naye Jean Damascene Hakuzimana
Wakati mkurupuko wa COVID19 ulikuwa unaharibu vikali nchi zenye nguvu na uwezo, miongoni mwao Marekani, Ufaransa, Italia, Uchina, na Uhispania, bara la Afrika, likiwa ni maarufu kwa milipuko ya mikurupuko kama Ebola, awali ilisajili kesi chache. Hivi karibuni, bara hili limeanza kuona ongezeko za kesi chanya.
Mnamo Juni 11, Afrika iliripoti jumla ya kesi 150,102 zikiwemo na kesi 4,815 kwa masaa 24 tu ya tarehe ya ripoti. Pia mnamo Julai 11, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilihesabu jumla ya vifo 3,593. Vifo 100 vikijitokeza kati ya masaa 24 ya kuripotiwa. Afrika ya Kusini na Nigeria waliongeza orodha hiyo na kesi 55, 421 na 13, 873 kwa mtawaliwa huo. COVID-19 iligunduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika katikati ya mwezi wa Februari.
Ripoti ya Kiafrika, mshirika wa Jarida Jeune Afrique, pamoja na machapisho mengine mengi, wamenadharia maandishi kadhaa ili kujaribu kuelezea kuenea polepole kusambazwa kwa COVID-19 kwa bara la Afrika. Kwa mwanzo, nchi nyingi barani Afrika zilitekeleza hatua kali za kinga mara moja, pamoja na nchi za Afrika Mashariki kama Rwanda, Uganda, na Kenya zilifunga kabisa mipaka yao na kuchukua mapema sana hatua zingine za kuizuia.
Pia, raia wa bara hilo kwa ujumla hawasafiri kwenda nje ya nchi kwa sehemu kubwa, walipunguza mawasiliano na maeneo ya ulimwenguni. Kati ya kesi chanya nchini Rwanda, idadi kubwa imelingana na watu wanaosafiri kutoka nchi za Asia au Magharibi, ambao waliingia Rwanda kabla ya kufunga mipaka yake ya angani na ardhini.
Zaidi ya hayo, bara hili lina tasnia nzuri ya nguo, ambayo hutoa masks ya nguo, na mfumo wa matunzo ya kiafya inayotumiwa kuzuia wingi wa mikurupuko kama vile Ebola. Ripoti ya Kiafrika imependekeza kusema kwamba hali ya hewa ya kitropiki na ikweta ambako zipo nchi nyingi za Kiafrika ingeweza kuzuia kuenea kwa virusi hivyo, lakini mtafiti Pierre-Marie Girard, Makamu wa kiongozi wa Mambo ya Kimataifa kunako Taasisi ya Pasteur, wakiwa pamoja na wanasayansi wengine wengi, wamegundua kwamba coronavirus “Hujizidisha bila shida kwenye majira joto,” tofautisha na nadharia.
Hata bila COVID-19, Afrika imekuwa katika shida dhidi ya magonjwa, na nakala zimekuwa ziki ji swali juu ya utayari wa Afrika katika uhusiano ulioko kati ya vitanda vya kitengo cha utunzaji mkuu (ICU) na kadhalika. Nchi nyingi zina viingilizi chini ya tano kwa wakazi wote. Gazeti New York Times iliripoti mnamo Aprili kwamba, “Sudani ya Kusini, taifa lenye watu milioni 11, ina marais makamu (watano) wengi kuliko viingilishi (nne).”
Ongezeko la sisitizo lililo kwa upande wa wengi humu Marekani ili kufungua uchumi ni tofauti sana na ilivyo barani Afrika, ambapo raia hawawa shinikize sana viongozi wao, na zaidi wamezoea kufuata maagizo. Kwa kesi la COVID-19, hii inaweza kusaidia viongozi wa Kiafrika kuweka uchumi wao kufungwa, na kushinda vita dhidi ya virusi na majeruhi machache. Hata hivyo viongozi kadhaa, kama kwa Tanzania na Burundi, wamekuwa chini ya changamoto kwa kuweka namba za kesi kuwa siri, na kutekeleza hatua zisizo za kutosha kwa kinga.