Kufaili ushuru waweza kuwa ngumu kwa yeyote Marekani lakini inaweza kuwa changamoto hata zaidi kwa wakimbizi na wahamiaji. Wakimbizi na wahamiaji wengi hujumuishwa kama “wakaaji wageni” na wanahitajika kulipa kiwango sawa ya ushuru kama wazaliwa wa Marekani. Hata hivyo sababu kuna walakini katika sheria hii na sababu wingi wa ushauri kuhusu ushuru hauelekezwi kwa wahamiaji –ProperityME inashiriki haya maelekezo ya kawaida kusaidia wasomaji wa Amjambo Africa kufahamu zaidi wajibu wao wa kulipa ushuru na wakati na mahali pa kupata usaidizi.
1. kulipa ushuru na kufaili marejesho ya ushuru ni lazima.kukosa kufanya hivyo ina madhara makubwa.Ushuru usiolipwa huweza kuathiri hali ya uhamiaji wa mhusika.Tarehe ya kufaili ni Aprili 15,2021.
2. ”Wakaaji wageni”na ‘wageni wasiowakaaji”wana gharama tofauti ya ushuru kulingana na sheria za Marekani. “Wakaaji wageni” wanastahili kulipa ushuru kama wananchi wa Marekani. Wakaaji wageni wanajumuisha:
- a. Walio na kadi ya Green card na wakaaji wanaokubaliwa kisheria.
- b. Ambao wamepita “jaribio la uwepo kwa muda.”Hii inachanganya lakini kwa kawaida yeyote aishie Marekani zaidi ya siku 31 ya kalenda ya mwaka uliopo pamoja na siku 183 au zaidi za miaka miwili iliyopita,huwa amepita hili jaribio na hutozwa ushuru kama mkaaji kwa wakati huo.Aina zingine za visa ni tofauti na “jaribio la uwepo kwa muda.”
“Wageni wasio wakaaji”wanashughulikiwa tofauti na IRS na wana jukumika na mapato iliyopatikana Marekani. Walipa ushuru wasiofahamu hali yao vyema wanastahili kuwafikia wataalamu wa ushuru kuwaongoza. Kufaili katika hali ya utata yaweza kumfanya mtu kulipa ushuru mwingi sana au kidogo zaidi.
3. Mapato yote yapatikanayo katika mwaka wa kalenda unaopita ni lazima iripotiwe katika urejesho wa ushuru mapato yatengenezwayo katika nchi isipokuwa Marekani yaweza kupunguzwa kupitia ushuru za kigeni chini ya hali teule.
4.Wategemiaji wowote waitishao kufaidika kutokana na urejesho wa ushuru ni lazima waidhinishwe kuwa wakaaji wa Marekani na mlipa ushuru lazima awe mzazi au mlezi anaye kubakiwa kisheria wa watoto wowote waitishao kufaidika.Walipa ushuru hawawezi faidisha wanandoa ama watoto wanaoishi ughaibuni kutokana na marejesho ya ushuru. “Jaribio la utegemeaji” laweza kumsaidia mhusika kujua iwapo mototo amefaulu kufaidika.
- a. Lazima awe mmoja wa wanaoishi katika nyumba yako.
- b. Lazima awe mkaazi wa eneo moja kwa zaidi ya nusu mwaka.
- c. Lazima awe chini ya miaka 19, au chini ya miaka 24 na mwanafunzi wa kila wakati kwa muda isiyopungua miezi mitano. Wanaweza kuwa umri wowote wakiwa na ulemavu wa kabisa.
- d. hawawezi kujipatia zaidi ya nusu ya mahitaji yao
- e. Mtoto hawezi kufaili jumla ya mapato ya mwaka
5.Faili ushuru haraka iwezekanavyo. Wajiri wengi watapeana fomu za W-2 ama1099 katikati ya Januari. Wenye biashara ndogo wanastahili kusawazisha vitabu vyao vya biashara na kukusanya risiti za gharama zote za mwaka upitao kwa wakati huo.
6. Epuka ulaghai. IRS haipigi simu ,haitumi baruapepe wala kutuma jumbe za kibinafsi kwa walipaushuru.
7. Epuka kulipa zaidi ukifaili. Nyingi za marejesho ya ushuru huwa rahisi na haigharimu mamia ya madola kuandaa. Wahamiaji wengi huwa wame faulu kuandaliwa kwa ushuru bure kupitia programu ya CASH. Kujisajili kwa miadi ya kutembelea tawi ya karibu ya CASH Maine yaweza kuokoa wakati na hela za walipa ushuru wachini.
Hivi vipengele vinaweza kumsaidia mlipa ushuru kuukabili msimu wa ushuru kwa ujasiri. Walio na maswali wanaweza kuifikia ProsprityME kwa nakala za kusaidia na maswala yanayohusiana na ushuru.