni ghali katika Maine, wafanyikazi wa mishahara ya chini mara nyingi huchangia makazi. Said amesema kama katika jamii yake watu wengi wanachangia nyumba moja na ana wasiwasi kuwa wanao pimwa na kuonekana wanao virusi vya ugonjwa huo hawana njia yoyote ya kujitenga na watu wengine walio nyumbani mwao.

Crystal Cron, Musimamizi wa Presente! Maine, kikundi cha utetezi kwa jamii ya Latinx huko Maine, pamoja na Said na wengine walio katika vikundi hivyo vya kazi, wamekuwa wakipaza sauti za utetezi wao kwa CDC kupanua ufafanuzi wa mipangilio ya kukusanyika ili kujumuisha magorofa ya makazi zilizo na vikundi vingi vya watu.

“Wanajumuiya wengi hukaa familia nne hadi tano katika ghorofa moja, na kila familia inachangia chumba cha kulala, na hiyo inafanya kuwa karibu haiwezekani kuheshimu umbali wa kijamii. Ikiwa unaugua na unahitaji kujitenga na familia yako, utaenda wapi? ” alisema Cron.

Dk. Shah alirudia kusema mara kwa mara kwa waandishi wa habari kwamba maambukizi ya nyumbani ya COVID-19 ni maarufu katika Uenezaji wa virusi huko Maine, na kwa kuwa usambaaji wa upimaji unaopatikana sasa, anahimiza kujipimisha kwa wale ambao walion na dalili, au ambao wame wasiliana na mtu ambaye amepimwa na kupatikana na ugonjwa. Mnamo tarehe Mei 19, mukurupuko ulitangazwa na CDC kwenye jengo la ghorofa namba 100 la State Steet huko Portland. Watu 200 walipimwa moja kwa moja kwenye ukumbi wa jengo hilo tarehe Mei 20, na matokeo ya vipimo hivyo yalikuwa yakisubiriwa tarehe Mei 21.

Suala la mwiba kati ya Daktari. Nirav Shah na wengi wa waandishi wa habari, miongoni mwa wengine, imekuwa kukataa kwake kwa kuripoti katika ngazi ya manispaa data za ukabila na kabila ambazo zimekusanywa na wataalam wa magonjwa. Daktari Shah ameelezea mara nyingi katika muhtasari wa waandishi wa habari wasiwasi wake kwamba kutolewa kwa data kama hizo kunaweza kuwa na hatari za kulenga wanamemba wa jamii hizo.
Chitam anakubaliana na msimamo wa Shah. “MIRC haiunge mkono kutolewa kwa data ya kikabila na makabila kwa ngazi za jiji / town kwa sababu haitabadilisha chochote kile tunachojua tayari juu ya athari isiyo na kipimo ya COVID-19 kwenye jamii za watu wa rangi, na tunaogopa kwamba itaweza kusababisha unyanyapaji na kutupa aibu kwa jamii zetu. Kiwango kikubwa cha maambukizo tunayoona ina msingi wa ukosefu wa usawa wa mfumo wa muda mrefu. ”

Alison Beyea, mkurugenzi mtendaji wa ACLU ya Maine, alinukulu katika barua aliyoiandika, “Katika jamii nyingi za Maine, kufichua habari ya afya inayotambulika ni sawa na kupiga kofi kwa mgongo wa mtu. Kutokana na hatari zinazowakabili jamii zilizo katika mazingira hatari, haswa jamii za watu wa rangi, serikali ina jukumu maalum la kulinda usalama wa kibinafsi kutokana na kufichuliwa kwa habari kama na hiyo. “ACLU inapendekeza data hizo kutolewa kwa kiwango cha serikali, badala ya kauti au kiwango cha jiji.

Claude Rwaganje

Katika kibarua pepe, Rachel Healy wa American Civil Liberties Union of Maine alisema, “Sisi sote tuna jukumu la kushughulikia tofauti hizi za sasa na sababu za kihistoria na za kisa cha mifumo yao – wakati kwa muda huo huo anapinga kwa nguvu sana jaribio lolote lile la kutumia data hii kwa kubagua, au kufanya dhuluma kwa hizo hizo jamii.”

Claude Rwaganje, Diwani wa Jiji la Westbrook, na mkurugenzi mtendaji wa ProsperityME, alisema, “Kutoa data kwa njia ya zip code hakutabadilisha chochote. Data tuliyo nayo tayari inatosha kwa kuonyesha kuwa kuna utofauti unao kuwa na msingi wa rangi ya ngozi, nayo inatosha kwa kutupatia picha kubwa ya jinsi jamii za walio wachache hazitunzwi vizuri. Hatutaki data hiyo kuwaathiri wale ambao tayari wameathiriwa. ”